Vidokezo 21 Kuhusu Uchungu Wa Uzazi Na Kujifungua Kwa Wazazi Wa Mara Ya Kwanza!

Vidokezo 21 Kuhusu Uchungu Wa Uzazi Na Kujifungua Kwa Wazazi Wa Mara Ya Kwanza!

Nusu ya wakati ama wakati wote baadhi ya wakati, hautakuwa na wazo lakini niamini, ni vyema kukosa wazo darasani lakini sio katika chumba cha kujifungua.

Tuli zungumza na wanawake 21 walio na uraibu na waka tujuza vidokezo bora kuhusu uchungu wa uzazi na kujifungua. Hivi ni muhimu hasa kwa wazazi wa mara ya kwanza.

Vidokezo 21 vya uchungu wa uzazi na kujifungua

1.Usiende kwenye chumba cha uchungu wa uzazi ukiwa njaa

vyakula vinavyo wasaidia watoto kuongeza uzito

"Wakati wote hakikisha kuwa unakula kitu, chakula cha kawaida. Huwezi fanya kitu chochote ukiwa njaa." Alisema Teo Lin mwenye miaka 32.

2. Tumia misuli ya tumbo vyema, mama

Hadi pale utakapo pata maumivu kwenye makalio, sukuma kutoka kwa makalio yako. Lakini usipo, ni sawa kutumia misuli ya tumbo, hata kama bado haionekani!" Alisema Rodriguez Aarin mwenye miaka 35.

3. Fanya urafiki na wauguzi

"Ni kweli, ni kazi ya daktari kukusaidia na kujifungua, lakini ni wauguzi wako karibu masaa yote hadi pale utakapo jifungua. Hao wauguzi ndiyo wanao kuhimiza waki kuongoza. Kwa hivyo ni wao unao paswa kuwa marafiki nao." Kulingana na Elizabeth Lim, wa miaka 33.

4. Usiogope kwenda haja kubwa

"Jambo la kufurahisha ni kuwa kuenda haja kubwa kunasaidia kuharakisha mchakato wa uchungu wa uzazi. Kwa hivyo, afadhali kusukuma masaa matatu ama kuenda haja kubwa na kupata mtoto baada ya nusu lisaa? Uamuzi ni wako!" Alisema Hanifah wa miaka 29.

5. Usihisi uwoga kuchukua darasa kuhusu kujifungua mtoto

"Nusu ya wakati ama wakati wote baadhi ya wakati, hautakuwa na wazo lakini niamini, ni vyema kukosa wazo darasani lakini sio katika chumba cha kujifungua." Kulingana na Amanda Lee mwenye miaka 29.

6. Usikimbize epidural

"Pata epidural, lakini ngoja hadi unapo fikisha sentimita 5-6, uchungu wa uzazi unapo zidi." Alisema Priyanka, wa miaka 33.

7. Usione aibu kuonyesha hisia

"Hifadhi kuwa na nguvu kwa miaka mingi inayo kuja. Huu ndiyo wakati wa kupiga nduru, kulia na kila kitu unacho weza kufanya." Alidokeza Diyanah mwenye miaka 30.

8. Sahahu mipango ya "uchungu wa uzazi" ama "kujifungua"

"Ukweli, katika maisha yangu yote ambayo nimeishi, hakuna kitu kinacho enda kulingana na mpango. Kubali kufanya mabadiliko. Ichukue kutoka kwa uraibu wangu. Nilidhania kuwa nitajifungua kifungua mimba changu njia ya kawaida, lakini alifika miezi miwili kabla, kupitia upasuaji wa C-section!" alisema Foo Yi Ling, wa miaka 34.

9. Panga mkoba wako wa hospitali mapema

"Mapema! Anza kupanga unapo fikisha wiki 34. Ili kupunguza vikwazo vya dakika ya mwisho. Naam, hauna habari kama mtoto wako atafika mapema hivyo." Wan Xin mwenye miaka 28 alishauri.

10. Uliza maswali mengi

"Ongea na daktari wako hospitalini kuhusu ishara za kukwazwa kimawazo baada ya kujifungua, kuwa na wasiwasi na OCD. Unahitaji maarifa." Alisema Hafizah, 27.

11. Usijali watu wanavyo fikiria

"Kupitia upasuaji, njia ya kawaida ama kukosa madawa, haijalishi. Fanya kinacho kufaa na mwanao. Sio mashindano."- Siyathma, mwenye miaka 29.

Vidokezo zaidi kuhusu uchungu wa uzazi na kujifungua

Vidokezo 21 Kuhusu Uchungu Wa Uzazi Na Kujifungua Kwa Wazazi Wa Mara Ya Kwanza!

12. Jua unacho tarajia

"Naam, kwa hayo namaanisha, usifikirie uraibu utakuwa wa kufurahisha ama wa mapenzi. Nina maanisha kwa uhakika, utakuwa wa kufurahisha, lakini, hatutakosa kuona kuhisi kutapika, uchi, kuenda haja na uchungu hapa!" Naomi Tham mwenye miaka 32.

13. Usijali kuhusu vitu vidogo

"Watu watakuona ukiwa uchi na ndiyo, watakuwa wengi. Ni sehemu ya mchakato huo!" Kulingana na dada wa miaka 30, Cynthia Koh.

14. Weka kamera kando yako!

"Unakutana kwa mara ya kwanza na mtoto wako na ni LAZIMA kuweka hilo kwenye kamera. Hata usijaribu kubishana nami kuhusu hili."- Alisema Fatin wa miaka 30.

15. Unaweza jaribu hypnosis

"Mbinu za hypnosis huenda zika kuanzia uchungu wa uzazi bila dawa! Alisema Devi mwenye miaka 29.

16. Tumia diaper za watu wakubwa

"Diapers za watu wakubwa baada ya kujifungua huwa anuwai nzuri. Unalala vyema bila hofu kuwa unavuja damu ama kitu chochote." Kulingana na Nasuha, 25.

17. Kuwa na uamuzi

"Fikiria kuhusu uchungu huo kama kutimiza lengo. Fikiria kuwa kila unapo banwa una karibia kumpokea mtoto wako- huenda ukahisi uchungu mdogo." Kulingana na Kimberly Chua, mwenye miaka 36.

18. Fanya utafiti

"Fanya utafiti wa kujifungulia nyumbani, vituo vya kujifungua, hospitali, pitocin, chanjo, doulas, kunyonyesha, epidural na kadhalika. Fahamu hatari na manufa na kwa nini mambo yana fanyika yanavyo fanyika. FAHAMU KILA KITU." Alisema Maria wa miaka 29.

19. Chukua usukani

"Jambo la kuongeza ujasiri kwa kasi ni kufahamu kuwa umechukua usukani na katika kesi hii, wewe ndiye unaye ongoza. Usiwe na hofu ya kuonyesha uwezo huo. Kulingana na Nabilah, 35.

20. Mtafute mamako ukitaka

"Hakuna kinacho kuliwaza zaidi kuliko mguso wa mkono wa mamako. Kuwa na mama yako kando yako, akikuhimiza njia yote ni mojawapo ya uamuzi bora zaidi maishani." Alisema Lynn, 30.

21. Kuwa jasiri

"Hofu na shaka ni aina mbaya zaidi ya maadui ambayo akili yako inaweza kuwa nayo. Kufanya mwili uwe baridi kutafanya uchungu wa uzazi uwe mgumu zaidi. Wakati wote jikumbushe kuwa hili ni kawaida na mambo yote yatakuwa sawa." Kulingana na Michelle Goh, 26.

Soma PiaMama Anapaswa Kungoja Muda Upi Kufanya Ngono Baada Ya Kujifungua?

Written by

Risper Nyakio