Maumivu ya kichwa hushuhudiwa kwa kawaida. Maumivu haya husababishwa na mambo tofauti. Wataalum hushauri kuenda hospitalini kupata tiba badala ya kununua dawa kwenye duka la madawa bila kuelewa chanzo. Hata hivyo, kuna wakati ambapo maumivu haya huwa makali na kukuhitaji kutafuta njia ya kuyapunguza kabla ya kwenda hospitalini. Tazama baadhi ya tiba za kinyumbani za maumivu ya kichwa.
Tiba za kinyumbani za maumivu ya kichwa

Dawa ya kinyumbani ya kupunguza uchungu kwa kasi. Mbali na kupunguza uchungu, hupunguza inflammation na kusaidia na uchakataji wa chakula tumboni.
Ongeza kipande cha tangawizi kwenye maji unayochemsha ama kwenye chai yako.

Husaidia kupunguza maumivu ya kichwa kwa kasi.
Jinsi ya kuitumia. Ongeza kiasi cha poda ya cinnamon kwenye bakuli safi, kisha ongeza kiwango kidogo cha maji. Changanya kisha upake kwenye paji la uso. Pumzika halafu uoshe kwa kutumia maji ya vuguvugu baada ya dakika 30-45.
Mazoezi mepesi ya kunyoosha mwili yanayohusisha sehemu ya kichwa na shingo yatasaidia kupunguza maumivu ya kichwa. Kila unapohisi maumivu ya kichwa, jaribu kuuonyoosha mwili.
Ili kupunguza maumivu ya kichwa, paka sugua kiasi cha thyme kwenye paji la uso. Ipe dakika chache kisha ufute ama kupanguza kwa kutumia kitambaa kisafi.

Kutokuwa na maji tosha mwilini kumehusishwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara. Hakikisha unakunywa maji unapohisi maumivu ya kichwa. Kula chakula kilicho na umaji maji, supu na matunda yenye viwango vya juu vya maji kama vile tikiti maji.
Kukunywa vileo huenda kukakosa kusababisha maumivu ya kichwa. Ila, unywaji wa vileo hupunguza viwango vya maji mwilini. Viwango vilivyopunguka vya maji mwilini vimehusishwa na maumivu ya kichwa. Punguza viwango vya vileo unavyokunywa kwa siku.

Kutolala vyema usiku husababisha maumivu ya kichwa. Unapohisi kuwa unaumwa na kichwa na hauna kazi ya kufanya, chukua dakika chache ulale. Ni muhimu sana kupata masaa 8 ya usiku kila siku.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Hongera! Sarah na Simon Kabu Wanatarajia Mtoto Wao Wa Tatu Pamoja