Jinsi Muziki Unavyo Saidia Watoto Ambao Hawajakomaa Kukua Kwa Kasi

Jinsi Muziki Unavyo Saidia Watoto Ambao Hawajakomaa Kukua Kwa Kasi

Tiba hii ya muziki hufanyika karibu na hatua yao ya ukuaji ambayo wangekuwa katika ikiwa hawakuzaliwa mapema.

Tuna habari njema kwa wamama walio na watoto kwenye kitengo cha utunzaji wa watoto ambao hawajakomaa. Tiba ya muziki inaweza wasaidia kukua kwa mbio zaidi na kuja nyumbani kwa muda mfupi zaidi. Kulingana na utafiti, uliofanywa na mkurugenzi wa programu ya tiba ya muziki katika Chuo Kikuu cha Florida, Jayne Standley na timu ya watafiti wengine, waligundua kuwa kucheza muziki katika NICU kunaweza sababisha mtoto kukua kwa kasi zaidi. Na pia kupatiwa ruhusa ya kwenda nyumbani mapema kuliko walivyo tarajia.

Kwanini Unapaswa Kupatia Tiba Ya Muziki Kwa Watoto Katika Kitengo Cha Utunzaji Wa Watoto Ambao Hawaja Komaa Nafasi

orodha ya nyimbo za ibada za kuwafunza watoto

Katika Afrika na sehemu nyingi za dunia, wazazi wamekuwa waki ajiri usaidizi wa kuimbiwa nyimbo za kulala ili kuwafanya watoto walale na kuwafariji wanapo kuwa wakikwazwa. Vivyo hivyo, utafiti huu una mwelekeo sawa na kudhihirisha kuwa wazazi walikuwa kwa njia sawa.

Jayne Standley mojawapo wa watu walio anzia mbinu hii wamekuwa wakijaribu matibabu haya kwa karibu miaka 20 sasa. Kutoka wakati alipo fahamu kuwa watoto walio zaliwa kama hawajakomaa wana nafasi zaidi za kuhitaji masomo spesheli wanapo zidi kuzeeka.

Pia, masomo haya haya dhihirishi kuwa wana toka hospitali mapema tu, mbali kusaidia katika kuboresha ukuaji wao wa lugha.

Mbinu hii inapo tumika kwa watoto walio katika NICU, mbinu hii inatumia njia mbalimbali za kuchechemua ili kumsaidia mtoto kufahamu jinsi ya kuitikia wanapo kuwa katika kipindi kinacho wakazwa. Hasa kwani watoto wanao kuwa kwa kitengo hiki hupitia hatua tofauti za kukua na hatua hii huwa nyeti sana.

Jinsi Tiba Ya Muziki Katika NICU Inavyo Fanywa

tiba ya muziki

Tiba hii ya muziki hufanyika karibu na hatua yao ya ukuaji ambayo wangekuwa katika ikiwa hawakuzaliwa mapema. Ni kuimba kusiko na maneno kulingana na hatua ambayo mtoto ako na kukua hadi kuwa kuimba kwenye maneno na sauti kwa wakati unaofaa. Baadhi ya wataalum wa tiba ya muziki huenda wakawa watu walio funzwa jinsi muziki unasaidia watoto katika hatua hii. Wanafamilia pia wanafunzwa mambo ya kufanya ili kuwawezesha kuingiliana na watoto inapofika hatua ambapo wanaweza enda nyumbani.

Hizi ni habari njema kwa wazazi walio na watoto katika NICU, mbali na watoto wao kwenda nyumbani mapema kuliko walivyo tarajia na kuwa na nafasi nzuri ya kukua kwa kasi; kunapunguza fikira nyingi kwa wazazi kwa sababu hauhisi kana kwamba unamchungulia tu akiwa katika hatua hii nyeti. Huenda ikahusisha fedha zaidi na inahitaji wataalum wa tiba ya aina hii kuwa hospitalini na kufunzwa jinsi ya kufanya mtindo huu inavyo hitajka. Tuna tazamia kuona mbinu hii ikitumika zaidi katika hospitali zaidi za ki Afrika.

Chanzo: Wusfnews

Soma Pia:Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Usafi Wa Sehemu Za Siri Kwa Watoto

 

Written by

Risper Nyakio