Kila mtu hupata matatizo ya tumbo mara kwa mara. Lakini kulingana na kiwango cha uchungu, huenda ukahitajika kutembelea kituo cha afya ili kufanyiwa vipimo kubaini chanzo cha tatizo lile. Je, tumbo kuuma ni dalili ya mimba? Maumivu ya tumbo husababishwa na mambo tofauti. Tuna angazia vyanzo vya maumivu ya tumbo.
Vyanzo vya kuumwa na tumbo
- Ugonjwa wa tumbo (gastritis)
Ili chakula kichakatwe tumboni, asidi nyingi inatumika. Baadhi ya wakati, huenda asidi hii ikapita kwenye tumbo na kuathiri kuta za tumbo, hali inayofahamika kama ugonjwa wa tumbo ama gastritis kwa kimombo. Hali hii pia husababishwa na bakteria, kusombwa kimawazo, watu walio na uraibu wa kunywa pombe sana wako katika hatari ya kupata ugonjwa huu. Hali hii isiporekebishwa mapema, huenda ikasababisha vidonda vya tumbo ama ulcers.
2. Vidonda vya tumbo vya peptic
Hivi ni vidonda wazi vilivyo kwenye ukuta wa tumbo. Husababishwa sana na bakteria ama utumiaji mwingi wa dawa za ibuprofen ama aspirin. Watu wanaotumia sigara na pombe sana huwa katika hatari ya kupata ugonjwa huu.
3. Virusi vya tumbo
Virusi kwenye matumboa. Mtu aliye na virusi hivi hushuhudia ishara kama kuendesha, kuumwa na tumbo, kichefuchefu na kutapika. Virusi hivi hupitishwa kupitia kwa ulaji wa chakula kilicho na virusi ama mtu aliye na virusi hivi. Sawa na virusi vingine, havina tiba, ila huisha bila matibabu.
4. Sumu kupitia chakula (Food poisoning)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi, bakteria na viini vilivyo kwenye chakula. Mtu aliye na ugonjwa huu huwa na ishara kama kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Hupungua baada ya muda. Lakini unapoanza kutapika damu, ni muhimu kwenda kwenye kituo cha afya kufanyiwa vipimo.
5. Mzio wa chakula
Hufanyika mwili unapochukulia chakula ulichokila kama kitu hatari na kujaribu kuulinda mwili wako. Ishara zake huwa kuumwa na tumbo, kufura mdomo ama koo na kuhisi kujikuna ngozi. Katika hali sugu, huenda ukasababisha kifo, ni vyema kuchukua dawa ya epinephrine punde tu chakula ulichochukua kinaanza kuwa na athari hasi kwa mwili wako. Baadhi ya vyakula vilivyo na mzio ni kama njugu, mayai, siagi, maziwa na vyakula vya baharini.
Tumbo kuuma ni dalili ya mimba? La hasha, kuumwa na tumbo sio ishara ya kuwa na mimba wakati wote. Unapoumwa na tumbo na kukosa hedhi, nafasi kubwa ni kuwa una mimba. Lakini unapoumwa na tumbo peke yake, sio ishara ya tumbo, ni vyema kufanyiwa vipimo kubaini chanzo chake.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Vyanzo Vya Maumivu Makali Kwa Matiti Katika Wanawake