Mavazi ya mazoezi yanahitaji kusafishwa kwa umakini ili kuhakikisha kuwa uchafu wote umetoka na yana harufu ya kuvutia unapoyavalia tena. Kuvalia mavazi yanayonukia vyema unapofanya mazoezi kunakupatia motisha ya kufanya mazoezi zaidi. Tunaangazia siri za mavazi ya mazoezi usizofahamu na ambazo zitasaidia mavazi yako kunukia vizuri na kudumu kwa muda mrefu.
Siri za mavazi ya mazoezi usizofahamu

- Wacha mavazi yapumue kabla ya kuyasafisha
Wazo la kwanza baada ya kutoka mazoezi ni kuongeza mavazi uliyofanya mazoezi nayo kwenye tita la nguo chafu. Kuyawacha yapigwe na upepo kwanza kabla ya kuyasafisha kutafanya mchakato wa kuyaosha uwe rahisi. Baada ya kufanya mazoezi, anika mavazi hayo mahali ambapo yanaweza kukauka kwanza kabla ya kuyaongeza kwenye tita la mavazi machafu.
2. Kutumia siki ama vinegar
Siki inatumika sana sana katika mapishi. Kwa wasiojua, siki ni muhimu katika kuondoa harufu mbaya. Ili kuhakikisha kuwa unalinda mavazi yako ya mazoezi na kuwa hayana harufu mbaya, tumia siki. Njia bora ya kuitumia ni kuiongeza kwenye maji, kisha kuweka mavazi yako kwa maji hayo. Fanya hivi dakika 30 kabla ya kusafisha.
3. Safisha mavazi ya mazoezi kutumia maji baridi
Kusafisha mavazi na maji moto hasa mavazi ya mazoezi huwa na athari hasi kwa nyenzo za mavazi yale. Huenda yakakunjana na kupunguza urefu wa kimaisha wa mavazi yale. Ili kurefusha maisha ya mavazi ya mazoezi, tumia maji baridi unapoyasafisha wakati wote.

4. Anika mavazi kwenye jua
Ni muhimu kuanika mavazi ya mazoezi kwenye jua. Tofauti na kukausha kutumia mashine, jua, huweza kukausha mavazi vyema na inavyohitajika na kuyawezesha kudumu kwa muda mrefu.
5. Safisha kutoka upande wa ndani
Kusafisha mavazi kutoka upande wa ndani husaidia kudumisha rangi. Pia,, kusafisha mavazi kwa njia hii kunasaidia kuyang'arisha zaidi. Hasa kwa sababu uchafu mwingi upo katika upande wa ndani.
Tumia siri tulizoangazia ili kunufaisha mavazi yako ya mazoezi na kukuwezesha kuyatumia kwa muda mrefu zaidi.
Soma Pia: Mambo 5 Muhimu Unayo Paswa Kufanya Kabla Ya Kufanya Mazoezi