Supu Ya Karoti Yenye Ladha Na Afya Kwa Familia Na Watoto Wako

Supu Ya Karoti Yenye Ladha Na Afya Kwa Familia Na Watoto Wako

Kuongeza supu ya karoti kwa lishe ya watoto wako kuta wahimiza kula chakula.

Je, unatafuta njia ya kuongeza mboga zaidi katika lishe ya watoto wako? Maandalio haya ya jinsi ya kutengeneza supu ya karoti ndiyo unayohitaji.

Supu ya nyanya ni mojawapo ya supu zinazo julikana zaidi, ila, iwapo ungependa kujaribu kitu kingine kipya, supu ya karoti ni wazo la busara. Mbali na kuwa na ladha na afya, ni mbadala mwema wa supu ya nyanya na inaweza tengenezwa pamoja na wali ama mihogo.

Nyanya ni za msimu na kwa mara nyingi huwa na bei ghali, ila karoti ni za bei nafuu na zinapatikana kwa urahisi. Karoti zinaweza tumika kutayarisha vitu kama salads za mboga, meat pie, wali wa kukaangwa, supu ya karoti, carrot sauce na karoti za kukaangwa. Hapa ni jinsi ya kupatia karoti nafasi kwenye jiko lako na maandalio ya supu ya karoti yanayo fuata:

Jinsi Ya Kutengeneza Supu Ya Karoti

carrot stew

Picha: Afrolems

      Viungo

 • 500g karoti
 • 300g nyama ya ng’ombe
 • 2 vitunguu vya wastani
 • 1 kijiko cha shallot kilicho kaangwa
 • 2 pilipili hoho za kijani ndogo
 • 3 pilipili hoho mbichi cha wastani za ladha
 • 1 kijiko cha kiungo cha rosemary
 • 2 seasoning cubes
 • 1 kipande cha kitunguu saumu
 • 1 kijiko cha poda ya turmeric
 • 1 kijiko cha curry poda
 • Chumvi ya kuongeza ladha
 • 250ml mafuta ya kupika

Matayarisho ya supu ya karoti

carrot stew

 • Osha karoti zako vyema, kisha utoe ngozi kisha uzioshe tena kabla ya kuzi wavu.
 • Osha na ukate kitunguu chako, na pilipili mbichi kisha uweke kando.
 • Pia, osha nyama yako na uiweke kando.
 • Wavu turmeric yako mbichi na kitunguu saumu, kisha uoshe na ukate pilipili hoho yako ya kijani.

onions and pepper

Maagizo

 • Tia nyama iliyo safishwa kwenye chungu kitupu, kisha ongeza viungo vya rosemary, shallot iliyo kaangwa, kitunguu saumu mbichi, turmeric, chumvi na maji machache kisha uchanganye kwa kutumia mwiko kabla ya kuongeza moto.
 • Wacha nyama iive kwa dakika 7 ama 10 kwa moto wa wastani kabla ya kutoa.
 • Mwaga mafuta ya kupika kwenye chungu kitupu na upashe joto kwa dakika mbili, kisha ongeza kitunguu kilicho katwa na uchanganye, kabla ya kuongeza karoti zako zilizo waviwa na uchanganye. Pika karoti hadi maji yakauke.
 • Kisha ongeza pilipili, viungo vya ladha, nyama, changanya na ufinikie na uwache kwa dakika 20. Baada yake, ongeza chumvi, maji kwa unene unao kupendeza, changanya, funika na uwache kwa dakika zingine 5.
 • Hatua ya mwisho ni kuongeza hoho za kijani zilizo katwa, kisha uchanganye na uwache kwa dakika mbili kabla ya kuzitoa kwenye moto.

Furahikia supu yako ya karoti na wali, ndizi, mbivu ama mbichi ama mihogo mieupe.

Soma Pia: Here’s How To Cook Stew With Goat Meat Naija Style

Chanzo: www.adasrecipes.com

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio