Siri Ya Kupata Mtoto Mrembo: Mambo Muhimu Ya Kufanya!

Siri Ya Kupata Mtoto Mrembo: Mambo Muhimu Ya Kufanya!

Hakikisha kuwa ona ongeza vyakula tulivyo zungumzia kwenye lishe yako unapokuwa mjamzito ili kuongeza nafasi zako za kupata mtoto mrembo.

Ujauzito huwa kipindi chenye furaha kwa mama hata kama safari hii ya ujauzito ina panda shuka zake. Kuhakikisha kuwa mwanamke anakula lishe bora na yenye afya ni muhimu kwa afya ya mama na mwanawe. Katika safari hii ya ujauzito, mwili wa mama unahitaji virutubisho zaidi kuboresha afya ya mtoto. Angalau kalori 400-500 kwa siku yenye lishe yako katika trimesta ya pili na ya tatu. Vyakula hivi vyenye afya vitakusaidia kupata mtoto mrembo.

Lishe duni huenda ikamfanya mama kuongeza uzito mwingi na kufuatia hili mama kuwa katika hatari ya changamoto za kujifungua. Unapokuwa na mimba, unahitaji kuwa makini zaidi na unachokula ili mtoto apate virutubisho anavyo hitaji katika ukuaji wake. Hakikisha kuwa una zingatia lishe bora na yenye virutibisho tosha kwako na fetusi. Lishe bora ni muhimu kwa mama kupoteza uzito kwa urahisi baada ya kujifungua.

Orodha ya vyakula muhimu ili kupata mtoto mrembo

kupata mtoto mrembo

  1. Bidhaa za maziwa

Ulaji wa bidhaa za maziwa ni muhimu sana unapokuwa na mimba. Zinakusaidia kupata protini zaidi na kalisi ambazo ni muhimu katika ukuaji wa fetusi. Hakikisha una kunywa angalau glasi moja ya maziwa kwa siku, ama una kunywa maziwa ya bururu.

2. Mayai

Mayai ni vyanzo bora vya vitamini, protini na madini. Protini zilizoko kwenye mayai zinafanya yawe bora kwa mtoto anaye kua na kusaidia katika kurekebisha seli mwilini mwake. Pia, kuwepo kwa choline kwenye mayai kuna saidia katika ukuaji wa ubongo na mfumo wa neva wa fetusi.

3. Ndizi

Ni muhimu kwa mama kuongeza tunda hili kwenye lishe yake. Ni chanzo kizuri cha folic acid, potassium, vitamini B6 na kalisi. Pia lina saidia katika kuboresha nishati.

4. Viazi vitamu

Viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha beta-carotene inayo badilishwa kuwa vitamini A mwilini na kusaidia katika ukuaji wa seli na tishu. Pia inasaidia katika kuboresha kinga na uwezo wa kuona. Bila shaka ni muhimu kwa afya ya mtoto na mama.

5. Njugu

Njugu zina ladha na wingi wa ufuta wenye afya. Kwa sababu hizi, ni chaguo bora la kula kama kitamu tamu katika ujauzito. Zina protini, omega-3 fatty acids na fiber, zote ambazo ni muhimu katika ukuaji wa mtoto.

6. Sharubati ya machungwa

Ina folate, vitamini C na potassium. Na ina hakikisha kuwa mtoto ana pata virutubisho muhimu na kum-epusha na changamoto za kuzaliwa. Ina ongeza uwezo wa mwili wa mtoto kutumia iron. Ongeza glasi moja ya sharubati ya machungwa kwenye kiamsha kinywa chako.

7. Mboga za kijani

kuchelewa kwa kipindi cha hedhi

Mboga za kijani zina virutubisho vingi na ni muhimu katika kuulinda mwili dhidi ya maradhi mengi.

Hakikisha kuwa ona ongeza vyakula tulivyo zungumzia kwenye lishe yako unapokuwa mjamzito ili kuongeza nafasi zako za kupata mtoto mrembo.

Chanzo: Healthline

Soma Pia:Ratiba ya lishe bora ya kuzingatia nchini Kenya ya mama mja mzito

Written by

Risper Nyakio