Kwa kawaida watoto wote hupitia hatua sawa tumboni mwa mama zao mwezi kwa mwezi. Hizi hatua huanza pindi mama anaposhika mimba hadi wakati wa kujifungua. Ukuaji wa mtoto haubagui iwapo ni mtoto wa kike ama kiume. Ila tutadadisi tabia ya mtoto wa kiume tumboni mwa mama yake.
Tabia Ya Mtoto Wa Kiume Tumboni

Ni wazi kuwa mtoto wa kiume hukua kwa haraka tumboni mwa mama ikilinganishwa na mtoto wa kike. Hivyo mahitaji yake ya chakula huwa juu. Hili linaweza kusababisha utapiamlo kwa mtoto. Pia inaeleza kwa nini mama akiwa anatarajia mtoto wa kiume hula chakula kingi.
Tofauti moja kuu katika ujauzito ni upande ambao mtoto huegemea. Mtoto wa kiume hujipandikiza kwa upande wa kulia wa uterasi. Hii ni ikilinganishwa na mtoto wa kike ambaye hujipandikiza kwenye upande wa kushoto.
Mtoto huanza kucheza katika trimesta ya pili. Lakini je, kati ya mtoto wa kiume na wa kike nani hucheza zaidi? Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mtoto wa kiume hucheza zaidi ya yule wa kike katika kipindi chote cha ujauzito. Ila wengine wanapinga na kusema hakuna tofauti kati ya tabia ya mtoto wa kiume tumboni.
Swala lingine huwa nani huweza kupiga teke kwa nguvu zaidi. Wengi hudhani kuwa mtoto wa kiume kwa vile ana nguvu huweza kupiga teke kwa nguvu. Lakini hakuna ushahidi wa kuonyesha hivyo. Watoto huanza kucheza katika trimesta ya pili na kuendelea hadi ya tatu.
Hatua Za Ukuaji Za Mtoto Wa Kiume

Katika trimester ya kwanza, hatua kama vile viungo muhimu hutengenezeka. Hivi ni kama vile ubongo, moyo, uti wa mgongo, macho, masikio, pua, mikono na vidole. Pia shingo na kope za macho huanza kutengenezeka.
Katika trimesta ya pili, mikono na miguu hukamilika, shingo inakamilika na mifupa inaanza kukomaa. Huanza kucheza tumboni na uzito kuongezeka. Huu wakati mtu huweza kuskia mipigo ya moyo ya mtoto. Vidole na kucha za mtoto hukamilika, mtoto huanza kulala na kuamka. Pia huanza kuskia sauti za nje na za mama.
Katika hii awamu ya mwisho ubongo wa mtoto hukamilika. Mboni za macho huanza kutanuka na uzito wake kuongezeka maradufu. Kucheza kunaongezeka na kwa nguvu zaidi, mifupa inakomaa na nywele zinakuwa zimeota.
Hakuna tofauti kubwa kati ya tabia ya mtoto wa kiume tumboni ikilinganishwa na ya mtoto wa kike. Hatua zao za ukuaji huwa sawia na tofauti ikionekana kwa mambo machache sana.
Soma Pia: Mama Anaweza Kufahamu Jinsia Ya Mtoto Kwa Kufuata Dalili Hizi Kuu Za Mimba Ya Mtoto Wa Kiume