Tiba ya Oral Rehydration Ni Nini Na Utaihitaji Wakati Upi?

Tiba ya Oral Rehydration Ni Nini Na Utaihitaji Wakati Upi?

Find out how oral rehydration therapy can treat dehydration caused by viral gastroenteritis and how to prepare the solution at home.

Tiba ya Oral Rehydration ni matibabu ya ukosefu wa maji mwilini. Inahusu kukunywa mkusanyiko maalum wa maji na glukosi na chumvi. Wazo ni kurudisha maji na sukari mwilini ili kuwa katika kiwango kifaacho.

Kwanini tunahitaji tiba ya oral rehydration?

tiba ya oral rehydration

Kwa tukio nyingi, ugonjwa huu hauko kiwango cha juu kwa hivyo hauhitaji daktari. Unaeza utibu kwa kumpa maji, maziwa ya mama, fomula ya watoto au sharubati iliyo na maji mingi.

Oral rehydration ni tiba ya hali iliyo ya kiwango cha juu .Ukosefu wa maji unasababishwa na virusi ya gastroenteritis ambayo pia inaitwa mafua ya tumbo. Virusi hivi vinaweza kumfanya mtoto wako ataike ama aendesha. Mambo haya huleta ukosefu wa maji mwilini.

Hivi juzi, Lagos ilipatwa na janga la virasi hii ya Gastroenteritis. Lilikuwa ni jambo la kushtua sana ambalo lilisababisha kifo cha watoto kadhaa hadi serikali ika ingilia kati.

Umuhimu wa ORS

matibabu ya oral rehydration

Iwapo mtoto wako anakosa maji mwilini kwa kiwango cha juu, anapaswa kuekwa maji mengine mwilini kutumia kifaa kinachoitwa laini ya  Intravenous (IV).Lakini  tiba ya oral rehydration inasaidia kama vile tu tiba ya maji ya intravenous ili kutibu ugonjwa huu wa kukosa maji mwilini.

Sababu:

 • ORT haina kiwewe kwa mtoto kwani hawahitaji kudungwa sindano.
 • ORT ni rahisi kupatia mtoto kwani unaeza mpatia hadi kwa nyumba.

Nini inayokuwa imeekwa ndaani ya mchanganyiko wa oral rehydration

Mchanganyiko wa oral rehydration imetengenezwa kimaalum inayokuwa na mchanyiko wa vitu mbali mbali:

 • maji
 • Sukari
 • Sodiamu, Potasiamu

Pamoja, vipengele hivi vinatumika kwa mujibu wa maji na virutubisho ambazo mwili inahitaji ili kufanya kazi vizuri.

Mchanganyiko huu huchukua muda wa dakika tano ili kuanza kupitia mchakato wa kusiaga chukula  kuelekea kwenye damu.

Utapata oral rehydration wapi?

tiba ya oral rehydration

Mchanganyiko huu unauzwa katika duka nyingi za dawa ikiwa:

 • Iliyochanganywa ndani ya chupa
 • Katiki hali ya poda ili ichanganywe na maji baadaye

Mifano ya kampuni za ORS ni kamaPedialyte, Infalte na Resol.

Dawa hii inayo uzwa kwa kama imechanganywa  ina idadi sawa yay a ugiligili ,chumvi na glukosi.Poda ya ORS sio ghali kibei na inakaa sana kabla ya kuharibika. Ingawa poda isipo changanywa kwa kiwango ambacho kinafaa cha maji ina haribu utenda kazi wake.

Ukinunua ilichanganywa tayari ama poda hakikisha kwamba umefuata mawaidha ifaavyo ili kuinua utendakazi wa dawa ile.

Jinsi ya kupatia mtoto mchanganyiko huu wa ORS

Patia mtoto kipimo kidogo mara nyingi, tumia kijiko ili kuhakikisha kwamba kipimo cha kwanza ni kidogo. Vipimo hivi vidogo vitahakikisha kuwa kwa ORS imebaki mwilini na kuzuia kutapika.

Unapoendelea kumpa mchanganyiko huu hakikisha kwamba unaongeza kipimo cha dawa unayompa kila wakati hadi mtoto aweze kumaliza kipimo chote kama ilivyopendekezwa na daktari.

Mtoto aliyechini ya umri wa miaka miwili anahitaji robo au nusu kikombe cha mchanganyiko kila anapoenda choo kimejaa maji.

Mtoto aliye na miaka miwili au zaidi anahitaji nusu au kikombe kimoja cha machanganyiko huu baada ya kwenda msalani umejaa maji.

Katika hali ambayo mtoto wako anakataa kukunywa mchanyiko huu, hospitali itatumia mpira unaoptia mapuani ili aweze kuikunywa.

Njia zingine isipokuwa ORS

Kuna matibabu ya kimila ambazo zitasaidia na hutengeneza mchanganyiko huu.Kuna dawa za kukunywa ambazo husaidia katika kuzuia mtoto wako kupoteza maji mingi wakati ambapo anaendesha:

 • Maziwa ya mama
 • Porojo iliyo na maji mengi
 • supu ya karoti
 • maji ya mchele

Unaeza pia jitengenezea mchanyiko wa chumvi na sukari ili kutinu mtoto wako nyumbani. Unachohitaji ni chumvi na sukari iliyochanganywa kwa viwango vifuatavyo:

Vijiko sita vya sukari

Kijiko cha chai nusu cha chumvi

Lita moja ya maji safi ya kunywa pia unaweza kuyachemsha kisha kupoesha.

Unaeza ongeza nusu kikombe cha naji ya nachungwa au ndizi zilizobondwa.

Unaweza tumia sukari aina tifauti tofauti kama sukari nyeupe au Molasses lakini sukari zingine zina vipimo vingi vya potasiamu kushinda sukari nyeupe.Pia unaeza tumia

 • Sharubati
 • Chai
 • Maji ya nazi

Kama hauna kitu kingine cha kutumia unaeza tumia:

 • Maji safi kisha uyachemshe tena uyapoeshe.

Kids Health

Also read: Everything You Should Know About Viral Gastroenteritis In Children

Written by

Risper Nyakio