Macho Ya Pinki Kwa Watoto: Jinsi Ya Kutibu Conjunctivitis Kutumia Matibabu Ya Kinyumbani

Macho Ya Pinki Kwa Watoto: Jinsi Ya Kutibu Conjunctivitis Kutumia Matibabu Ya Kinyumbani

Learn to detect the signs of pink eyes. Find out when you should take your kid to the doctor and which home remedies you can use to soothe sore eyes.

Wakati ambapo mtoto wako anaamka akijikuna macho. Chini ya kutu ya njano kuna rangi nyekundu na pinki. Iwapo wenye ni mama mwenye maarifa, utafahamu kuwa huu ni ugonjwa wa conjunctivitis ama macho ya pinki. Wamama kutoka vijijini wanaifahamu hali hii kama Apollo. Hali hii huonekana mbaya zaidi ya ilivyo.  Ugonjwa huu ni kama homa haufai kukupatia mawazo mengi na kwani inaweza tibiwa kwa urahisi nyumbani. Lakini kuna wakati ambapo unapaswa kumtembelea daktari wako kuhusu ugonjwa huu. Tunakuelezea zaidi katika makala haya.

hali ya conjunctivitisJe, conjunctivitis ni nini?

Conjunctivitis inamaanisha uchochezi wa conjunctiva, ambayo ni ngozi nyembamba inayofunika mboni na ndani ya kope.Macho ina duct ya machozi, tezi ya makamasi ilikuifanya iwe na mafuta. Mchakato huu ukizidiwa unaeza pita kiasi.Macho yaweza anza kutoa machozi na makamasi ya kujikinga na kusababisha kufura macho. Hizi ni baadhi ya ishara za ugonjwa huu wa conjunctivitis.

Nini kinacho sababisha ugonjwa huu?

ugonjwa wa conjunctivitisMaambukizi, ni sababu kuu inayo sababisha ugonjwa huu wa conjunctivitis. Hali hii huambukizwa sana sana katika shule na husababishwa na bacteria ama maumbikizi ya virusi. Huambukizwa na tone la makamasi inayoenezwa kupitia kuchemua ama kukohoa.Kulingana na wataalam wa kiafya ukiona usaha kando na macho ukiwa wa rangi ya njano. Inasababisha na bacteria kama vile Golden staph (lakini inaweza tibiwa na viuajiasumu).Usaha ukiwa mweupe,virasi inaweza kuwa inasababisha shida hii.Mzio- Hii ni sababu ya kawaida inayosababisha kufura macho. Watu ambao wana mzio kwa poleni wanaweza pata conjunctiva ambayo ni nyekundu.Vikeri - Vitu kama chlorine inayopatikana katika bwawa la kuogolea inaweza sababisha kuongezeka kwa conjuctiva.

Ishara za ugonjwa wa conjunctivitis

conjunctivitis

  • Jicho moja au zote mbili kuwa nyekundu au pinki.
  • Kunata kwa kope wakati unaamka.
  • Kutu kuwa ya rangi ya njano kwenye kope.
  • Usaha mweupe au njano kwenye macho.
  • Kujikuna au kuadhiriwa na mwangaza.
  • Homa au kufura limfu karibu na maskio.

Jinsi ya kutibu macho iliyo fura

ugonjwa wa conjunctivitisMara nyingi, ugonjwa huu wa conjunctivitis sio hatari ila una enezwa kwa urahisi. Iwapo mtoto wako ana ugonjwa huu, ni bora zaidi akae nyumbani hadi macho yake yanapo pona.

Iwapo ungependa kujaribu mbinu tofauti za kinyumbani za kupunguza uchungu wa mwanao, tuna himiza ujaribu yafuatayo:

– Yakubalishe machozi yake yaoshe vijidudu hivi! Naam, hiyo ni kweli. Machozi yana kemikali zinazopigana na vijududu na viini hivi. Bila matibabu yoyote. Visa vinga vya conjunctivitis ya kuambukiza vinaisha kwa kipekee baada ya siku 2-5 na kwa ujumla, havipitishi wiki 1 ama 2.

– Vijitambaa vilivyo baridi ama vyenye joto. Hakikisha kuwa mwanao amefunga jicho lake kisha uwekelee kijitambaa hiki kupunguza uchungu. Wataalam wanahimiza kutumia vijitambaa vilivyo baridi kwa conjunctivis ya mzio na vijitambaa vyoto kwa maambukizo.

– Safisha macho ya mwanao kutoka upande wa ndani (karibu na pua) na upande wa nje kwa kona na tishu zilizo na maji ama chai chamomile iliyo pikwa na kuachwa ipoe.

– Tumia vyakula vya kuponya kama vile machungwa, cantaloupe, matunda ya kiwi, ya strawberry na broccoli kwenye lishe ya mwanao.

– Maziwa ya mama haisaidii kuimarisha mwanao pekee ila pia ni tiba ya kinyumbani ya macho yaliyo fura. Tumbukiza kijitambaa kisafi ama tishu kwenye maziwa ya mama iliyo kamuliwa. Kisha utumie kusafisha jicho la mwanao kwa njia sawa na ile ya kutumia maji.

–Dawa za Uchina ni njia bora ya kutibu macho yaliyo fura. Daktari wa kiasili wa matibabu ya kichina(TCM) atamchunguza mwanao. Baada ya kutambua ugonjwa, ata shauri matibabu bora ya ugonjwa wake.

wakati bora wa kumtembeza mwanao aliye fura macho kwa daktari

Macho mekundu katika watoto husababishwa na virusi. Kwa mara nyingi, huambatana na ishara za mafua ama homa. Kwa ujumla, wazazi wanapaswa kuwapeleka watoto wao kwenye kituo cha hospitali iwapo hawahisi vyema. Ama iwapo hali yao haibadiliki baada ya siku 3-5 za mapumziko. Walakini, iwapo, mtoto wako anateta kuhusu uchungu wa jicho ama kuto ona vizuri, ni muhimu kumtembelea daktari kwa kasi.

Ikiwa mtoto wako mchanga ana hali hii ya conjunctivitis, mtembeze hospitalini bila kukawia. 

Virusi zinavyo julikana kama chlamydia ama gonorrhia huenda vikasababisha conjunctivitis katika watoto wachanga. Virusi hivi vina ambukizwa kupitia ngono na mama huenda akaupitisha kwa mtoto mchanga. Hii ni iwapo, ana mojawapo ya magonjwa haya anapo jifungua.

Hii ni tofauti sana na jicho la mnato katika watoto wachanga inayo sababishwa na duct ya machozi iliyo funikwa. Hii haitasababisha jicho kuwa lekundu ama kufura kwa conjunctiva.

Iwapo mwanao analia kuhusu uchungu mwingi, ni vyema kumpeleka kwa daktari.

Daktari anaye mshughulikia mwanao kwa ujumla atatibu jicho lililo fura kwa kutumia antibiotic eye drop ama dawa ya kupaka ya macho. Kulingana na uwingi wa hali ya conjunctiva, daktari atashauri njia nyingine ya matibabu.

Wazazi, iwapo mwanao anaugua ugonjwa huu wa conjunctiva, kumbuka kumhimiza anawe mikono kila mara. Mkumbushe kutumia maji moto na sabuni. Pia, washauri kuto gawa chakula chao ama midoli yao na watoto wengine (pamoja na ndugu zao). Hii itasaidia kupunguza kueneza kwa maambukizi kwa watu wengine.

CDC

Also read: Study Says Breast Milk Has Cancer Dissolving Properties

 

Written by

Risper Nyakio