Uchungu wa uzazi katika mimba ni mchakato ambapo mtoto mchanga pamoja na placenta zinatolewa kutoka kwenye uterasi na mwili wa mwanamke.
Uchungu wa uzazi una hatua tatu kutoka kuanza hadi kukamilika kwake. Ishara maarufu za kuanza kwa mchakato huu ni kuhisi uchungu kwenye tumbo. Uchungu mkali sawa na uchungu wa hedhi. Mwanamke pia hushuhudia kuumwa na mgongo, kubanwa kwa tumbo na kuharisha. Hatua tatu za mchakato huu ni kubanwa kwa kizazi, kujifungua mtoto na sehemu ya placenta kutoka mwilini.
Ishara za kuanza kwa mchakato wa uchungu wa uzazi

Kuna aina ya kubanwa kunako fahamika kama Braxton-Hicks ambako ni uchungu wa uzazi usio wa kweli. Mara nyingi hudhaniwa kuwa uchungu wa kweli. Mchakato wa uchungu huu, huchukua kati ya masaa 12 hadi masaa 24. Hizi ndizo ishara za uchungu wa uzazi wa kweli.
- Maumivu makali ya mgongo
- Kuharisha
- Maumivu ya tumbo, sawa na ya hedhi
- Kuvuja kwa maji
- Kubanwa tumbo
Kujiandaa unapo enda hospitalini
- Chagua rafiki ama mwanafamilia atakaye kupeleka hospitalini na kukuegemeza
- Fanya mazoezi ya kuupumzisha mwili
- Jaribu kufanya yoga
- Jielimishe kuhusu kujifungua na kumtunza mtoto
- Kunywa maji tosha
- Koga kwa maji ya vugu vugu kuupumzisha mwili
Hatua ya kwanza

Katika hatua hii, kizazi kina kuwa chembacha kisha kupanuka hadi kuwa sentimita 10. Kuna vitu vitatu vinavyo tendeka katika hatua hii ya kwanza.
Hii ndiyo hatua iliyo ndefu zaidi. Hata hivyo haina uchungu mwingi. Kizazi cha mama kina kuwa chembamba kisha kupanuka hadi kuwa sentimita 3. Hatua hii huchukua masaa, siku chache ama hata wiki.
Katika hatua hii, kizazi hupanuka kutoka sentimita 3 hadi 8. Mama ana hisi kubanwa na uchungu mkali unao rudi baada ya kila dakika 3. Hatua hii ina uchungu mkali.
Hapa kizazi hupanuka kutoka sentimita 8 hadi 10. Kubanwa huwa mara zaidi na kuna uchungu zaidi. Mama ata hisi haja ya kwenda msalani kila mara.
Hatua ya pili

Hatua hii huanza baada ya kizazi kupanuka hadi sentimita 10 na kukamilika mtoto anapo zaliwa. Kubanwa katika hatua hii kuna chukua muda zaidi. Kubanwa kunapo fika kilele, huenda mama akahisi kusukuma mtoto atoke. Daktari ama mkunga atamshauri mama jinsi anavyo stahili kusukuma mtoto ili asishuhudie kuraruka anapo msukuma mtoto.
Kichwa cha mtoto kinapo toka, mkunga atamshika mtoto kwenye mabega na kuulekeza mwili wake ufuate mkondo.
Hatua ya tatu
Dakika 30 baada ya mtoto kuzaliwa, uterasi hubana ili kusukuma placenta nje ya mwili. Kisha misuli kupungua ili kukomesha kuvuja kwa damu. Hii ndiyo hatua ya mwisho ya uchungu wa uzazi katika mimba.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Je, Mama Atafahamu Vipi Anapo Karibia Kujifungua? Kubaini Leba Halisi