Tatizo la kukosa usingizi hushuhudiwa na mamilioni ya watu kutoka sehemu tofauti duniani. Mtu anapokuwa na tatizo hili hushindwa kupata usingizi, kuendelea kulala, kuamka mapema asubuhi tofauti na ilivyo kawaida, kukosa kupata usingizi baada ya kuamka. Kukosa usingizi hakuathiri usingizi tu, mbali nyanja tofauti maishani mwako pia kama kikazi na kiasi cha ubora wako.
Kiasi cha usingizi kinachoshauriwa kuwa bora kwa afya ni kupata masaa manane ya usingizi kila usiku. Huenda mtu akatatizika na kupata usingizi kwa muda mfupi wa siku na wiki chache ama miezi mingi. Kuna sababu nyingi zinazoathiri uwezo wa kulala vyema ama kukosa usingizi usiku.
Tatizo la kukosa usingizi

Dalili za tatizo la kukosa usingizi
- Kuamka katikati ya usiku
- Kuamka alfajiri na mapema asubuhi
- Kutatizika kupata usingizi usiku
- Kuhisi uchovu baada ya kuamka
- Kulegea kazini mchana
Vyanzo vya tatizo la usingizi
Kukosa usingizi ama kutatizika kufanya usingizi kunaweza sababishwa na tatizo lingine unalopitia ama kuwa hilo ndilo tatizo la kipekee. Baadhi ya sababu maarufu zinazo sababisha kukosa usingizi ni kama vile:
1.Kusafiri: Unapozoea kulala wakati fulani kila siku, mwili wako hupata ratiba ya usingizi unaofuata, wa kulala na kuamka kila siku. Unaposafiri na kubadili mazingira yako, mpango wako wa kulala huvurugika na kuifanya iwe vigumu kwako kupata usingizi kama ilivyo kawaida kwako.

2. Kusongwa na mawazo: Msongo wa mawazo unaosababishwa na masuala ya kimaisha kama vile ya kikazi, mapenzi, fedha, familia na masomo yanaweza kufanya iwe vigumu kwako kulala baada ya siku ndefu shuleni ama kazini. Pia, matukio makubwa maishani kama kupoteza mtu unayempenda, ugonjwa, kuwachwa na mchumba ama kupoteza kazi kuna athiri uwezo wako wa kulala.
3. Kulala mchana: Jambo lingine linalofanya iwe vigumu kupata usingizi usiku ni kulala mchana. Unapokuwa na wakati wa ziada mchana, badala ya kulala, fanya jambo lingine la kupitisha wakati, kama kuandika, kuchora, kusoma kitu kipya ama kusoma kitabu. Kulala mchana kutafanya iwe vigumu kulala usiku ama kukufanya ulale usiku zaidi kuliko ilivyo kawaida yako.
Tatizo la kukosa usingizi pia huathiriwa na tabia hafifu za kulala kama kutumia simu kitandani, mazingira hafifu ya kulala, kutazama runinga kitandani, kucheza video simuni na kadhalika.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Faida 7 Za Kufanya Yoga Kwa Afya Yako