Ongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation

Ongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation

Kwa wanawake wanao tatizika kupata mimba, kujua siku yako ya kuovuleti itakusaidia kufahamu siku ambapo una dirisha kubwa ya kupata mimba.

Kupevuka kwa yai ambako kuna julikana kama ovulation ni pale ambapo yai moja ama zaidi katika mwili wa mwanamke yana achiliwa kutoka kwenye ovari (mfuko wa mayai). Hufanyika mara moja katika kila mzunguko wa hedhi wa mwanadada. Ovari ya mwanamke ina mayai kati ya 15-20 kila mwezi. Yai lililo zaidi hutolewa na kuwachiliwa kutoka kwa ovari hadi kwa fallopian tube ama mirija ya uzazi. Ni vyema kufahamu kuwa mwanamke ana ovari mbili, upande wa kulia na kushoto. Kila mwezi ovari moja huachilia yai. Hakuna mpangilio mahususi wa upande utakao achilia yai mwezi fulani, ila, haya yote yana tendeka bila mpango wowote ule. Na unapo fahamu mzunguko wako wa hedhi, unaweza tumia style za kupata mimba ili kuongeza nafasi zako za kutunga mimba.

Jinsi ya kupata mimba katika ovulation

styles za kupata mimba

Wakati huu ndio bora zaidi kwa wanandoa wanao jaribu kutunga mimba. Kufanya ngono isiyo salama siku mbili ama tatu kabla ya siku ya kupevuka kwa yai, kuna wapatia nafasi zaidi ya kupata mimba. Manii yana uwezo wa kudumu kwa siku 3-5. Yai likipatana na mbegu yenye afya, kutunga mimba kuna tendeka.

Ovulation inatokea wakati upi?

Kwa watu walio na mzunguko wa hedhi wa kawaida wa siku 28, siku yao ya kuovuleti huwa siku ya 14 baada ya hedhi yao kuisha na kabla ya kipindi cha hedhi kijacho.

Siku ya kuovuleti huwa siku 14 kabla ya kuanza kwa kipindi kinacho fuata cha hedhi. Kwa hivyo kama ungependa kujua siku yako ya kuovuleti ni gani. Chukua mzunguko wa hedhi kisha utoanishe na siku 14.

Wanawake huwa na mizunguko tofauti kutoka siku 21 hadi siku 28.

Je, dalili za ovulation ni zipi?

Sawa na kuanza kwa kipindi chako cha hedhi ama hata mimba, ovulation huwa na dalili. Na ukiwa makini utazitambua. Utaanza kushuhudia dalili hizi siku tano kabla ya siku ya kupevuka kwa yai. Dalili za kuovuleti huwa kama vile:

  • Kuhisi joto jingi mwilini
  • Kuumwa na upande mmoja wa tumbo ya chini
  • Chuchu kuwa laini ama hata kuuma
  • Hamu iliyo ongezeka ya kufanya mapenzi
  • Mabadiliko ya uchafu wa uke (ute wa uzazi)

Mabadiliko katika ute wa uke wa uzazi

When does ovulation start

Huu ni uchafu unao uona kwa chupi na huwa mwepesi na wenye rangi ya maziwa. Unapo ona kuwa kiasi cha uchafu wa uke unao toka ni zaidi ya kawaida, fahamu basi kuwa uko katika kipindi cha ku ovuleti. Na una mwanya zaidi wa kupata mimba. Hauna rangi na unavutika kati ya mikono ama karatasi ya kujipanguzia msalani.

Baada ya kipindi chako cha hedhi kupita, hali ya ute wa uke pamoja na kiasi chake hubadilika. Kazi yake ni kulinda na kuilinda mbegu inapo safari kutoka kwa mlango wa uke hadi kwenye mirija ya uzazi na baada ya kupatana na yai lina evuka. Tumia style za kupata mimba ili kuongeza nafasi zako za kupata mimba.

Soma pia:Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Ya Mapacha

Written by

Risper Nyakio