Kuna styles za kupata mimba ambazo wanandoa walio katika harakati za kutunga mimba wanaweza kutumia ili kupata mimba kirahisi. Katika makala haya, tuna angazia style za kupata mimba ambazo wanandoa wanaweza kutumia. Tazama!
Styles za Kupata Mimba

- Mtindo wa kufanya mapenzi wa missionary
Njia ya kwanza ya kuongeza nafasi za kutunga mimba ni kufanya mapenzi kwa staili inayofanya manii ya mwanamme yabaki kwenye mlango wa kizazi kwa muda zaidi. Ili yaweze kupanda hadi kwenye kizazi. Mtindo wa missionary huwa bora zaidi kwani mwanamke amelala kwa mgongo na kusafiri kwa manii hakuathiriwi.
- Kufanya mapenzi siku ya ovulation
Kufanya tendo la ndoa siku tano kabla ya siku za hatari ama siku ya kuengua kwa yai, humwezesha mwanamke kutunga mimba kirahisi. Katika siku ya ovulation, ovari huachilia yai lililokomaa, linapopatana na manii, yai hilo hurutubishwa na kiinitete kuanza kukua. Siku ya kuengua kwa yai huwa ya 14 kutoka siku ya kwanza ya kipindi cha hedhi kwa wanawake walio na mzunguko wa hedhi wa siku 28.
Kifaa hiki kinamsaidia mama kufahamu siku yake ya ovulation. Na kumwezesha kufanya mapenzi ya kimaksudi na lengo la kupata mimba. Kufanya mapenzi siku tatu kabla ya siku ya ovulation kunaongeza nafasi za mama za kushika mimba kirahisi.
- Kuzingatia ulaji wa lishe bora
Lishe huchangia pakubwa katika uwezo wa wanandoa kushika mimba. Mama anayelenga kushika mimba anashauriwa kujitenga na ulaji wa vyakula visivyo na dhamani mwilini. Kama vile vyakula vilivyo kaangwa kwa ufuta mwingi, kupunguza ulaji wa ngano na wanga zaidi. Badala yake, lishe yake inapaswa kuwa na viwango tosha vya virutubisho vyote na matunda na mboga kwa wingi.
- Kupunguza utumiaji wa vileo na sigara

Vileo na sigara huwa na athari hasi kwa juhudi za kushika mimba. Kwa wanaume, utumiaji wa vileo hupunguza idadi ya manii mwilini na kufanya iwe vigumu kwake kumpa mwanamke mimba. Koma kutumia pombe hadi mnapo pata mimba.
Kutunga mimba huwa juhudi za pamoja za mwanamke na mwanamme. Wawili hawa wanapofanya kazi kwa pamoja, huwa rahisi kwao kutimiza lengo lao kirahisi. Styles za kupata mimba tulizo angazia zinawasaidia wanandoa kupata mimba kwa kasi wanapozifuata kwa makini.
Twawatakia mema katika safari yenu ya kuwa wazazi. Je, una vidokezo zaidi vya jinsi ya kupata mimba kwa kasi? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mdogo hapa chini!
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Je, Kuna Uwezekano Wa Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Cha Hedhi?