Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Orodha Ya Tembe Za Kukusaidia Kupata Mimba

3 min read
Orodha Ya Tembe Za Kukusaidia Kupata MimbaOrodha Ya Tembe Za Kukusaidia Kupata Mimba

Unapo jaribu kutunga mimba, kuna mbinu nyingi ambazo wanawake hutumia kupata watoto, kama vile homoni na tembe.

Kwa wanawake wanao jaribu kupata mimba, daktari anaweza shauri tembe za kupata mimba. Kuchukua dawa za kiume bila kushauriwa na daktari wako hakutakusaidia kupata matokeo unayo tarajia. Hii ni kwa sababu baadhi ya madawa ya uzazi hutumiwa kutibu matatizo mengine.

Ugumba unaweza fanyika kwa wake na waume, hata kama baadhi ya wakati huenda ukaonekana kana kwamba ni tatizo kwa wanawake pekee. Kwa wake, tatizo huenda likatokea kufuatia vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida na matatizo mengine ya kiafya. Na kwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 35, wataalum wa afya wanashauri upate matibabu baada ya miezi sita ya kujaribu kutunga mimba.

Ugumba ni nini?

tembe za kupata mimba-

Wanandoa wanaweza semekana kuwa gumba ikiwa hawawezi tunga mimba baada ya kufanya ngono bila kutumia visuizi vyovyote vya kupata mimba. Shida huenda ikawa moja wao. Kuna uwezekano wa mwanamme kukosa kuchangia katika kutunga, ama mwanamke kuto weza kutunga ama kubeba mimba kipindi chote kinacho hitajika cha miezi tisa kisha kujifungua.

Aina ya tembe za kupata mimba

Kuna aina mbili ya tembe ambazo zinaweza saidia wanawake wasio weza kutunga. Baadhi ya dawa za kutunga zimetengenezwa kuharakisha wanawake wasio weza kupevua. Wakati wa kupevuka kwa yai, mwanamke huwa na 'rutuba' nyingi ya kizazi. Pia, kuna homoni ambazo mwanamke anapaswa kuchukua kabla ya uhamishaji bandia (artificial insemination) kufanyika.

Tembe za kutunga ujauzito

Tembe tunazo orodhesha zinatumika mara nyingi kusaidia kutunga mimba.

  1. Clomid ama Serophene

tembe za kupata mimba- Clomid

Kama una pevua (ovulate) kama unavyo paswa, daktari wako atashauri Clomiphene citrate. Dawa hii imetumika kwa miaka mingi, zaidi ya miaka 40 kutibu matatizo mbali mbali. Pamoja na mbinu zingine za uzazi kama vile njia za uzalishaji wa kusaidia, Clomid na Serophene zinatumika kufanya ovari zako kutengeneza mayai.

Mara nyingi, Clomid na Serophene husababisha hypothalamus na pituitary gland kujua ubongo wako. Kisha ubongo wako unatoa homoni inayo fahamika kama gonadotropin- homoni ya kutoa, homoni ya follicle-stimulating, na luteinizing hormone. 

Kipimo cha dawa

Milligramu 50 za clomiphene kila siku kwa siku tano ndicho kipimo cha kawaida. Baada ya kuanza kipindi chako cha hedhi, chukua tembe ya kwanza siku ya tatu, nne na ya tano.

Matarajio ni kuwa siku saba baada ya kuchukua tembe ya mwisho unaweza tarajia kupevuka kwa yai. Walakini, ikiwa hilo halitendeki, daktari wako anaweza kuambia uongeze kipimo.

Athari hasi

Athari zake huwa nyepesi. Lakini huenda ukawa na matatizo ya kuona, kujaa tumbo, kichefu chefu na kuumwa na kichwa.

  1. Homoni

Ikiwa madawa haya hayata fanya kazi kwako, daktari wako anaweza shauri homoni. Hapa kuna homoni chache za uzazi. Pia, zinachukuliwa kama shuti (shots).

Follicle-stimulating hormone (FSH)

Madawa haya huanza ukuaji wa mayai kwenye ovari. Dawa hizi ni kama vile Bravelle, Fertinex, Follistim, na Gonal-F. 

Human menopausal gonadotropin (HMG) 

Dawa hii inachanganya FSH na LH (homoni ya luteinizing). Zina husisha Menopur, Metrodin, Pergonal, na Repronex.

Human chorionic gonadotropin (HCG)

Homoni ya HCG ina changanyika na dawa zingine za uzazi na kusababisha ovari kuachilia yai. HCG huhusisha  Novarel, Ovidrel, Pregnyl, na Profasi. 

Ikiwa unajaribu kupata mimba na mwenzi wa kiume, mpeleke afanyiwe vipimo vya kizazi. Mara nyingi wanawake hudhani tatizo ni wao peke yao. Kujitibu peke yako bila mwenzi wako hakutasaidia ikiwa tatizo ni kutoka kwake.

Soma pia: Jinsi Ya Kulea Wasichana Shupavu Wenye Maarifa Wasio Jua Maana Ya ‘Siwezi’

Chanzo: Healthline

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Trying To Conceive
  • /
  • Orodha Ya Tembe Za Kukusaidia Kupata Mimba
Share:
  • Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

    Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

  • Je, Mwanamke Ana Uwezo Wa Kuamua Wakati Ambao Atapata Mimba?

    Je, Mwanamke Ana Uwezo Wa Kuamua Wakati Ambao Atapata Mimba?

  • Orodha Ya Vyakula Bora Vya Kukusaidia Kupata Mtoto Kirahisi

    Orodha Ya Vyakula Bora Vya Kukusaidia Kupata Mtoto Kirahisi

  • Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba

    Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba

  • Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

    Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

  • Je, Mwanamke Ana Uwezo Wa Kuamua Wakati Ambao Atapata Mimba?

    Je, Mwanamke Ana Uwezo Wa Kuamua Wakati Ambao Atapata Mimba?

  • Orodha Ya Vyakula Bora Vya Kukusaidia Kupata Mtoto Kirahisi

    Orodha Ya Vyakula Bora Vya Kukusaidia Kupata Mtoto Kirahisi

  • Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba

    Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it