Tiba Bora Ya Kinyumbani Ya Miguu Inayo Uma

Tiba Bora Ya Kinyumbani Ya Miguu Inayo Uma

Njia rahisi za kinyumbani za kuponya miguu inayo uma!

Kuumwa na miguu hasa kushikana kwa misuli baadhi ya wakati huwa ya kushangaza na ya haraka na kukupata usipo tarajia. Na bila kupoteza muda, mikono yako hupepea hadi kwa sehemu hiyo ili kupunguza uchungu huo. Misuli iliyoko kwenye sehemu hiyo hushikana na huwa ngumu kugusa na unahisi kana kwamba utapiga nduru kwa nguvu. Je, unatambua hali hii? Huo ni uchungu wa misuli. Mara nyingi, sio ishara ya tatizo lolote la kiafya, kuna tiba ya kinyumbani ya miguu kuuma ama kuumwa na misuli.

Unapo pata shambulio la kuumwa na misuli, huenda ikakaa kwa hadi lisaa limoja ama zaidi. Inaweza athiri mguu ama mkono wote hadi uchungu huo upungue. Na baadhi ya wakati huenda ika athiri misuli inayo fanya kazi pamoja na tandem ama misuli inayo enda athiri mwendo wa baadhi ya viungo vya mwili kwa upande tofauti.

 

Nini kinacho sababisha maumivu ya miguu ama misuli?

causes of leg cramp

Maumivu ya misuli husababishwa na vitu vichache. Mzunguko duni wa damu kwenye sehemu fulani huenda uka sababisha maumivu haya. Baadhi ya wakati, huenda ikasababishwa na athari za baadaye za maumivu ya neva ama misuli. Matibabu, kukosa maji mwilini ama viwango vidogo vya kalisi, magnesium ama potassium huenda ikasababisha maumivu haya. Ukosaji wa vitamini kama vile thiamine, pantothenic acid na pyridoxine pia husababisha maumivu ya misuli.

Tiba za kinyumbani za miguu kuuma.

Hapa kuna baadhi ya tiba za kinyumbani ambazo unaweza jaribu peke yako ukiwa nyumbani.

 

  • Kunyoosha miguu

tiba ya miguu kuuma

 

Wacha kufanya kitendo kilicho sababisha uchungu ule iwapo kunacho. Jaribu kutuliza misuli inayo uma. Huku ukipiga mesi misuli ile, kwa utaratibu, nyoosha misuli hiyo kwa upole. Iwapo maumivu ya misuli inafanyika katikati ya usiku, simama na unyooshe mguu ulio athiri. Iwapo ni kwenye upande wa nyuma wa mguu, wekelea aina ya uzito.

  • Magnesium

Huenda ukawa hauna magnesium tosha iwapo unashuhudia maumivu ya miguu mara kwa mara isiyo husika na matatizo ya kiafya. Pia, unaweza jaribu kuongeza magnesium kwenye lishe yako. Mbegu na njugu ni vyanzo vizuri vya magnesium mwilini.

Magnesium ina julikana kama tiba ya miguu kuuma kwenye wanawake walio na mimba, ila utahitaji kuongea na daktari wako kabla ya kuchukua bidhaa zozote zinazo ongeza magnesium mwilini.

 

  • Ongeza joto

Jaribu matibabu ya kawaida ya kutumbukiza taulo kwenye maji moto kisha uiwekelee kwa sehemu inayo uma. Kufanya hivi kumewasaidia wengi waliokuwa wana shuhudia miguu kuuma. Pia, unaweza jaribu kupasha joto pedi iliyo kauka, ila anza kwa kiwango kidogo zaidi kisha uzidishe kutoka hapo. Ila iwapo una maumivu ya uti wa mgongo ama matatizo mengine ya kiafya yanayo kuthibiti kuto hisi joto, kupasha pedi joto haitafuzu kwako.

Additionally, many experts recommend using magnesium on your body exterior as Epsom salt.

 

  • Tembea

Unapo shuhudia maumivu ya miguu, jaribu kutembea. Jambo hili lina saidia misuli yako kutulia. Iwapo haifanyi kazi na unaendelea kuumwa na miguu, piga mesi sehemu hiyo ili kukusaidia kutuliza misuli yako.

 

  • Kunywa maji tosha

Suluhu nyingine ya miguu kuuma ni kunywa maji. Huenda ikakosa kutuliza uchungu kwa kasi, ila maji ama kinywaji cha michezo kilicho na electrolytes kinaweza saidia kukuponya kutokana na kuumwa na misuli siku za usoni.

Je, kuna matibabu ya miguu inayo uma?

Walakini, watu wengi wamegundua kuwa kunywa maji yaliyo na quinine ama tonic kabla ya kulala. Mbali na kuwa tiba ya miguu kuuma, inatuliza misuli na inaweza saidia katika kupunguza uchungu pia. Sindano ya tiba imetumika kutatua tatizo la misuli ila ni kwa kikundi hasa cha misuli.

Kwa hivyo, iwapo maumivu ya miguu yatazidi, kupimwa damu na vipimo huenda vikafanyiwa na neurologist. Mtembelee tena daktari wako ukishuhudia maumivu sawa. Na ufuatilie na daktari wako ikiwa unahitajika ili kugundua maradhi ambayo yanahitajika kutibiwa ili kukomesha kuumwa na misuli.

Ni kipimo kipi kinatumika na wataalum wa afya kubainisha maumivu ya miguu?

Daktari wako atajaribu kuangalia na kupima kila kitu. Kutoka kwa historia ya aina, sehemu, wingi na mara unazo shuhudia maumivu yale. Ikifuatiwa na kuangalia matibabu ili kujua kwa kina kinacho sababisha ishara. Dawa zako zita angaliwa kudhibitisha iwapo huenda zikawa ndizo zina sababisha ishara zile.

Kipimo cha damu kitahusisha upimaji wa viwango vya kalisi, potassium, hali ya neva na thyroid. Wakati ambapo kipimo cha fizikia huenda kikahusisha kuangalia nguvu za misuli na ufanyaji kazi wa neva.

Hitimisho

Iwapo maumivu ya misuli inaendelea kukutatiza, ni vyema kumtembelea daktari wako, ama mtaalum wa afya aliye angazia visa vya uchungu kama vyako. Wakati ambapo madaktari wengi hutibu maumivu, wataalum kama rheumatologists, physiatrists, na neurologists huenda wakafanya vyema zaidi.

Soma pia: Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kusaidia Kuponya Mauimivu Ya Tumbo

 

Written by

Risper Nyakio