Jinsi Ya Kupika Supu Ya Konokono

Jinsi Ya Kupika Supu Ya Konokono

Nyama ya konokono ni mojawapo ya nyama bora zaidi ila baadhi ya watu wanaogopa kuzila. Matayarisho haya yata hakikisha kuwa mapishi yako ya nyama hii yana pendeza.

Konokono wana ladha na virutubisho. Konokono tunaye ongelelea hasa ni wale wakubwa wanao fahamika kama nyama wa Congo. Ni vigumu kupata sherehe ya Kinigeria isiyo kuwa na supu ya konokono wa pilipili kwenye vyakula. Mwenyeji mwema atakua na chakula hiki cha kuwalisha wageni wake wa tabaka la juu.

snail sauce

Chanzo: answeresafrica.com

Ina ripoti kuwa wauzaji wa vilabu huuza vileo zaidi wanapo wauzia wateja wao konokono moto zenye pilipili. Hasa katika vilabu vingi Nigeria, hiki ni chakula ambacho hutakosa kwenye vilabu vingi. Bila shaka konokono mwenye pilipili ni mojawapo ya vitamu tamu vya tabaka la juu vinavyo pendwa zaidi.

Sababu kwa nini unapaswa kula nyama hii

Iwapo uko miongoni mwa watu wachache ambao lazima washa wishiwe kabla ya kujaribu nyama ya konokono, hii ndiyo sababu kwa nini ni nzuri kwako. Ina viwango vikubwa vya protini na ufuta mdogo. Pia ina vitamini E, B12, A, na K. Pia ni chanzo kizuri cha iron. Watu wanao taka kupunguza ulaji wao wa nyama nyekundu wanaweza jaribu konokono.

Nyama ya konokono inaweza pikwa kwa njia nyingi. Unaweza ongeza kwa supu ama rojo ama hata kula baada ya kukaanga huku ukingoja chakula chako kiive.

Walakini, kuna baadhi ya tamaduni ambazo ulaji wa konokono haukubaliki.

Vidokezo vya kupika supu ya konokono

Kabla ya kuanza matayarisho yako, kuna vitu vichache ambavyo unapaswa kujua iwapo unapika chakula hiki kwa mara ya kwanza.

• Unapotoa konokono kutoka kwa maganda, hakikisha kuwa hakuna chembechembe za maganda zinazo baki kwenye nyama

• Osha na uhakikishe kuwa utelevu umeisha kabla ya kuanza kupika

• Unaweza toa utelevu ule na chumvi, garri iliyo kauka ama alum

• Iwapo unatumia alum kutoa utelevu ule, hakikisha kuwa una suuza konokono asafike

• Jaribu usipike zaidi; inapaswa kuwa na ugumu kidogo unapokula

• Chagua konokono wa wastani ama wakubwa

snail sauce

Chanzo: dobbyssignature.com

Viungo

10 onokono 10 wakubwa
I kitunguu cha wastani kilicho katwa
2 pilipili hoho zilizo siagwa
1 viungo vya ladha
Chumvi
1 kikombe cha nyanya zilizo changanywa na pilipili (tomapep)
½ kikombe cha mafuta ya kupika
Pilipili hoho nyekundu na za kijani

Jinsi ya kupika rojo wa konokono wa pilipili

supu ya konokono

Picha: Pinterest

  • Hatua 1 – Kuosha konokono

Toa konokono kutoka kwa ganda, na uwe makini kutoa kila sehemu ya ngozi/ganda ngumu

Safisha nyama ili kutoa sehemu inayo teleza, mchanga na uchafu

Suuza nyama hiyo kwa kutumia maji safi

  • Hatua 2 – Kupika nyama ya konokono

Weka nyama kwenye chungu kidogo na uweke maji tosha ya kuifunika

Ongeza chumvi kiasi kisha upike kwa dakika 10

Toa chungu motoni na ukaushe maji

  • Hatua 3 – Kupika rojo ya pilipili

Mwaga mafuta ya kupika kwenye chungu kisafi na upashe joto kwa dakika 2

Ongeza kitunguu kilicho katwa na ukaange kwa dakika 1

Ongeza nyanya zako (pepper puree), chumvi, na viungo vya ladha, kisha ukaange kwa angalau dakika 3

Ongeza konokono na uendelee kupika kwa dakika 5 ama zaidi

Rembesha kwa kutumia pilipili hoho

Zima jiko lako kisha upakue chakula chako, konokono wa roojo la pilipili.

Ungependa kuwapendeza wageni wako? Unaweza pakua chakula hiki kama cha kutayarisha mdomo unapokuwa na wageni!

Kumbukumbu: healthyEating.sfgate.com 

Soma Pia : Nigerian chicken pepper soup recipe

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio

Written by

Risper Nyakio