Habari Kuhusu Uhusiano Wa Snoop Dogg Na Binti Laurie Holmond

Habari Kuhusu Uhusiano Wa Snoop Dogg Na Binti Laurie Holmond

Ni vigumu kuongea kuhusu binti Laurie Holmondbila kumtaja mpenzi wake wa shule ya upili Snoop Dogg. Yeye ndiye kisa na maana tunamjua Laurie leo. Snoop na Laurie walikuwa pamoja hadi pale ambapo Snoop alifunga ndoa kwa ghafla katika mwaka wa 1997. Laurie Holmondalisikia habari za harusi ya mchumba wake kama watu wengi- kwa redio.

Laurie Holmond

Vyanzo: incolours.club

Alienda kwa Snoop na habari hizi za kushtua, ila Snoop aliitikia habari hizi na kumwambia kwamba hangeelewa. Laurie Holmondaligundua kwamba alikuwa amefunga pingu za maisha na mtu mwingine na akashtuka. Ila miezi mitatu baada ya harusi, wawili hawa walipatana kwa muda mfupi katika hoteli ya La Reve huko Hollywood.

Kupatana huko kwa muda mfupi kulipelekea kupata mimba, miezi tisa baadaye, Laurie Holmondalijifungua mtoto wa kiume wa Snoop, Julian Corrie Broadus. Kwanza, Snoop alikuwa na wasiwasi kuhusu kumjulisha bibi yake Shante habari hizi, ila alikuwepo wakati mtoto wake alizaliwa. Hata Laurie alimpongeza kwa kuyatimiza majukumu ya mtoto wake katika siku za hapo awali. Kwa wakati mrefu, sehemu kubwa ya dunia haikujua kuweko kwa Julian. Miaka baada ya kuzaliwa kwake, kurasa za umbea wa watu mashuhuri zilikuwa na habari nyingi kuhusu mtoto wa siri wa Snoop. Habari moto zaidi kuhusu ulezi zilikuwa kwamba Snoop alikuwa amewacha kumtembelea mwanawe na Laurie.

Laurie Holmond

Snoop Dogg. Vyanzo: LaineyGossip.com

Je, yapi ya hivi punde kumhusu binti Laurie Holmond?

Kwa kuwa alikuwa katika mahusiano na mtu mashuhuri kuna maana kuwa kwa wakati wowote ule, jina lake litahusishwa na Snoop. Mbali na kujulikana kama mchumba wa hapo awali wa Snoop na mamake Julian Corrie Broadus, Laurie Holmondni nani?

Kwa sehemu kubwa, Laurie amebaki kuwa mbali na vyombo na habari mbali na vituko vinavyo fuatana kwa asili unapokuwa na mtoto wa mwanamuziki mashuhuri na uvumbuzi wa habari hizi kwenye vyumba vya habari. Mwanamke huyu wa miaka arobaini na sita alikuwa wa kwanza kuitikia kuwa Snoop alikuwa tayari kuyachukua majukumu yake Julian alipo zaliwa. Walakini, alihojiwa mara nyingi na kusema kuwa mwanamuziki huyu hana uhusiano wa karibu na kijana wake.

Jinsi Laurie alivyo dhihirisha mtoto wa siri wa Snoop Dogg kwa vyumba vya habari

Familia ya Broadus ina programu yenye fanaka ya maisha ya kisasa inayo itwa Snoop Dogg Father Hood iliyo anzishwa mwaka wa 2007. Ina elezea zaidi kuhusu yeye kuwa mwana familia wa kupendeza. Picha hiyo ya kwanza ya familia ilimshika kila mtu na wakaamini jinsi alivyo onekana kwenye televisheni. Hadi pale ambapo habari za kijana wake wa siri zilipo ibuka kwenye vyombo vya habari.

Dunia iligundua kwamba mwanamziki huyu alipata mtoto wa kiume na mwanamke ambaye hakuwa Shante. Ugunduzi huu ulileta umbea wa Laurie Holmondkwenye laini ya kwanza. Picha na mtazamo wa Snoop ulibadilika kabisa baada ya uhusiano huu kujulikana.

Kuna ripoti kuwa ndoa yake na Shante ilikuwa karibu kufika tamati mwaka wa 2004 baada ya bibi yake kugundua kuhusu kuweko kwa Julian. Snoop Dogg anakisiwa kuwa alianza utaratibu wa kutengena na bibi yake, na hapo baadaye kubadili kauli yake baada ya familia yake kutatua suala la habari za mtoto wa siri.

Laurie

Julian Corrie Broadus. Source: heightline.com

Julian ambaye ni kijana wake Laurie asema kuwa hana uhusiano na babake

Julian Corrie Broadus hana woga kumwita Snoop Dogg ambaye hajakuwa akitimiza majukumu yake kama mzazi. Kulingana na vyanzo kuhusu umbea wa binti Laurie Holmond, Julian alitaka kuhusika katika maonyesho ya babake ya runinga, ila jambo hili halikuwa litendeke.

Kwa sasa kwani Julian ana umri mkubwa zaidi, ana haya ya kusema kuhusu uhusiano wake na babake: “Kwa sasa kwani nina umri zaidi, akili yangu sio nzito kama hapo awali.”

Katika mwaka wa 2018, kijana wake Laurie Holmondalitia saini mpango wa kuimba kwa jina la ki usanii la Teen Snoop.

Maudhui Ya Uhusiano Ya Kusoma Kutoka Kwa Hadithi Ya Mapenzi Ya Snoop Na Laurie Holmond

  • Mioto ya kitambo ni rahisi kuwasha tena, kwa hivyo sio jambo la busara kuwa na urafiki wa karibu na mchumba mliye wachana naye.
  • Huenda ukawa mchumba wa kando maarufu kama side chick bila kujua.
  • Ndoa sio sababu kamili kwa mwanamme kuwa mwaminifu.
  • Wanawake wengine watamtaka bwanako kwa sababu ameoana.
  • Kama Snoop na bibi yake, huenda bado ukawa na ndoa ya mafanikio baada ya mmoja wenu kutoka nje ya ndoa.

Kumbu kumbu: snoopdogg.com

Soma pia: Were these Kenyan teenage girls switched at birth?

Written by

Risper Nyakio