Mtoto Wangu Wa Mwaka Mmoja Ana Uchafu Wa Uke!

Mtoto Wangu Wa Mwaka Mmoja Ana Uchafu Wa Uke!

Nimegundua kuwa kila ninapo mbadilisha mtoto wangu wa chini ya mwaka mmoja nepi ana uchafu kwenye uke wake. Sijui cha kufanya wala cha kufikiria kwani mtoto wangu angali mchanga wa kuanza kuwa na uchafu wa uke. Tatizo ni lipi? Huenda akawa mgonjwa?

uchafu wa uke

Uchafu wa kike ni nini hasa?

Uchafu wa kike wa rangi nyeupe ni kawaida kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka minane ama michache. Na hakuna jambo la kukutia shaka unapo ona kuwa mtoto wako wa kike mwenye miaka kama minane na kushuka anatoa uchafu kwenye uke wake. Jambo hili ni la kawaida. Ila, unapogundua kuwa rangi ya uchafu kutoka kwa uke wa mtoto wako umebadili rangi na kuwa wa rangi ya hudhurungi ama kinjano. Ama pia ikiwa uchafu huu una harufu mbaya kana kwamba ya samaki. Hizi huenda zikawa ni ishara kuwa mtoto wako anaugua maradhi. Huenda ukagundua kuwa mtoto wako wa mwaka mmoja ama miezi kadhaa anajikuna, kuhusi kusumbuka, uvimbe ama kujikuna kwenye sehemu yake ya uke. Uchafu wa uke wa rangi ya kinjano kwa mara nyingi huandamana na hali ya kuhisi kujikuna.

Katika umri huu mchanga, mtoto wako ana mfumo wa kinga ambao bado hauja kua na hauna nguvu tosha kupigana na magonjwa na maradhi. Kwa hivyo huenda mtoto wako akaugua maradhi mengi ikilinganishwa na watu wazima kwani mifumo yao ya kinga huwa ime imarika.

Sababu kuu ya mtoto wako kuwa na uchafu wa uke katika umri huu mara nyingi huwa kwa sababu ya maambukizi ya chachu. Epuka kumpatia mtoto wako dawa bila kupata ushauri wa daktari. Hakikisha kuwa unampeleka mtoto wako kuona daktari ilia pate vipimo mwafaka kudhibitisha chanzo na maradhi ambayo ako nayo mwilini na apate matibabu yanayofaa.

Mtoto Wangu Wa Mwaka Mmoja Ana Uchafu Wa Uke!

Je ni njia zipi bora kusimamisha hali hii kwenye mtoto?

Zingatia Usafi

Kwa mara nyingi, mtoto mdogo kupata uchafu wa uke huwa ni kufuatia vipande vidogo vya kinya kuingia kwenye uke wako na hivi kusababisha maradhi kwenye mtoto wako. Hakikisha unampanguza mtoto wako ifaavyo kutoka nyuma hadi mbele na wala sio kutoka mbele hadi nyuma. Mtoto anapokuwa mdogo, hakikisha kuwa uko makini zaidi naye hasa katika kumbadilisha nepi ama diaper. Unapaswa kufanya hivi baada ya masaa machache na wala si baada ya muda mrefu. Unapo mwacha mtoto na nepi moja aliyo ichafua kwa muda mrefu, unamweka kwa hatari ya kupata maradhi ama kuchomeka kwenye sehemu yake ya uke.

Epuka kutumia sabuni inayo nukia

Kwa mara nyingi, watoto wengi huwa na mzio wa sabuni za kunukia sana. Huenda zikasababisha kujikuna kwenye sehemu ya uke wao. Ni muhimu kwa kila mzazi kuzingatia kutumia sabuni zilizo sawa kwa umri wake. Baada ya kumaliza, mpanguze kwa utaratibu kwa kutumia kitambaa kisafi. Kisha hakikisha kuwa wakati wote unamvalisha mtoto wako nguo ambazo hazijamkaza sana ilia pate nafasi ya kupumua.

uchafu wa uke

Kutibu uchafu wa uke

Unapogundua kuwa mwanao ana toa uchafu, hakikisha umempeleka kwenye kituo cha matibabu ili daktari akushauri dawa bora zaidi za kumpatia mtoto wako. Mbali na haya, ni vyema kuhakikisha kuwa unampatia mtoto wako vinywaji vingi hasa maji safi na pia maziwa ya bururu yasiyo kuwa na sukari nyingi. Lishe bora ni muhimu kwa mtoto wako, hakikisha unaongeza nafaka nzima, kitunguu saumu na mboga kwenye chakula chake na upunguze idadi ya sukari unayomlisha. Hakikisha kuwa wakati wote huichukulia afya ya mtoto wako mikononi mwako na kuwa wakati wote unampeleka hospitalini kuona mtaalum wa afya ya watoto.

Vyanzo: Verywellfamily, webmd

Written by

Risper Nyakio