Vyakula Vya Watoto Vya Soko Vina Sukari Nyingi Sana Kulingana Na WHO

Vyakula Vya Watoto Vya Soko Vina Sukari Nyingi Sana Kulingana Na WHO

Shirika la WHO lime tengeneza mwongozo wa lishe ya watoto. Ripoti hii inadhihirisha kuwepo kwa sukari nyingi kwenye vyakula vya watoto.

Shirika la World Health Organisation limeweka mwongozo wa lishe ya watoto wachanga. Ripoti hii imedhihirisha kuwa kuna sukari nyingi sana kwenye vyakula vya watoto vya soko. Kiwango hiki cha sukari kina ibua shaka, WHO ilisema.

 

Vyakula Vya Watoto Vya Soko Vina Sukari Nyingi Sana Kulingana Na WHO

Kupima kuwepo kwa sukari nyingi kwenye vyakula vya watoto

Mtihani uliofanywa na ofisi ya European ya UN kuhusu vipimo vya afya vya umma vilipima bidhaa za chakula 8,000 zilizo kwenye soko kwa miezi mitatu kati ya Novemba 2017- Januari 2018.

Uajenti huo ulipata kuwa asilimia 30 ya kalori kwenye ainai tofauti zilikuwa kutoka kwa sukari zote. Pia, 1/3 ya vyakula hivi vya watoto vilikuwa na ladha na sukari za kuongeza. Shirika hilo lilipima kuwepo kwa sukari nyingi kwenye vyakula vingi vya watoto kwa kupima ainai za vyakula vya watoto kwenye maduka 500 yaliyoko Israel, Bulgaria, Austria na Hungary.

Cha kuzangasha ni kuwa label zilizoko kwenye vyakula hivyo zina onyesha kuwa ziko sawa kuliwa na watoto wa umri wa miaka 6 hata kama sio kweli.

sukari nyingi kwenye vyakula vya watoto

Madhara yake

Shirika la World Health Organisation limeonya kuwa mvumo ulioko wa kuongeza viwango vingi vya sukari kwa bidhaa za kuuza ni shaka ya kiafya. Inaweza ongeza hatari ya kuwa na uzito mwingi wa mwili na kufanya watoto wapate shimo kwenye meno. Pia, huenda ika sababisha kufanya uchaguzi mbaya wa chakula na kuwa na hamu ya kula vyakula vya sukari maishani.

 

Kukabiliana na tatizo hili

1. WHO ime sisitiza msimamo wake wa kunyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza ya maisha ya mtoto

2. Shirika hili lina himiza nchi kutengeneza sheria za nchi ambazo zitapunguza kiwango cha ulaji wa sukari na pia kupiga marufuku kemikali za ladha na sukari kwenye vyakula vya watoto

3. Shirika la World Health Organisation linasema kuwa nchi zinapaswa kusimamisha mvumo wa kubadilisha maziwa ya mama na vitu vingine kama formula zenye ladha

4. Inapaswa kuwa jambo la lazima kuweka lebo/labels kwenye switi na candies kuonyesha kisicho sawa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitatu, ilisema WHO

5. Shirika lilihimiza kuwa watoto wanapaswa kulishwa vyakula vya nyumbani vyenye afya na virutubisho

 

Watoto wanahitaji lishe yenye virutubisho wanapokuwa wachanga na katika miaka ya mapema ya maisha yao. Ili kukuza ukuaji mzuri na maendeleo na kuhimiza afya bora na maamuzi bora ya lishe katika siku za usoni.

Kumbukumbu: WHO

Soma pia:Mwongozo Wa Vinywaji Vyenye Afya Vya Watoto Kuepuka Uzito Mwingi Kwa Watoto

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio