Siri Za Kupata Ngozi Yenye Afya Na Inayo Ng'aa

Siri Za Kupata Ngozi Yenye Afya Na Inayo Ng'aa

Sababu kama vile jua kali na kuwa kupata uchafu huathiri ngozi yako. Kuna siri za utunzaji wa ngozi zitakazo kusaidia.

Ngozi ndiyo sehemu kubwa zaidi ya mwili wote, na kazi zake ni kama vile kulinda mwili dhidi ya kupoteza maji ama kupata maambukizi. Kazi zingine muhimu za ngozi ni kama vile utengenezaji wa vitamini D ya mifupa yenye afya na kuthibiti joto. Kufuatia mabadiliko ya hali ya anga, hali hubadilika kutoka joto jingi hadi baridi nyingi. Sababu kama vile jua ama kuwa kwa mfichuo wa vumbi, huenda zika athiri ngozi yako na kuifanya iwe vigumu kwa ngozi yako kung'aa. Ila kuna siri za utunzaji wa ngozi ambazo zina weza kusaidia kupata aina hii ya ngozi.

Ngozi yako ina seli nyingi. Seli za ngozi ya nje hukua na kisha kufa. Kila mtu ana seli za ngozi zilizo kufa. Zinapo kaa kwa muda mrefu juu ya ngozi yako, utaanza kushuhudia kuvunja kwa uso, madoa, vidonda na ngozi iliyo kauka.

Siri Za Utunzaji Wa Ngozi

siri za utunzaji wa ngozi

Hapa kuna siri za utunzi wa ngozi ambazo zinaweza kusaidia kupata na kuhakikisha kuwa ngozi yako ina afya na kung'aa wakati wote.

  • Shea Butter

 

siri za utunzaji wa ngozi

Iwapo unatafuta ngozi laini, unapaswa kuwa na bidhaa hii nyumbani mwako. Ngozi yako ina fichuliwa kwa vitu tofauti kama vile kemikali, hii ndiyo maana vitamini E ni muhimu sana. Ni antioxidant mwafaka inayo punguza radicals zinazo tolewa mwilini baada ya ngozi kufichuliwa kwa kemikali, na bidhaa zinazo kuwa na shea butter zina imarisha utoaji wa collagen.

Pia ina linda ngozi dhidi ya miale ya UV (SPF 6) na kuipatia ngozi fatty acids na virutubisho vinavyo hitajika kwa utoaji wa collagen.

Pia, mbali na faida za vitamini E za kupunguza uzee, pia inasaidia kulinda ngozi yako kutokana na athari za kuharibu za miale ya UVA na UVB ya jua. Hii inaweza husishwa na uwezo wa antioxidant wa shea butter inayo ipatia ngozi nguvu na kuilinda dhidi ya uharibifu. Lakini, shea butter sio mbadala wa sunscreen.

  • Turmeric na sabuni nyeusi 

Black soap

Turmeric ni nzuri kwa ngozi. Inasaidia kutoa madoa na kuifanya ngozi mpya imee. Sabuni nyeusi ni maarufu kwa kazi kubwa inayofanya kwa ngozi nyeusi. Kwa sababu ya antioxidants na vitamini A na E kwenye sabuni nyeusi za ki Afrika, inafanya kazi njema ya kutoa matatizo ya ngozi kama vile ngozi iliyo kauka, madoa ya ngozi na eczema.

Kwa hivyo, sabuni nyeusi ya ki Afrika inapo changanywa na turmeric, inafanya kazi nzuri kwa ngozi. Na kuiwacha ngozi yako ikiwa na unyevu tosha na kung'aa kila siku.

  •  Mafuta ya Palm Kernel 

Palm Kernel Oil

Nchini nyingi, hali ya anga inayo kaa ikibadilika mafuta, uchafu na vitu vingine vinavyo kusanyika kwenye ngozi yako unapokuwa ukifanya kazi zako za kila siku. Hii inaifanya ngozi yako kuwa ngumu na kuiwacha ikiwa na shimo za ngozi kubwa kuliko za kawaida. Athari yake ni kuwa na seli za ngozi zilizo kufa kwenye uso wako. Na iwapo hakuna kitakacho fanywa kuzitoa, huenda ukajipata na vidonda kwa ngozi wakati wote.

Ili kutoa seli za ngozi zilizo kufa, ni muhimu kutumia bidhaa za kutoa seli zilizo kufa al maarufu kama exfoliater. Pia, kuosha kwa undani hutoa uchafu unao baki kwenye ngozi yako. Hii ndiyo sababu unahitaji mafuta ya palm kernel. Pia, iwapo una kusudia kutoa kuto ng'aa kwa ngozi yako, mafuta haya yatasaidia sana.

Kitu muhimu cha kufahamu unapo tumia bidhaa hizi ni kujua aina ya ngozi yako. Watu wengi hawana ujumbe huu. Kuna baadhi ya njia chache za kufahamu aina ya ngozi yako unapokuwa nyumbani, bila kutatizika sana.

Pia, iwapo ngozi yako ina matatizo yasiyo isha ama inakaa kana kwamba kuna kitu kisicho cha kawaida, ni wakati wa kumtembelea daktari wako.

Soma pia: Five Reasons Your Facial Skin Isn’t As Beautiful As It Should Be

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio