Unene Wa Kupindukia Kwenye Watoto: Wakati Ambapo Unapaswa Kuwa Na Shaka

Unene Wa Kupindukia Kwenye Watoto: Wakati Ambapo Unapaswa Kuwa Na Shaka

Sukari ndiyo chanzo kikubwa katika kusababisha uzito mwingi usio takikana. Sukari inapatikana kwenye sharubati ya matunda, ketchup, siagi za mkate ama mkate.

Unakumbuka wakati ambapo mtoto wako alikuwa amenenepa na ufuta kila mahali ulio mfanya atabasamu mara tu ulipomshika? Kwa sasa kwani mtoto wako amezeeka na ako shuleni, kuwa mnene huenda kukawa hakupendezi tena kulingana na viwango vya jamii na huenda pia akawa katika hatari kubwa ya kuwa na tatizo la uzito wa kupindukia katika watoto ama obese.

Ikiwa mtoto wako ana uzito mwingi, huku kuta athiri kivipi afya yake na unaweza fanya nini kumsaidia?

Athari za kiafya zinazo husishwa na tatizo la uzito wa kupindukia katika watoto

kumsaidia mtoto kulala

Kuna masomo ambayo yame onyesha kuwa watoto walio na uzito mwingi huenda waka tengwa kwa wengine na kuwa wahasiriwa wa unyanyaswaji.

Huku kuna weza athiri matokeo yao shuleni.

Athari zingine za kiafya ambazo zinaweza ibuka kutokana na uzito wa kupindukia katika watoto ni kama vile:

 • Kisukari
 • Hypertension
 • Marathi ya moyo
 • Saratani
 • Matatizo ya kupumua
 • Kutatizika kulala(sleep apnea)
 • Ugonjwa wa gallbladder
 • Maisha yaliyo fupika

Vyanzo ni nini hasa?

Kuna sababu tofauti ambazo zinaweza changia kwa tatizo la uzito mwingi kwa mtoto wako, kama vile:

 • Lishe isiyo na afya(kula vyakula vingi vilivyo chakatwa ama kula chakula kingi)
 • Maisha bila kusonga(kuto fanya mazoezi)
 • Geni
 • Homoni
 • Kufikiria sana ama mawazo mengi
 • Aina fulani ya madawa

Hiari za matibabu kwa watoto walio na uzito mwingi

maendeleo ya mtoto wa miezi mitatu

Ikiwa mtoto wako ana uzito mwingi ama obese, hapa kuna anuwai ya hiari ambazo unaweza tilia mkazo kumsaidia kukata uzito zaidi mwilini:

 • Kubadili lishe

Jaribu kupunguza vitamu tamu na vyakula vyenye sukari kutoka kwa lishe ya mtoto wako na umhimize kula matunda zaidi, mboga na nafaka nzima na pia kunywa maji mengi kila siku.

Sukari ndiyo chanzo kikubwa katika kusababisha uzito mwingi usio takikana. Sukari inapatikana kwenye sharubati ya matunda, ketchup, siagi za mkate ama mkate--kwa hivyo hakikisha unasoma maagizo kwenye karatasi za bidhaa kufahamu kiwango cha sukari kilichoko.

 • Ongeza shughuli za kifizikia na  mazoezi

Mkubalishe mtoto wako kutoka nje ya nyumba na afurahie kukimbia nje ili mtima wake upige na misuli isonge.

Ikiwa mtoto wako anakula kwenye kiti na kutizama runinga siku nzima ama kucheza video kwenye simu, hatatumia kalori za kutosha kwa siku ili kuwa na uzito wenye afya.

 • Matibabu

Daktari wako anaweza mpima mtoto wako kisha kumwandikia baadhi ya matibabu yatakayo msaidia kudhibiti uzito wake.

Matibabu haya lazima yaegemezwe na mabadiliko katika mtindo wa maisha na mazoea ya kula ili upate matokeo chanya.

 • Upasuaji wa bariatric

Upasuaji wa kupunguza uzito hufanyika kwa watu walio na BMI za angalau 37.5 na zaidi, kwani wana tatizo la uzito mwingi zaidi.

Aina hii ya upasuaji una utaratibu tofauti wa kupunguza uzito kama vile gastric banding ama gastric sleeve na gastric bypass. Hata kama upasuaji huenda ukaonekana kama uamuzi wa kasi kutatua tatizo la uzito kwa mtoto wako, lakini kwa wengine, huenda likawa ni jambo linalo hitajika na lenye manufaa kwa kipindi kirefu kwani uzito mwingi unaweza punguza maisha ya mtoto wako.

Soma Pia:Lishe Na Mazoezi Haya Yatakusaidia Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio