Jinsi ya Kuepuka Uchungu Wa Uja Uzito Usio Komaa; Njia 11 za Kufuata

Jinsi ya Kuepuka Uchungu Wa Uja Uzito Usio Komaa; Njia 11 za Kufuata

Ni muhimu kwa mama aliye mja mzito kujitunza ili kuepukana na uchungu wa uja uzito usio komaa unao sababishwa na kufanya kazi nyingi kama vile kupiga deki. Ili kuyalinda maisha yake na ya mtoto.

Wamama, unapokuwa mja mzito, una majukumu mapya ya kupiga deki unayo faa kufikiria kuhusu. Kwa hivyo jambo la mwisho unalofaa kufikiria kuhusu ni uchungu wa uzazi ambao hauja komaa. Lakini ni jambo la muhimu kujua unavyo paswa kuliepuka tokeo hili kwa njia ya kawaida ili ujifungue mtoto aliye komaa na mwenye afya bora.

 Hili linasaidia kutokumbana na matatizo wakati wa kuzaa kwa mama na mtoto na pia baada ya kujifungua.

Jina hili uchungu wa kuzaa usio komaa ni ambapo mama anajifungua mtoto wake kabla ya wiki 37 baada ya kutunga mimba. Ina julikana kama muda uliokomaa japo mimba inapo fikisha wiki 37 ambapo mtoto amekomaa ipasavyo na anaweza ishi nje ya tumbo la mama. Uchungu usiokomaa unatendeka kunapo kuwa na kupanuka na kupunguka na kusababisha kufunguka kwa kizazi cha mama muda kati ya wiki 20 na wiki 37 ya uja uzito.

Walakini, wakati mwingine, wana wake hukuwa na uchungu wa uzazi usio komaa kufuatia sababu mbali mbali na kusababisha shida hili. Hizi ni baadhi ya njia bora zaidi za kuepukana na uchungu wa kuzaa usio komaa kwa njia ya kikawaida ili uweze kutimiza ndoto lako la kuwa na mama na mtoto wenye afya bora.

 

Njia 11 Za Kuepukana Na Uchungu Wa Kujifungua Usio Komaa Kwa Kikawaida

kuepukana na uchunga wa uja uzito usio komaa

 1. Ongea na daktari wako. Kama una historia ya uchungu wa kujifungua usio komaa hapo awali, ni muhimu kumjulisha daktari wako kwani hatari ya tukio hili liko juu zaidi. Daktari wako atahakikisha unapata malinzi bora zaidi.
 2. Kunywa maji mengi. Watu wengi wana puuza kunywa maji mengi wanapokuwa waja wazito. Ukosefu wa maji ya kutosha mwilini unaweza sababisha kupanuka na kupunguka kwa kizazi cha mama na kupelekea kupata uchungu wa uzazi usio komaa. Hakikisha una kunywa maji ya kutosha.
 3. Kunywa virutubisho. Ni muhimu kwako kuvichukua virutubisho vya hali ya juu ya vitamin unapo kuwa mja mzito ili kusaidia uja uzito wako kupata nutrients unazo hitaji. Kukosa vitu hizi mwilini kunaweza changia kupata Maumivu ya uja uzito yasiyo komaa.
 4. Tazama mlo wako. Chakula unachokula kina maathari kwa mwili wako na wa mtoto aliye tumboni. Vyakula visivofaa na visivyo na dhamana huchangia katika matatizo ya uja uzito kama vile kujifungua kabla ya wakati kufika na ugonjwa wa sukari ya kihisia. Ongeza bakteria bora mwilini kwa kuvila vyakula kama yoghurt, sauerkraut na kefir. Hizi ni murua kabisa katika kuviongeza vidudu hivyo mwilini na kusimamisha kuongezeka kwa vijidudu vibaya kwenye uke wa mama.
 5. Tembea. Mojawapo ya mazoezi bora zaidi ambayo unaweza fanya ni kutembea. Inasaidia mpigo wako wa moyo kuwa unavyo faa na kuongezeka kwa mzunguko wa damu mwilini.
 6. Fanya Yoga ya uja uzito. Darassa hizi zina funzwa na wataalamu watakao kusaidia kuboresha utendaji kazi wa mwili wako na pia mzunguko wa damu mwilini.
 7.  Kisafishe kibofu chako cha mkojo. Kuukaza mkojo utachangia katika kufanya kibofu chako cha mkojo kuongezeka. Na kupata vijidudu itakayo kuwa na athari hasi mwilini na kwa uterasi. Tumia msalani mara kwa mara.
 8. Jizuie kulala kwa mgongo. Una shauriwa kulala kwa pande unapo lala kwani inachangia katika kuongezeka kwa mpigo wa damu mwilini. Kulala kwa mgongo kuna weka mkazo kwa uti wa mgongo na kuifanya uterasi kupanuka.
 9. Oga kwa maji moto. Kuoga kwa maji moto katika digrii 36 celsius kuna saidia kuutuliza mwili na misuli. Hii ni njia nafuu ya kuituliza uterasi wakati wa jioni unahisi una fikira nyingi na hujatulia.
 10. Jipe muda wako. Pewa massage ya uja uzito mara kwa mara. Ni njema kwa mwili na akili kutulia unapo toa mawazo mengi akilini.
 11. Uskize mwili wako. Usifanye kazi nyingi inayo weka mkazo kwa tumbo yako ama inayo kufanya kuhisi uchovu. Hakikisha unapata usingizi wa kutosha na uukubalishe mwili wako kuzoea wakati huu wa ujauzito.

Read Also: Midwife suspended after delivering premature twins at home birth

 

Written by

Risper Nyakio