Hali Ya Ugumba Kwa Wanawake Na Kulisuluhisha

Hali Ya Ugumba Kwa Wanawake Na Kulisuluhisha

Kuna vyanzo vingi vya ugumba kwa wanawake. Lakini vyanzo vinavyo julikana sana ni kutatizika kupevusha yai, mirija ya uzazi.

Ugumba ni hali ambayo mwanamke hana uwezo wa kujifungua na kwa wanaume, hawana uwezo wa kuzalisha mwanamke. Hili ni tatizo sugu ambalo hata ingawa halija zungumziwa sana kwa vyombo vya habari, linawakumba watu wengi, wanawake kwa waume. Lakini leo tuna zungumzia kuhusu ugumba kwa wanawake.

Hili ni tatizo linalo wakumba mmoja kati ya wanawake 6 walioko katika ndoa. Kwa sababu tofauti, kuna wanawake wanao shindwa kujifungua.

Kipi Chanzo Cha Ugumba Kwa Wanawake?

ugumba kwa wanawake

Kuna vyanzo vingi vya ugumba kwa wanawake. Lakini vyanzo vinavyo julikana sana ni kutatizika kupevusha yai, mirija ya uzazi kuwa na matatizo ama magonjwa ya mlango wa uzazi. Kuna umri ambao mwanamke akitimiza ana tatizika kupata mimba.

Sababu za matatizo ya kupevushwa kwa yai

 • Kuvimba kwa mfuko wa mayai
 • Kutumia madawa ya kulevya ama pombe
 • Kuwa na tezi la thyroid
 • Kusongwa kimawazo
 • Mabadiliko ya homoni mwilini
 • Mzunguko mfupi wa kipindi cha hedhi
 • Upungufu wa mafuta mwilini kufuatia mazoezi makali

Kuharibika kwa mirija ya uzazi ama tubu za falopian kuna sababishwa na:

 • Kuvimba kwa nyonga
 • Maradhi ya endometriosis ama kuvimba kwa fuko la uzazi
 • Maambukizi ya nyonga ya hapo awali
 • Magonjwa sugu ya muda mrefu
 • Mimba ya hapo awali ya kutunga mimba nje ya uterasi

Je, mwanamke atawezaji kutambua iwapo ana tatizo la ugumba?

ugumba kwa wanawake

Kwa kufuatia vipimo hivi:

 • Kipimo cha mkojo ama damu kuona iwapo homoni mwilini ziko sawa
 • Sampuli ya ute kutoka kwa kizazi cha mwanamke kudhibitisha iwapo yai linapevushwa mwilini
 • Kipimo cha nyonga kudhibitisha iwapo mwanamke anaweza beba ujauzito bila tatizo
 • Kipimo cha ultrasound kuangali hali ya uterasi ama mfuko wa mimba na fuko la mayai

Je hali ya ugumba inaweza tibika?

Kuna njia tofauti ambazo zinatumika kurekebisha hali ya ugumba katika wanawake. Kama vile:

 • Matumizi ya tembe za homoni kusawasisha homoni mwilini
 • Virutubisho vya kusaidia kuongeza uwezo wa kutunga mimba
 • Dawa za kuhamasisha upevushaji wa yai

Njia za kujikinga dhidi ya ugumba

 • Epuka kutumia madawa ya kulevya
 • Jikinge dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ya kingono
 • Punguza utumiaji wa pombe nyingi
 • Kula lishe yenye afya

Chanzo: healthline

Soma Pia: Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Miaka Zaidi Ya 35

Written by

Risper Nyakio