Mwanamme Huyu Kutoka Cameroon Awa Mwafrika wa Kwanza Kupona Corona Virus Huko Uchina

Mwanamme Huyu Kutoka Cameroon Awa Mwafrika wa Kwanza Kupona Corona Virus Huko Uchina

He was the first African to contract the disease in china and the first African to recover!

Kem Senou Pavel Daryl, mwanafunzi kutoka nchi ya Cameroon anayeishi katika mtaa wa Jingzhou huko Uchina, ameweza kupona na kutangazwa huru kutokana na maambukizi ya kifo ya coronavirus, COVID – 19. Kulingana na BBC, alifanyika mwafrika wa kwanza kupona coronavirus huko Uchina baada ya kutibiwa katika hospitali huko eneo la kwao. Tuna angazia habari hizi za mwafrika aliyepone kutokana na ugonjwa huu hatari, kwa kimombo, african coronavirus survivor.

Kem Senou Pavel Daryl: Mwafrika wa kwanza kupona maambukizi ya coronavirus huko Uchina

African coronavirus survivor in China

Image: BBC

Senou alibakia kwenye chumba cha pekee katika hospitali eneo la kwao alipotibiwa kwa kutumia antibaotiki na dawa za kutibu wagonjwa wa HIV kwa siku kumi na tatu ambapo baadaye alionyesha dalili za kupona.  Wakati picha ya CT haikuonyesha dalili zozote za ugonjwa, akawa mwafrika wa kwanza aliyejulikana kuambukizwa coronavirus na wa kwanza aliyepona.

Ingawaje, wakati wa ugonjwa, Senou hakuwa na nia ya kurudi nyumbani Cameroon. Hii ni kwa sababu hakutaka kuupeleka ugonjwa Afrika. Serikali ya Uchina iligharamia matibabu yake yote.

coronavirus

Image: CNN

Senou alisemekana kupata virusi hivi baada ya kutembea mtaa wa Wuhan ambako maambukizi yalianza tangu Disemba mwaka uliopita. Baada yake kupona, alisisitiza asirudi nyumbani hadi baada ya kumaliza masomo yake.

Je, Nigeria imeitika raia wake walioko uchina?

Pavel Daryl Kem Senou

Raia kutoka Nigeria hujumuisha asilimia kubwa ya waafrika huko uchina. Walakini, kufikia hapa inaonekana kuwa hii nchi haina mpango wa kuwaondoa raia wake huko.

“watu wanasema : msiturudishe nyumbani kwani Nigeria hawatuwezi.” Nahisi mgogoro lakini mwisho wa siku mimi pia ni binadamu,” akasema Angela raia wa Nigeria aliyekipa kituo cha utangazaji  cha BBC jina moja tu.

“Tungeshukuru sana kama wangegundua kuwa kuna raia wa Nigeria huku lakini inaonekana sisi sio wa kipaumbele. Hatukupata msaada wowote kutoka kwa serikali yetu,” akasema.

Raia wengi wa Nigeria walioko huko uchina wanaishi kama Angela, aliyelazimika kutoka chumbani mwake kwa mara ya kwanza kwa siku 22 baada ya chakula chake kuisha. Nchi zingine kutoka Afrika kama vile Ghana na Ivory Coast walisemekana kutuma msaada wa kifedha kwa raia wao Uchina. Walakini, wengi wao wangependelea kurudishwa nyumbani.

“Kukaa huku hakuna uhakikisho wa usalama wetu. Tuko tu katika nchi iliyo na huduma bora za afya,” akasema Salima.

Wakati huo huo, kulingana na Aljazeera, Misri ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kudhibitisha kisa cha coronavirus. Taarifa kutoka kwa wizara ya afya huko Misri ilidhibitisha kuwa aliyeugua alikuwa mgeni na alikuwa amewekwa chemba. Habari hizi za african coronavirus survivor zinaendelea kutamba ila ni muhimu kwa kila nchi kuhakikisha kuwa wanazingatia usalama kuwalinda wananchi wao.

Pia Soma: How You Can Protect Your Family From The Wuhan Virus

Vyanzo: BBC, Aljazeera

Written by

Risper Nyakio