Aina Tofauti Ya Ndoa Zinazo Kubalika Nchini Kenya

Aina Tofauti Ya Ndoa Zinazo Kubalika Nchini Kenya

Hivi majuzi, mwimbaji mashuhuri kutoka nchi ya Nigeria Yemi Alade amekuja wazi na kusema jinsi barobaro moja kutoka familia ya ki-Maasai kutoka nchini Kenya alivyo taka kumpa ng’ombe ishirini ili wafunge pingu za maisha pamoja. Ila rafikiye barobaro huyu alimvunja moyo kwa kumwambia kuwa Yemi ana mwili mkubwa na atashindwa kujenga nyumba ya kinyesi cha ng’ombe. Je, unajua aina ya ndoa zinazo kubalika nchini/types of marriages in Kenya?

Je, ndoa ni nini hasa? Ndoa inatambulika kama muungano wa mke na mume na kuamua kufunga pingu za maisha pamoja na kuanza maisha ya umoja. Ili iwe rasmi, lazima ifuate sheria za nchi ya Kenya kama zilivyo andikwa kwenye katiba. Watu huoana kwa sababu tofauti. Huenda ikawa ili kuanzisha familia na kupata watoto, kuepuka mkazo wa kupata mchumba ama sababu ya mapenzi. Makala haya yana angazia types of marriages in Kenya!

Aina ya ndoa nchini Kenya/ Types of marriages in Kenya

Ndoa za kanisa/ kikristiano

Hii ni aina ya ndoa ambayo mchumba mmoja ama wote wawili ni wa kristiano. Ndoa hii ina hutubishwa na mhubiri wa kanisa lao. Wa kristiano wana tazama ndoa hii kama agano  na uhusiano huu unategemea masharti na kuahidiana. Ukijiingiza katika ndoa hii, hauna nafasi ya kupata mchumba wa pili kwani ina kuza uhusiano kati ya bibi mmoja na bwana mmoja. Cheti cha ndoa huidhinishwa baada ya siku 14 katika ofisi ya serikali ya kujisajilisha. Ili ipitishwe, haipaswi kupingwa na mtu yeyote. Visa vinavyo pelekea kuto idhinishwa na kukubalika kwa ndoa kati ya watu wawili ni sababu kama vile:

 • Harusi kuhutubishwa na mtu ambaye hajapewa mamlaka ya kuhutubisha ndoa nchini.
 • Ndoa yenu kupingwa kabla ya siku 14 kuisha tangu ndoa yenu kutendeka.
 • Iwapo kuna mtu ana kuja na sababu mbona wawili wenu hampaswi kufunga ndoa na mhubiri kukubalia sababu hiyo.
 • Iwapo mmoja wenu anahusika katika kesi ya talaka ambayo haija kamilika.

types of marriages in kenya

Ndoa za Kihindu

Aina hii ya harusi hutendeka pale ambapo mchumba mmoja ama wote wawili wana imani ya kihindu. Ina hutubishwa na mtu aliye sajilishwa kufanya hivi kulingana na imani za kihindu. Mahari inalipwa kwa familia ya bibi. Ili ndoa hii kuwa rasmi, mtu anaye waunganisha wawili hawa kupeleka barua yao kwenye ofisi ya kujisajilisha ya nchi. Uhusiano huu utakosa kuwa rasmi iwapo mambo yafuatayo yatafanyika:

 • Iwapo mmoja wa wachumba hawa wameolewa kwa watu wengine.
 • Mmoja wa wachumba hawa haja fikisha umri unaotakikana.
 • Mchumba mmoja hana akili timamu.
 • Iwapo mmoja wa wachumba hawa anaamua kumpa mwingine talaka.
 • Mmoja wa hawa ameenda nje ya ndoa.
 • Iwapo mmoja wao anahusika na tabia duni za ukatili.

Aina Tofauti Ya Ndoa Zinazo Kubalika Nchini Kenya

Ndoa za Kiislamia

Ndoa hizi zinajulikana kama nikah. Ili kufanya ndoa aina hii, lazima wawili  hawa wawe wa imani ya kiislamia. Imam aliye pewa mamlaka ya kuhutubisha ndoa hii anawaunganisha wawili hawa. Na baadaye kupewa urasmi na ofisi ya usajili nchini. Katika ndoa hii, inakubali kuwa na bibi zaidi ya mmoja. Ina sherehekewa kulingana na sheria za imani ya kiislamu. Ndoa hii inakosa kufanyika iwapo:

 • Wawili hawa ni ma binamu.
 • Iwapo bwana anataka kumrithi bibi bila ya makubaliano.
 • Mchumba mmoja anataka talaka.
 • Iwapo mwanamme anataka kufunga pingu za maisha na mama yake ama mwanamke aliyekuwa ameolewa na babake.
 • Iwapo korti ya Kadhi ina sababu za kukataa uhusiano kati ya wawili hawa.

Aina Tofauti Ya Ndoa Zinazo Kubalika Nchini Kenya

Ndoa ya Kisheria

Aina hii ya ndoa ina wapa wana ndoa kujulikana kwa kutumia cheti za ndoa nchini Kenya.  Wanao taka kufunga ndoa wanapaswa kuandika barua rasmi kwa ofisi ya usajili wa eneo lao siku zisizo pungua 21 na zisizo zidi 90. Baada ya kuchapishwa na kukosa kupingwa, sherehe inafanyika. Ndoa hii inakosa kufanyika iwapo:

 • Barua rasmia haiku andikwa kwa ofisi ya usajili.
 • Mmoja wa wachumba hawa ako katika uhusiano usio kubalika.
 • Iwapo mmoja wao ameolewa.
 • Mchumba mmoja na kifungo cha jela cha zaidi ya miezi saba.
 • Wana achana kwa zaidi ya miaka mitatu.

Ndoa za kiasili ama kitamaduni

Ndoa ya aina hii inafanyika kufuatia kanuni na desturi za kila jamii. Wazazi wa mchumba wa kike wanaipa familia ya mchumba wa kiume vitu ambavyo wangependa zitimizwe kabla ya kuwapa msichana wao kwa kijana huyu. Kulingana na kitamaduni, katika ndoa hii, mwanamme alikubalishwa kuwa na zaidi ya bibi mmoja. Baada ya kuifanya harusi hii, unapaswa kujulisha ofisi ya usajili nchini.

Uhusiano huu unakosa kukubalika iwapo:

 • Msajili anagundua kupingwa kwa uhusiano wenu
 • Wazee wa kijiji wanapinga uhusiano wenu
 • Mmoja wa wachumba hawa analazimishwa kufanya harusi hii
Ndoa ya kukaa pamoja

Hii ni ndoa ambapo mwanamke na mwanamme wanakubaliana kuishi pamoja. Katika mpangilio huu, hakuna cheti cha ndoa rasmi. Ila, mpangilio huu ni maarufu zaidi nchini Kenya. Kwa mara nyingi, mvulana huwatembelea wazazi wa msichana na kuwaomba wamruhusu kuishi na binti yao. Katika mipangilio ingine, wawili hawa huishi pamoja bila kuwajuza wazazi wao. Hadi pale wanapo pata watoto na kuenda kuwajulisha wazazi wao kuwa walipata wachumba na kuomba baraka za wavyele wao katika safari yao ya uzazi. Iwapo mpangilio huu sio rasmi, bado unajulikana na katiba ya nchi ya Kenya kwani watu wengi wana ufuata mfumo huu. Mnapo pata watoto na kuishi kwa pamoja, katiba ina watambua kama bibi na bwana rasmi.

Vyanzo: hivisasa

Written by

Risper Nyakio