Wakati wa ujauzito mwili wa mwanamke huwa na mabadiliko mengi kutokana na homoni. Kwa wakati mwingine haya mabadiliko huwa sumbufu lakini kwa nyakati nyingi huwa ya kawaida ya kumwezesha mama kulisha na kulinda fetasi. Haya mabadiliko wakati wa ujauzito hutokea kwenye uterasi, seviksi, uke, mfumo wa moyo, mfumo wa tumbo na mfumo wa mkojo, matiti na pia ngozi. Tumbo ya chini ina hisi vipi katika ujauzito?
Mabadiliko ya Tumbo Katika Ujauzito

Homoni kuu za uzazi za mwanamke estrojeni na projesteroni huiandaa uterasi kudhibiti ujauzito. Viwango vya hizi homoni huwa kuu sana kipindi chote cha ujauzito. Viwango vya juu vya projesteroni husababisha ukubwa wa baadhi ya viungo vya ndani ya mwili ikiwemo pamoja na uterasi ili iweze kubeba mtoto aliyehitimu muhula wote wa ujauzito. Ila kiwango hiki pia kina athari zingine kwenye mishipa ya damu na jointi.
Baada ya utungisho, uterasi hutoa mandhari yenye lishe na kinga ambapo fetasi itaweza kukua na kustawi. Uterasi huongezeka kwa ukubwa kutoka kwa saizi ya pea ndogo wakati mwanamke hana ujauzito hadi iweze kubeba mtoto aliyehitimu kipindi chote cha ujauzito. Tishu ambazo hutumika kuunda uterasi huendelea kukua kwa wiki 20 zinazofuatia utungisho na huendelea kuongezeka kwa uzani kutoka gramu 50-1000.
Baada ya wiki 20 kupita, uterasi huwa haiongezeki kwa uzani ila itajivuta ili kumpa mtoto anayekua nafasi , plasenta na viowevu vya amniotiki. Kufikia mwisho wa ujauzito uterasi itakuwa imeongezeka kwa ukubwa mara tano zaidi ya ukubwa wake wa kawaida. Kwa urefu kutoka juu hadi chini huongezeka kutoka sentimita 7.5 hadi 30.
Uterasi Kuongezeka Ukubwa

Katika mwisho wa wiki 12 ama mwisho wa trimesta ya kwanza, pembeni ya juu ya mwili wa uterasi inaweza kupapasika kupitia fumbatio juu ya mfupa wa kinena. Kwa kawaida kilele cha ukubwa wa uterasi hufukia baada ya wiki 36 baada ya ujauzito. Kwa kipindi chote cha ujauzito seviksi hubakia na urefu wa sentimita 2.5.
Katika kipindi cha mwisho ama trimesta ya mwisho seviksi hunyooka kufuatia mikazo isiyo chungu ya pembezo zake zinazoongezeka. Inapokaribia mwisho wa ujauzito uke pia huenedelea kunyumbulika. Haya mabadiliko huwezesha uke kutanuka katika awamu ya pili ya leba huku mtoto akishukia katika njia ya uzazi. Mtoto anavyoendelea kukua, mkao kwa kijumla wa mama huendelea kubadilika. Fumbatio lake hubadilika kutoka hali bapa hadi kubinuka sana (kutoka nje).
Hili husababisha kuongezeka kwa mpindiko wa mgongo wake. Uzito wa fetasi, kuongezeka kwa uterasi na plasenta pamoja na ongezeko la mpindiko wa mgongo yote husukuma mifupi na misuli ya mwanamke. Kufuatia hili wanawake wengi wenye mimba huumwa na mgongo.
Aina nyingi ya maumivu ya mgongo wakati wa ujauzito ni kawaida ila pia inaweza kuwa ishara ya maambukizi kwenye figo.
Hitimisho
Ongezeko la uzani kwa mama mjamzito hukisiwa kuwa ishara kuwa mwili wa mama umeanza kukubali mabadiliko na kukua kwa fetasi na kuathiri tumbo ya chini ina hisi vipi katika ujauzito. Hata hivyo, upimaji wa uzani wa mara kwa mara wa mama mjamzito kwa sasa unaonekana kutokuwa na umuhimu sana kwa sababu haulingani vyema ma malengo ya ujauzito. Ila ukosefu wa kuongeza uzani si jambo la wasiwasi kwa wanawake wengi ila inaweza kuashiria fetasi haikui vizuri.
Soma Pia: Je, Kuna Uwezekano Wa Kukomesha Mimba Baada Ya Siku Nane?