Mwanamke Huyu Wa Miaka 109 Awajulisha Watu Siri Ya Kuishi Miaka Mingi

Mwanamke Huyu Wa Miaka 109 Awajulisha Watu Siri Ya Kuishi Miaka Mingi

Siri ya kuishi miaka mingi kulingana na wanawake walio weza kufikisha miaka 100 na zaidi ni kuchukua kiamsha kinyua kizuri na kufanya mazoezi mengi.

Una maswali kuhusu siri ya kuishi miaka mingi na kinacho wafanya watu kuishi hadi miaka 100 na zaidi? Hata kuishi miaka 90 bado ni jambo nzuri, ama sivyo?

Walakini, tumeona kuwa kipindi cha maisha cha binadamu wa wastani kime imarika pakubwa. Tuna utunzi wa kiafya bora zaidi pamoja na maarifa kuhusu lishe na mazoezi -  changio kuu katika maisha ya kudumu na marefu.

Masomo yana dhihirisha kuwa watu wenye furaha huishi muda mrefu na wana shuhudia afya bora ikilinganishwa na marafiki wao wasio na furaha. Lakini hakuna njia bora ya kung'amua siri za maisha marefu kuliko kuuliza mtu aliye na miaka zaidi ya karne moja.

Siri ya Jessie Gallan ya kuishi miaka mingi

siri ya kuishi miaka mingi

Patana na Jessie Gallan anaye toka Scotland na kufikisha miaka 109 mwezi wa Januari. Yeye ni mojawapo ya watu wazee zaidi huko Scotland na amefanya kazi kwa juhudi maishani mwake kutoka alipokuwa 13.

Wakati ambapo habari za STV zilimhoji, aliwaambia, "Sijawahi mtegemea mtu yeyote. Lakini niko sawa." Aliiambia STV siri zake za kuishi muda mrefu ni kuchukua kiamsha kinyua kizuri na kufanya mazoezi mengi. Lakini wakati ambapo The Times walipata nafasi kuongea na mwanamke huyu mwenye miaka 109 aliwaambia haya:

"Siri ya kuishi miaka mingi imekuwa kukaa mbali na wanaume. Wao tu ni shida tupu kuliko dhamani yao. Pia nilihakikisha kufanya mazoezi mengi, kunywa kikombe cha uji kila asubuhi, na sikuwahi funga ndoa.

Halafu kuna wengine ambao pia wali sema siri zao za kuishi muda mrefu... na kunaonekana kuwa na usawa!

Kuna Gladys Gough, mwanamke kutoka Britain aliye fikisha miaka 104 aliye sema:

"Sijawahi fanya ndoa ama kuwa na mwanamme. Huenda hilo lilichangia. Singekubali kutaabishwa na wanaume.

Pia kuna Leandra Becerra Lumbreras, ambaye ni mwanamke kutoka Mexico aliye ishi hadi umri wa miaka 127 aliye sema kuwa kuishi kwake kwa muda mrefu ni kufuatia kuto olewa. Lakini pia alichangia ulaji wa "chocolate" na kulala kwa siku nyingi muda mrefu.

Je, wanaume wengi wana nyonya maisha kutoka kwetu sisi wanawake?

siri ya kuishi miaka mingi

Kusema ukweli, baadhi ya wanaume huenda wakawa wa kimchezo, na amini baadhi yetu tuna fahamu tayari ilivyo tunapo danganywa na wenzi wetu, wanapo toka nje na kupata wenzi wengine, kukosa kutoshelezwa kihisia ama kushambuliwa kifizikia. Kwa njia fulani, kuna wanaume huku nje wanao penda kufikiria kuwa wanawake wako hapo kutumiwa kwa njia yoyote ile na kuwakosea heshima.

Kwa kuyasema hayo, sio wanaume wote walivyo hivi, na kuna dhahabu huku nje. Lakini hata hivyo, je wana tunyonya maisha kama wanawake? Huenda kwa kiwango kidogo, lakini ni kwa sababu wanaume kwa asili huwa tofauti nasi. Huenda pia wakawa na mjadala kuwa wanawake huwa nyonya maisha pia!

Baada ya yote, ukiongeza uraibu wako, uliyo yapitia hapo awali, ulezi na utu kwenye picha, nyote wawili hamta kosa kuvurugana. Niamini, ikiwa kungekuwa na mabishano machache kati ya wanandoa, wote wawili wangeishi muda mrefu!

Na kwa kuwa na furaha bila mchumba... ingekuwa vipi kuto jua harufu ya kichwa cha mtoto wako unapo mkumbatia mkilala? Ama kuto ona uso wa kushangaa wa bwanako alipo ona kichwa cha mtoto wako? Je, ungeyatupilia mbali hayo yote kwa siri ya kuishi miaka mingi na kuishi peke yako?

Sidhani. Lakini kuyaweka hayo mbali, wanaume, mnapaswa kuturuhusu kushinda baadhi ya vita ili tuishi muda mrefu kuwasumbua zaidi. Umesoma makala ya kuwa kusumbua kunakusaidia kuboresha maisha yako, siyo?

Vyanzo: People, Business Insider, WebMD

Soma Pia:

Written by

Risper Nyakio