Je, Tawi Kali Linaweza Kutoa Mimba? Mambo Yote Unayopaswa Kujua Kuhusu Mmea Huu

Je, Tawi Kali Linaweza Kutoa Mimba? Mambo Yote Unayopaswa Kujua Kuhusu Mmea Huu

Yote unayo paswa kujua kuhusu tawi kali na ujauzito!

Umuhimu wa tawi kali wakati wa ujauzito haupaswi kuwa chanzo cha wasiwasi. Hii ni kama unajuwa kula kila kitu kwa viwango vinavyo faa. Kuna umuhimu mwingi wa matawi kali kwa wanawake wajawazito. Baadhi yake yame orodheshwa hapa chini, ila, kwanza, tuelewa matawi kali ni nini. Je, matawi kali ni nini, na tawi kali linaweza toa mimba?

Athari za Tawi Kali Kwenye Mwili: Matawi kali yanaweza toa mimba?

can bitter leaf abort pregnancy

Ni mmea unaopatikana katika nchi za Kiafrika. Mmea huu wa kipekee ni tofauti kwa sababu una ladha kali ya kuuma. Tawi kali linajulikana kwa majina tofauti nchini Nigeria. Baadhi ya watu wanalitambua kama ewuro, etidot, onugbu na mengineyo.

Ni kali sana kiasi kuwa watu wanatumia wakati mwingi wakiosha matawi ili kupunguza ukali wake kabla ya kuyatumia katika mapishi yao. Tawi kali pia ina faida za kimatibabu. Wataalum wa matibabu ya mimea wanaitumia kutibu hali kama vile shinikizo la damu, kisuri na maradhi mengineyo.

Tawi kali linaweza toa mimba? Faida zake

tawi kali linaweza toa mimba

Image of pregnant woman touching her belly with hands; Shutterstock ID 111643082; PO: redownload; Job: redownload; Client: redownload; Other: redownload

Unapokuwa mjamzito, madaktari wanakushauri kuwa makini na lishe yako. Hii ni kwa sababu baadhi ya vyakula vinaweza kuwa hatari kwa mama na mtoto. Iwapo unashangaa iwapo kula tawi kali ni salama na athari za tawi kali kwa ujauzito, kwanza unapaswa kufahamu matumizi ya kimatibabu ya mmea huu wa kufurahisha.

benefits of bitter leaf during pregnancy

 Kupunguza sukari ya damu

Tawi kali linapambana na athari za sukari mwilini. Baadhi ya watu hulichukua kupunguza kisukari na kukumbana na sukari kwenye damu.

Tawi kali na saratani

Tawi kali limethihirishwa kupunguza hatari ya saratani na kupunguza usambazaji wa seli za saratani kwa wale walio na saratani tayari. Hii hasa ni kweli iwapo una saratani ya prostate.

Kulingana na Majaribio ya Kibiolojia ya Februari 2005, wanawake wanaotaka kupunguza hatari za kupata saratani ya matiti wanaweza ongeza matawi kali kwa lishe yao na wafanye mazoezi ya kifizikia mara kwa mara.

Malaria

Sharubati ya tawi kali inaweza ponya magonjwa mengi kama vile malaria, joto jingi, pneumonia, typhoid na kadhalika.

Kupunguza shinikizo la damu

Viwango vya juu vya potassium vinavyo patikana kwenye tawi kali vinasaidia kukumbana na shinikizo la juu la damu. Kutafuna tawi hili ama kunywa sharubati yake mara nyingi kunasaidia kukumbana na hali hiyo.

Somo lililo chapishwa na Makala ya Chakula ya Biochemistry ilionyesha kuwa tawi kali ni nzuri sana kwa watu wanao kabiliana na tatizo la hypertension.

Uzazi

Tawi kali linasaidia na kutunga mimba. Kulingana na daktari Grace Johnson katika makala haya yaliyo chapishwa kwenye Guardian Nigeria, tawi kali linasaidia kuboresha afya yako ya kijumla, na kusaidia ovari kuachilia mayai yenye afya na kusawasisha homoni.

Bila shaka, tawi kali linaweza saidia kuimarisha uzazi kwa wale wanalo lila kwa kawaida.

Je, tawi kali linaweza toa mimba? Athari hasitawi kali linaweza toa mimba

  • Kupoteza mimba

Kula matawi kali mengi katika hatua za mwanzo za ujauzito huenda yakafanya upoteze mimba. Sehemu ya nyuma ya mti wa tawi kali iliyo kaushwa hasa, inaweza sababisha kubanwa katika ujauzito wa mapema.

Ni muhimu kujua kuwa hili linaweza tendeka pale tu ambapo mwanamke anakula kiasi kikubwa cha matawi makali. Ni salama kwa wanawake walio katika hatua za ujauzito uliokomaa kuyala kwa kuthibiti kiasi.

  • Indigestion ama kuto chakata chakula

Iwapo mwanamke mjamzito anakula kiasi cha juu cha tawi kali, ako kwa hatari ya kupata matatizo ya tumbo, kukosa maji tosha mwilini ama kuto chakata chakula. Katika kesi hii, huwezi tumia matawi haya kutibu hali hii kwani yamesababisha hali hii.

Ni muhimu kugundua kuwa ni vigumu ukala viwango hatari vya matawi makali kwenye supu. Hii ni kwa sababu watu wanapo safisha matawi haya kupunguza ukali wake kabla ya kuyaongeza kwenye supu, yanapunguza uwezo wa matawi haya. Kupunguza huku kuna yafanya kuwa rahisi kula chakula chako cha supu ya matawi makali bila shaka ya kula kiwango cha juu.

Walakini, iwapo unapenda sharubati ya tawi kali, uko katika hatari ya kunywa viwango vya juu. Unaweza furahia tawi kali yako unapoila kwa kuthibiti!

 

Kumbukumbu: Natural Remedy Lab

DrHealth.com 

International Journal of Environmental Research and Public Health

Soma pia: Bleaching during pregnancy: Is it safe?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio