Watu wanaokula lishe ya mboga pekee ama vegans wanajitenga na ulaji wa nyama hasa nyama zinazotokana na wanyama, maziwa na bidhaa za maziwa na mayai. Kwani protini za wanyama huwa na ufuta mwingi na kalori nyingi. Tunadadisi ukweli iwapo kuna uhusiano kati ya lishe ya mboga na kupoteza uzito wa mwili.
Lishe ya mboga na kupoteza uzito wa mwili

Kulingana na utafiti uliofanyika, watu wanaozingatia lishe za mboga walionekana kuwa na body mass index maarufu kama BMI ya chini. Yenye maana kuwa lishe ya mboga husaidia kupunguza uzito wa mwili. Watu waliozingatia lishe hii walishuhudia afya bora ikiwemo kupunguka kwa viwango vya kolesteroli mwilini na hatari ya kupata ugonjwa wa saratani.
Manufaa ya lishe za mboga
- Kupunguka kwa nafasi za kupata saratani
- Kupunguka kwa cholesterol
- Kupunguza hatari ya kupata kisukari
- Kupunguza glucose ya damu
- Kupunguka kwa mwako ama inflammation
Hata kama lishe za mboga zina manufaa mengi ya kiafya, huenda zika waweka wanaozitumia katika hatari. Kama kuwa na upungufu wa kalisi, iron, vitamini C, vitamini D na protini. Ili kuepuka hatari hizo, wanaozingatia lishe ya aina hii wanashauriwa kuhakikisha wanatafutana vyakula mbadala vya nyama, nafaka nzima, soy, oats na almond na pia tembe za nyongeza ama supplements.
Kutumia lishe ya mboga kupunguza uzito wa mwili

Ili mbinu hii ya kupunguza uzito iwe na mafanikio, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
Kupunguza ama kuepuka ulaji wa chakula kilicho chakatwa. Vyakula vingi vilivyo chakatwa huwa na idadi kubwa ya kalori, na kufanya iwe vigumu kupoteza uzito wa mwili.
Kula kiwango kidogo cha chakula. Badala ya kula sahani mbili za chakula kwa siku moja, ni vyema kula mara tatu ama nne kwa siku. Kila mara kuhakikisha kuwa unatumia sahani ndogo.
Kufanya mazoezi. Mazoezi ni muhimu katika kupunguza uzito na kuboresha afya. Mazoezi yanaweza kuwa mepesi kama kutembea, kuogelea ama kufanya kazi zaidi badala ya kukaa chini siku nzima.
Kupunguza ufuta unaoongeza kwenye chakula. Kuweka ufuta mwingi kwenye chakula kunapigana dhidi ya juhudi za kupunguza uzito.
Lishe ya mboga huchukua muda kutengeneza kisha juhudi kuifuata. Kufanya hivi kunakupa maarifa zaidi kuhusu kila chakula unachotia mdomoni. Kula lishe ya mboga pekee kunasaidia kupoteza uzito, kwani lishe haina vyakula vingi vilivyo chakatwa ama bidhaa za maziwa zinazochukua muda mrefu kuchakatwa.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi