Matatizo Ya Ugumba Na Jinsi Ya Kuya Jadili Kwa Uwazi

Matatizo Ya Ugumba Na Jinsi Ya Kuya Jadili Kwa Uwazi

Bwana aficha hali yake ya kuwa gumba baada ya kufanya utaratibu wa vasektomi. Bibi akasirika baada ya kujua ukweli huu na kutishia kumpa talaka.

Wanandoa wengi huchelewesha kupata watoto kufuatia sababu tofauti. Siku hizi, ni kawaida kwa mwanamke kupata kifungua mimba chake akiwa miaka ya kati ya thelathini. Walakini, miaka yenye ‘rutuba’ ya uzalishaji katika wanawake huwa miaka yake ya 20 (ya mapema hadi mwisho). Anapofikisha miaka yake ya 30, uzazi (uwezo wa kupata mimba) huanza kupunguka. Kupunguka huku huwa kwa kasi zaidi unapo fikisha miaka ya kati ya 30 na ugumba katika miaka yako ya 30 sio jambo geni.

Ugumba katika miaka yako ya 30s

Changamoto za ugumba huumiza na kujaribu mbinu ya IVF ni hatua ambayo ina hitaji fedha nyingi na hisia.

Wakati ambapo mwanamke ambaye alikuwa anajaribu kupata mtoto bila mafanikio kwa muda mrefu aligundua kuwa bwanake alimfichia ukweli, bila shaka alihisi vibaya.

Ukweli ulifichuka

Ukweli ni kuwa alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kisiri wa vasektomi kabla ya kufunga ndoa. Kwa sasa, mwanamke huyo amekasirika sana na anataka waachane.

“Bwanangu wa miaka 50, alifanyiwa utaratibu wa vasektomi miaka 10 iliyo pita alipokuwa ameoa bibi yake wa kwanza. Tulipo patana miaka 5 iliyo pita, hakuniambia habari hizi na tulifunga ndoa miaka 3 iliyo pita,” alieleza katika Reddit.

“Tumekuwa tukijaribu kupata mtoto, bila mafanikio yoyote hadi tukaamua kujaribu IVF mwaka wa 2018 Disemba, ambayo haikufaulu.

Mwezi uliopita, nili angalia vipimo vyetu vyote na wazo likanijia kuwa kiwango sufuri cha manii yake mara nyingi kwenye kipimo chake cha manii sio kawaida na nika shuku vasektomi.”

Alipo mwuliza bwanake, alikubali kuwa alifanyiwa utaratibu wa vasektomi lakini akasema kuwa alikuwa na matumaini kuwa hali hiyo “inge jirekebisha kiasili.”

infertility in your 30s

Mwanamke huyo alijaribu utaratibu wa IVF bila mafanikio. | Chanzo: Pxhere

Mwanamke huyo alihisi uchungu

“Nime kasirika sana, na kuumia kwani alinikubalisha kuyapitia hayo yote na kuumia kihisia nikifikiria kuwa nilikuwa gumba na hata kutoa wazo la IVF wakati ambapo alifahamu tatizo la kuto pata watoto lilikuwa utaratibu wake wa vasektomi,” aliandika.

“Ni vigumu kumwamini sasa. Mngeshauri nibaki ama nimpe talaka na nitafute mtu mwingine ambaye atakuwa mwaminifu kwangu na ambaye najua nitapata watoto naye. Nahisi nime danganywa na wakati hauko upande wangu. Sijui nifanye nini.”

Habari yake kwenye mtandao ilipata majibu zaidi ya 200, huku watu wengi wakiwa kwa upande wa mwanamke huyo na kusema kuwa kitu ambacho bwanake alifanya hakiwezi samehewa.

Mazungumzo kuhusu ugumba na kutaka kupata watoto yana paswa ku zungumziwa kwa uwazi na mwenzi wako ili nyote muwe na uelewano na kuegemezana katika uamuzi mtakao ufanya.

Njia za kuzungumza kuhusu ugumba na mwenzi wako

  1. Epuka lawama

 Haijalishi aliye na ugumba. Hili ni jambo lililo juu ya uwezo wenu. Mfanye mchumba wako aamini kuwa mko kwa jambo hili pamoja. Kumbuka unavyo hisi kuhusu mchumba wako, kwa nini unampenda, kwa nini unataka kupata mtoto nao.

  1. Ongea kwa uwazi

Jadili kuhusu hisia zako kwa uwazi. Masomo yana onyesha kuwa wanandoa wanao ficha hisia zao wana uwezekano zaidi wa kuwa na matatizo yanayo husika na ugumba.

  1. Fahamu kuwa nyinyi ni timu

Lengo lako la kwanza linapaswa kuwa kuelewa tatizo vizuri mkiwa pamoja, kwa hivyo unaweza penda kuanza mazungumzo kwa kusema “Nina shaka na nafikiria tunapaswa kujadili jambo hili na daktari.” Mnaweza pata msaada kutoka kwa mtaalum kuwasaidia kuendeleza mazungumzo yenu.

infertility in your 30s

Ugumba katika miaka yako ya 30: ” Chanzo: Pxhere

  1. Zungumza kuhusu majonzi yenu

Kuwa mwaminifu unapo ongea kuhusu hisia zako na ni sawa kuwa na huzuni. Ikiwa mmoja wenu ana historia ya kukwazwa kifikira ama shaka, ongea na mwenzi wako kuhusu mabadiliko yoyote ya hisia ama tabia unazo gundua kwako ama kwa mwenzi wako. Jaribu kuepuka kuongea mambo hasi kujihusu ama mwili wako.

     5. Kuweka uhusiano ukiwa wenye afya

Pumzisha juhudi zako za kujaribu kupata mimba. Kupunguza mawazo katika uhusiano wenu wa kimapenzi sasa kuta hakikisha kuwa maisha yenu ya kimapenzi yatakuwa chanzo cha kuwasisimua na kuwapumzisha kwa miaka mingi ijayo. Jaribu kufanya mitindo ya ngono ya kusisimua na lengo lenu lisiwe kupata mtoto.

CHANZO: Mayo Clinic

Soma Pia: Orodha Ya Tembe Za Kukusaidia Kupata Mimba

Written by

Risper Nyakio