Mama Apeana Maziwa Kwa Heshima Ya Mtoto Wake Aliyeishi Masaa Matatu

Mama Apeana Maziwa Kwa Heshima Ya Mtoto Wake Aliyeishi Masaa Matatu

Sierra Strangfield alifanya jambo la hekima sana. Baada ya kupoteza kijana wake Samuel kwa sababu ya ugonjwa wa kimaumbile uitwao Trisomy 18 kwa watoto. Ugonjwa huu unasababisha kukua polepole. Samuel alizaliwa na wiki 25 mwezi wa September 5 katika hospitali iliyokuwa karibu na nyumba ya familia yake katika makao ya Neillville, Wisconsin.

Kifo chake kilihuzunisha mama yake. Lakini alikuwa ameamua kuwasaidia watoto wengine wagonjwa. Aliendelea kukamua maziwa ya kuwapatia hadi Novemba 7-siku ambayo alikuwa ametayarisha kukaribisha Samuel duniani. Sierra alihifadhi maziwa yake kila siku kisha baadae akawapatia watoto waliougua.

Sierra aandika kuhusu alicho kipitia

trisomy 18 kwa watoto

Kuandika katika mtandao wa Facebook, Sierra alieleza: ’Nilipogundua kuwa niko na mimba tena, nilitaka niwe mzuri kwa kunyonyesha mtoto. ’Lakini tulipogundua ugonjwa ambao Samuel alikuwa nao, nilijua kwamba singe nyonyesha tena.

‘Hili lilikuwa tumaini lingine ambalo nilikuwa nimenyang’anywa’. Kabla Samuel aage dunia nilijiambia kuwa ningehifadhi maziwa yangu ili nisaidie watu wengine.’Siera alisema kwamba msichana wake mzee Porter alipata maziwa ya kusaidiwa kwa miezi kadhaa baada ya kuzaliwa na jambo hili lilimpa motisha wa kufanya jambo kama hilo.

Aliongeza na kusema kwamba:’ Singeokoa maisha ya Samuel lakini labda ningeokoa maisha ya mtoto mwingine.

‘Kukamua maziwa si jambo la wanyonge.

trisomy 18 kwa watoto

Ni jambo ligumu sana kiakili na kimwili. Pia ni vigumu zaidi wakati hauna mtoto. ’Kuna wakati nilikuwa nimekasirika kwa sababu maziwa yake ilikuja wakati hana mtoto wa kunyonyesha? ’Kwa nini alikuwa anaamka usiku kwa sababu ya jambo hili.

‘Kwa upande mwingine niliskia kwamba jambo hili ndilo tu lilikuwa linanihusisha na Samuel duniani. Nilitumaini kuwa anaskia vizuri! ’Nilitoa maziwa siku 63 baada ya kuzaliwa kwake.Sikutoa kwa wingi lakini nilijaribu vyovyote ningweza ili kutoa itakayotosha.

‘Na leo, siku yake ya mwisho, nimepatiana maziwa yangu kwa NICU kwa mara ya kwanza na ya mwisho. ’Kutembea humo hospitalini lilikuwa njia moja ya kupona rohoni mwangu najua hivi sababu kindandani nilimhisi, Samuel alikuwa hapo nami'. Ujumbe huu Sierra aliouandika ulisambaa kote mitandaoni, na maelfu ya watu kumpa hongera kwa sababu ya kitendo hiki cha ukarimu. Alisema kwamba alishtuliwa na jinsi watu walivyo kichukulia kitendo hiki, na sasa anataka kuzidisha ufahamu wa ugonjwa huu wa Trisomy 18.

Unacho paswa kujua kuhusu Trisomy 18 kwa watoto

Mama Apeana Maziwa Kwa Heshima Ya Mtoto Wake Aliyeishi Masaa Matatu

Trisomy 18 kwa watoto ni shida ya kimaubile. Unajulikana pia kama’ Edwards Syndrome’ daktari aliyeugundua.

Chembeuzi  miundo yenye umbo kama uzi  kwenye seli  zinazobeba jeni. Jeni zinabeba maagizo yanayohitajika ilikusaidia kila sehemu ya mwili wa mtoto.

Wakati ambapo ovari na manii zinaposhikana na kutengeza kiinitete, chembeuzi zake zinashikana. Kila mtoto anapata chembeuzi 23 kutoka kwa ovari za mama yake na chembeuzi 23 kutoka kwa manii ya baba yake, kwa jumla kuwa 46.

Wakati mwingine ovari ya mama ua mani ya baba yake ina idadi isiyofaa ya chembeuzi. Wakati ambapo ovari na manii zinapoungana, kosa hili linapitishwa kwa mtoto.

‘Trisomy’ inamaanisha kuwa mtoto ana chembeuzi zaidi katika seli moja au zote. Katika tukio hili Trisomy 18, mtoto ana nakala tatu za chembeuzi 18. Hii inasababisha vuingo vya mtoto kukuua kwa njia isiyokuwa ya kawaida.

WebMD, MetroUK

Also read: Midwife suspended after delivering premature twins at home birth

 

Written by

Risper Nyakio