Unaufahamu Ugonjwa Wa Listeria Katika Ujauzito?

Unaufahamu Ugonjwa Wa Listeria Katika Ujauzito?

Mtoto hupitishwa chakula na maji kupitia kwa mfuko wa mimba na vitu hivi vinapo pita, ako katika hatari ya kuambukizwa maradhi ya listeria.

Ugonjwa wa listeria unasababishwa unapo gusa bakteria inayo fahamika kama listeria. Kupitia kwa chakula kilicho na bakteria hizi ama hata kwa udongo, maji na kinyesi. Mama mjamzito ako katika hatari kubwa zaidi ya kuugua maradhi haya. Kinga ya mwili hukua duni mama anapo pata mimba na ako katika hatari kubwa ya kuugua magonjwa tofauti. Mama ako katika hatari mara 20 zaidi ya kuugua maradhi ya listeria.

Dalili za listeria kwa mama mjamzito

ugonjwa wa listeria

Ugonjwa wa listeria una dalili sawa na mafua

 • Homa
 • Uchungu kwenye misuli
 • Kuhisi baridi
 • Kuendesha ama kuharisha
 • Kichefuchefu

Ni vyema kukumbuka kuwa dalili hizi zinaweza kaa hata baada ya wiki 10 baada ya kugusana na bakteria zinazo sababisha listeria. Mama mjamzito ana shauriwa kuenda hospitalini anapo hisi kuwa ana homa ili kufanyiwa vipimo kuhakikisha kuwa bayana hana maradhi ya listeria. Kuna wanawake ambao pia hawaonyeshi dalili za ugonjwa huu hadi pale unapo sambaa sana na kuanza kuathiri shingo, kuanza kutetemeka ama kuugua maumivu mengi ya kichwa.

Ugonjwa wa listeria unaweza dhuru mtoto tumboni?

Maambukizi yanaweza kumwathiri mtoto na ni hatari sana kwake. Mtoto hupitishwa chakula na maji kupitia kwa mfuko wa mimba na vitu hivi vinapo pita, ako katika hatari ya kuambukizwa maradhi haya. Ama wakati mama anapo jifungua.

Mama anapo gundua kuwa una ugonjwa huu, ni vyema kupata matibabu mapema kupitia kwa antibiotics ili kumlinda mtoto wake. Yasipo tibiwa kwa haraka, ugonjwa huu wa listeria una hatari ya kusababisha vitu hivi:

 • Mimba kuharibika
 • Mama kujifungua kabla ya wakati
 • Mtoto kukufia tumboni ama stillbirth

Huenda mtoto akaonyesha ishara za ugonjwa huu punde tu anapo zaliwa ama baada ya wiki chache. Mtoto aliye athiriwa na ugonjwa huu ata hisi uchungu mwingi baada ya kuzaliwa, kuugua nimonia, matatizo ya kupumua ama hata uti wa mgongo.

Jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huu

maji tosha mwilini ukiwa na mimba

Kuwa makini na chakula unacho kila kisiwe na bakteria hizi za listeria, kama vile:

 • Kunywa maziwa ambayo haina vidudu ama yaliyo pasteurised
 • Nyama iliyo pikwa ika iva vizuri
 • Safisha mikono vizuri kabla na baada ya kupika
 • Safisha matunda vizuri kabla ya kuyala
 • Kula chakula kilicho iva vizuri

Unapogundua kuwa una dalili za ugonjwa huu, wasiliana na daktari wako bila kusita. Jikinge dhidi ya bakteria hizi uwezavyo ili kuyasalamisha maisha na afya ya mtoto wako.

Chanzo: WebMd

Soma Pia:Vyakula Vya Mimba: Umuhimu Wa Kalisi Katika Ujauzito

Written by

Risper Nyakio