Ni Salama Kwa Mama Mjamzito Kujihusisha Katika Tendo La Ndoa?

Ni Salama Kwa Mama Mjamzito Kujihusisha Katika Tendo La Ndoa?

Ngono ukiwa na mimba ni salama isipokuwa katika wiki za mwisho chache kabla ya kujifungua. Kwani prostaglandins katika manii husababisha kubanwa kusiko komaa.

Kuwa na mimba hakumaanishi kuwa una paswa kutupilia mbali tendo la wanandoa. Unaweza endelea kufurahia tendo la ndoa katika ujauzito bora una safari ya mimba yenye afya. Ikiwa una shaka kuwa matendo ya kitandani yanaweza athiri mtoto wako, ama ikiwa kuna mitindo ya ngono ya kuepuka katika ujauzito, soma zaidi!

Kwa hivyo, unapaswa kufanya tendo la ndoa katika ujauzito?

faida za kiafya za tendo la ndoa

Ndio! Ni kawaida kuhofia kuwa kuna jambo ambalo linaweza enda mrama, lakini ikiwa una ujauzito wa afya bila matatizo yoyote, haupaswi kuwa na uwoga wa uchungu wa uzazi usio komaa ama kuharibika kwa mimba. Mtoto ako salama nyuma ya kuta za uterasi, amniotic sac inamlinda ipasavyo. Hakuna sababu ya kuogopa kufika kilele katika ngono katika hatua hii ya maisha yako.

Hamu ya ngono katika ujauzito

Hakuna mimba ambayo ni sawa, na kwa hivyo, libido yako huenda ikawa juu katika ujauzito mmoja na kuenda chini katika mimba ingine. Mabadiliko haya katika hisia za ngono katika ujauzito ni kawaida. Kupenda ngono kwako huenda kukazidi kubadilika katika safari yote ya mimba. Unaweza anza na libido ya chini na kumalizia safari yako na libido ya juu.

Zungumza na mchumba wako kuhusu hisia zako za ngono wakati wowote ule kisha mjue mtakavyo endelea kama wanandoa.

Kuna wakati unapo paswa kutofanya mapenzi?

tendo la ndoa katika ujauzito

Kuna wakati ambapo ni jambo la busara kuto jihusisha katika tendo la kufanya mapenzi kwa ajili ya afya yako na ya mtoto wako.

  • Wiki za mwisho chache za ujauzito

Ngono ukiwa na mimba ni salama isipokuwa katika wiki za mwisho chache kabla ya kujifungua. Hii ni kwa sababu prostaglandins katika manii zinaweza sababisha kubanwa kabla ya wakati. Wanawake walio pitisha siku wanaweza anzia uchungu wa mama kwa kufanya mapenzi.

  • Unapo toa damu

Kutoa damu kunaweza ongezeka unapofanya mapenzi hasa kama una placenta iloiyo chini. Daktari anaweza kushauri ukose kufanya mapenzi kwa muda ili kuepuka hali yako kuwa mbaya zaidi.

  • Baada ya maji kuvunja

Ikiwa maji yamevunja tayari, huku kuna maana kuwa mtoto hapati ulinzi kutoka kwa amniotic sac. Kwa hivyo kufanya ngono kuna ongeza nafasi yake kupata maambukizi.

  • Watu walio na wapenzi wengi

Wanandoa walio na wapenzi wengi wanastahili kutumia kondomu ili wasipitishe maambukizi ya kingono kwa mtoto.

  • Wanawake wenye historia ya uchungu wa uzazi wa mapema ama kama una mimba ya mtoto zaidi ya mmoja.

Chanzo: AmericanPregnancy.org

Soma Pia:Wanandoa Wanapaswa Kufanya Ngono Mara Ngapi Kwa Wiki?

Written by

Risper Nyakio