Ongezeko La Udanganyifu Katika Ndoa Na Kinacho Sababisha!

Ongezeko La Udanganyifu Katika Ndoa Na Kinacho Sababisha!

Ni vigumu kuhalalisha udanganyifu katika ndoa kwa sababu yoyote ile. Walakini, kuelewa sababu kwa nini watu hufanya hivi angalau kutakusaidia kuwaelewa.

Ni vigumu kuhalalisha udanganyifu katika ndoa kwa sababu yoyote ile. Walakini, kuelewa sababu kwa nini watu hufanya hivi angalau kutakusaidia kuwaelewa.

Haijalishi jinsi udanganyifu katika ndoa umekuwa maarufu, bado ni vibaya. Hata kama ina onekana kuwa tabia inayo shika kasi katika jamii, ni tabia inayo paswa kukemewa.

Hakuna jina mbaya linalo weza kuelezea watu wanao danganya katika uhusiano na ndoa haijalishi lilivyo. Lakini, tunaweza tuliza ghadhabu zetu na kujaribu kuelewa sababu zinazo wapelekea kufanya hivi.

Kwa nini watu hudanganya? Je, inaonekana kwao kuwa jambo la kusisimua kuwaumiza wengine hisia na kuharibu maisha yao, ama kuna sababu zisizo epukika zinazo wawezesha kufanya hivi?

Tazama baadhi ya sababu zinazo sababisha udanganyifu katika ndoa

udanganyifu katika ndoa

  1. Kukosa kuwajibika katika ndoa

Huenda ikawa kuna watu walio zoea kuishi maisha kivyao na hata baada ya kufunga ndoa, wanaendelea kuishi maisha kana kwamba hawana mchumba maishani. Unapo fanya uamuzi wa kuwa katika uhusiano na mtu yeyote, ni vyema kuwajibika na kuwa mwaminifu.

2. Hamu ya kutaka kutoka nje

Kwa walio na nyoyo zenye hamu ya kujaribu mambo mapya, huenda waka taka kujua inavyo hisi kutoka nje ya ndoa, bila kufikiria kuhusu madhara watakayo fuata tendo hilo.

3. Kutaka kudekezwa na kupatiwa muda

Baadhi ya watu hujipata wakitafuta wenzi wengine nje ya ndoa baada ya kukosa kupatiwa wakati tosha ama kudekezwa wanavyo taka na wachumba wao.

uhusiano unao dumu

4. Kuto ridhishwa

Matarajio yao waliyo kuwa nayo akilini kabla ya kuingia kwenye uhusiano haya kutoshelezwa. Na kuwafanya wazidi kuendelea kutafuta walicho kitaka hapo awali.

5. Mahitaji ya kimapenzi kuto toshelezwa

Hapa tuna maanisha, hamu ya ngono ya kawaida isipo toshelezwa. Hii ni mojawapo ya sababu kuu inayo wafanya wanandoa wengi kutoka nje ya ndoa na kwenda kutafuta wachumba wengine nje watakao tosheleza hamu zao za ngono.

6. Kulipiza kisasi

Mwanandoa mmoja anapo toka nje na mwenzi wake kugundua, huenda akatafuta mtu mwingine nje pia ili alipize kisasi.

Ni vyema kukumbuka kuwa makosa mawili haya fanyi hali kuwa bora zaidi, ila mambo yana zidi kuharibika zaidi. Na hakuna njia ya kuhalalisha uovu wa udanganyifu katika ndoa.

Kuna sababu zingine zaidi zinazo wafanya watu kutoka nje ya ndoa ama kuwa na wachumba zaidi ya mmoja. Kumbuka kuwa kamwe jambo hili halikubaliki na sio sawa kwani unamwumiza mwingine.

Soma PiaJinsi Kufikiria Sana Kutakavyo Haribu Uhusiano Wako

Written by

Risper Nyakio