Ishara Za Uchungu Wa Uzazi: Jinsi Ya Kujua Kuwa Mtoto Ako Njiani

Ishara Za Uchungu Wa Uzazi: Jinsi Ya Kujua Kuwa Mtoto Ako Njiani

Siku yako ya kujifungua inapo wadia, aina yoyote ya maumivu ya mwili na kuto starehe kunaweza kufanya ushangae kama siku yako kuu imewadia. Je, niko katika uchungu wa uzazi? Kichefu chefu ni ishara kuwa uchungu wa uzazi una wadia? Mchakato wa kutoa mtoto wako mwilini na kumweka mikononi mwako ni kazi nyingi. Haijalishi kama uchungu huu ni mfupi na wenye kasi, mwili wako huanza kujitayarisha wiki kabla ya siku kuu kufika. Kufahamu uchungu wa uzazi ni nini na ishara za kuwa makini kuona kutakusaidia kukupatia vitu unavyo paswa kuwa mwangalifu kuhusu. Hapa chini kuna baadhi ya ishara za uchungu wa kujifungua ambazo unaweza kushuhudia kujifungua kwa mtoto wako kunapo karibia. Lakini kwanza, uchungu wa uzazi ni nini?

Uchungu kabla ya kujifungua ni mchakato wa kujifungua mtoto. Huanza na kubanwa kwenye uterasi na kuisha na kujifungua kwa mtoto wako.

Ishara za uchungu wa uzaziuchungu wa uzazi

  • Mtoto ana shuka

Ikiwa wewe ni mama wa mara ya kwanza, mtoto wako ataanza kushuka kwenye pelvisi yako wiki chache kabla ya uchungu wa uzazi. Na huenda kushuka huku kukafanyika katika uchungu wako wa uzazi. Tarajia watu kukwambia kuwa mtoto wako ameshuka wanapo kuona wiki chache kabla ya kujifungua.

Tarajia kuenda msalani mara kwa mara kwa sababu katika hatua hii, mtoto wako anasukuma chini kibofu chako cha mkojo. Habari njema ni kuwa unaweza pumua kwa urahisi sasa kwa sababu mtoto wako ako mbali na mafua yako.

  • Una harisha

Unapo karibia kujifungua, misuli mwilini huanza kulegea ikijitayarisha kwa mchakato wa kujifungua. Misuli yako ya rectum pia ina legea, na huenda ukaanza kuharisha. Hata kama ni jambo linalo kera, ni kawaida sana; hakikisha kuwa unakunywa maji tosha na ukumbuke kuwa ni ishara nzuri!

  • Mlango wa uke kupanuka

uchungu wa uzazi

Mlango wako wa uke pia utaanza kujitayarisha kwa mchakato wa kujifungua. Huanza kufunguka na kuwa konde siku ama wiki chache kable ya kujifungua. Katika wiki zako za mwisho kabla ya kujifungua, daktari wako ataanza kupima kiwango ambacho umefunguka unapo enda hospitalini.

  • Kuumwa na mgongo na tumbo

Hasa kama hii sio mara yako ya kwanza kuwa na mimba, huenda ukahisi uchungu mwingi tumboni na kwenye mgongo. Kwa sababu misuli yako ina nyooka na kusonga kujitayarisha kwa mchakato wa kujifungua.

  • Kuhisi uchovu mwingi

Unapo karibia kujifungua, huenda ukahisi kana kwamba umekuwa ukifanya kazi siku nzima. Tumbo kubwa inaweza fanya iwe vigumu kwako kupata usingizi usiku katika wiki chache za mwisho za ujauzito.

Chanzo: Healthline

Soma Pia: Vidokezo Bora Vya Jinsi Ya Kujifungua Kwa Urahisi

Written by

Risper Nyakio