Ni kawaida kwa wanawake wote kutoa uchafu kutoka kwa uke wao. Uchafu huu unaweza kumsaidia mwanamke kufahamu afya yake ilivyo. Kwa kuangalia uchafu wa uke wake, mwanamke anaweza kung'amua ikiwa ana afya nzuri, ni mgonjwa, ana tarajia kipindi chake cha hedhi, iwapo ana maji tosha mwilini ama ni mjamzito. Zote kati ya hizi hutofautiana. Uchafu wa uke katika ujauzito hukaa vipi?
Uchafu wa uke katika ujauzito

Mabadiliko katika kiwango cha uchafu wa uke baadhi ya wakati ni ishara ya kuwa na mimba.
Uchafu wa uke ni kawaida kwa wanawake, na hutoka kwenye sehemu ya uke wao. Kulingana na kiwango, rangi na harufu ya uchafu huu, mwanamke anaweza fahamu hali ya afya yake na iwapo ana mimba ama matatizo mengine.
Homoni mwilini mwa mwanamke zina athiri kamasi inayo tolewa kutoka kwenye uke wa mwanamke. Viwango vya homoni mwilini hubadilika mwanamke anapo anza kipindi chake cha hedhi na anapo kuwa na mimba. Na kuathiri jinsi kamasi kutoka kwa kizazi cha mwanamke inavyo kaa na kiwango chake.
Kutofautisha uchafu wa uke wenye afya na usio na afya
Usio na afya
- Rangi ya manjano ama kijani
- Kujikuna kwenye uke
- Uchungu mwanamke anapo enda haja ndogo
- Harufu mbaya kali
- Uchafu kushikana kama vile unga
Wenye afya
- Hauna harufu
- Rangi nyepesi
- Mwepesi unapo gusa
- Sio mwingi sana kiwango cha kukukosesha amani
Uchafu wa uke katika ujauzito

Katika siku za mwanzo za ujauzito, mwanamke ana shuhudia ongezeko la uchafu kutoka kwa uke wake. Ongezeko la homoni ya estrogen mwanamke anapokuwa na mimba husababisha mwili kutoa uchafu zaidi unaotolewa kupitia sehemu ya uke.
Uchafu huu unaotolewa mwilini mwa mwanamke unasaidia kulinda fetusi dhidi ya maambukizi kufika kwenye uterasi kupitia kwa uke. Kadri ujauzito unavyo zidi, ndivyo kiwango cha uchafu huu kitakavyo zidi kuongezeka hadi pale ambapo mwanamke atajifungua.
Mambo yanayo athiri uke unao tolewa mwilini
Mbali na kuwa na mimba, kuna vitu vingine vinavyo badilisha rangi, kiwango na harufu ya uchafu unao tolewa kwenye uke wa mwanamke.
- Maambukizi ya bakteria yanayo fanya uchafu huu uwe na harufu ya samaki
- Maambukizi ya trichomoniasis yanayo ufanya kuwa na rangi ya kijani ama manjano
Makala haya ya uchafu wa uke katika ujauzito hukaa vipi yana malengo ya kuwaelimisha wanawake kufahamu wakati panapokuwa na tatizo katika hali ya afya yao. Je, una maswali kuhusu makala haya? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mdogo.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Sababu 3 Kuu Zinazo Sababisha Maumivu Ya Matiti Kwa Wanawake