Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Lini Wakati Bora Zaidi Kupata Mimba?

3 min read
Lini Wakati Bora Zaidi Kupata Mimba?Lini Wakati Bora Zaidi Kupata Mimba?

Kubeba mimba huwa sio rahisi kila wakati. Ila kwa kuzingatia staili za kupata mimba hapa juu utagundua kuwa ni jambo lisilo ngumu.

Pale unapotaka kushika mimba haraka unagundua  kwamba kufanya tendo la ndoa ni zaidi ya kufurahia na kukidhi matamanio ya mwili. Unaelewa  kuwa  unahitaji kufanya vizuri kitandani ili  kuongeza chansi zako za kupata mimba. Hakuna njia ambazo ni asilimia 100% ila kujua wakati gani wa kushiriki tendo la ndoa na staili za kupata mimba hurahisisha mambo.

Staili Za Kupata Mimba

staili za kupata mimba

Jambo la kwanza na la msingi ni kuelewa kuwa kuna siku ambazo mwanamke huweza kupata mimba kwa urahisi. Hizi siku hujulikana kama siku za rutuba za mwanamke. Hizi ni siku ambapo yai la mwanamke huweza kuachiliwa kutoka kwa ovari. Pia hujulikana kama ovulation.

Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote. Isipokuwa  kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba  au mwanamume wake ana matatizo.

Utazijuaje Siku Hizo?

Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako wa hedhi. Kuna aina tatu za mzunguko. Mzunguko mrefu unaochukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao.

Unajuaje Mzunguko Wako?

Hesabu siku tangu siku ya kwanza uliyopata siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa  uchukue miezi mitatu mpaka sita ukihesabu ili ujue kwa uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki.

Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu hizo zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata28…maana yake wewe una mzunguko wa siku 28.

Umuhimu wa tendo la ndoa katika ndoa

Siku Za Hatari Ni Zipi?

Siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita. Hapa ndipo watu wengi wanachanganyikiwa na kupata mimba. Mfano kama mzunguko wako ni wa kawaida  siku 28, chukua 28 toa 14 utapata 14.

Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14. Lakini kwa kuwa mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano ndani ya mwili wa mwanamke na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24, basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari.

Dalili Uko Kwenye Siku Zako Za Hatari

Lengo ni mbegu ya kiume ikutane na yai la mwanamke ili urutubishija ufanyike na mimba itungwe. Dalili kuwa yai limeachiliwa huwa:

  • Kubadilika kwa ute. Kwa kawaida mama mwenye afya nzuri hutokwa na ute ukeni mwake. Ila yai linapoachiliwa huo ute hubadilika na kuwa mzito na mweupe kama eneo jeupe la yai
  • Kupanda kwa joto la mwili(basal body temeperature).  Joto la mwili huongezeka taratibu  baada ya ovulation. Unaweza kupima mabadiliko ya mwili kwa kutumia kipima joto asubuhi baada tu ya kutoka kitandani. Ili kukupa uhakika fuatilia mizunguko mingi ya hedhi upate siku iliyo sahihi
  • Ovulation kits. Unaweza kutembelea duka la dawa kupata vifaa ambavyo hupima mkojo kujua mabadiliko ya homoni kwenye kipindi cha ovulation

Kubeba mimba huwa sio rahisi kila wakati. Ila kwa kuzingatia staili za kupata mimba hapa juu utagundua kuwa ni jambo lisilo ngumu.

Chanzo: Healthline

Soma Pia:Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Ya Kushika Mimba Kwa Urahisi Katika Miaka Ya 30’s

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Lini Wakati Bora Zaidi Kupata Mimba?
Share:
  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it