Uhusiano Kati Ya Kula Mihogo Na Kupata Mapacha

Uhusiano Kati Ya Kula Mihogo Na Kupata Mapacha

Kula mihogo na kujifungua watoto mapacha kuna andamana. Kulingana na utafiti, mji unao kuwa na idadi kubwa zaidi ya mapacha hula mihogo zaidi.

Iwapo wewe ni mwanamke katika umri wa kupata watoto, ni vyema kufikiria kwa makini kabla ya kutupa sahani hizo za mihogo. Huenda ukapata mimba ya mapacha. Mitaa inayo kuwa na rekodi ya juu zaidi ya watoto mapacha mara nyingi huwa na ulaji mwingi wa mihogo.  Mihogo na watoto mapacha zinahusiana vipi?

Somo lililo fanywa na mtaalum wa afya ya wamama kutoka Britain, Patrick Nylander kati ya miaka ya 1972 na 1982. Alirekodi wastani wa mapacha 45-50 kwa kila kuzaliwa kwa 1000 huko Kusini Magharibi. Utafiti wa hivi majuzi una kisia kuzaliwa kwa mapacha katika kila watoto 22 wanao zaliwa.  Nambari hizi ni kubwa kwa mara nne ikilinganishwa na sehemu zingine zozote duniani. Hili ni jambo la kupongezwa. Lakini hakuna mtu aliye na uhakika kwa nini mji wa Oyo huko Nigeria una mapacha wengi zaidi ikilinganishwa na mahali popote pale duniani. Walakini, watafiti wame kisia kuwa lishe yao ina eleza utafiti wao. Hasa ulaji wa mihogo kila siku.

Mihogo na watoto mapacha: Mihogo Ina Aina Ya Estrogen

mihogo na watoto mapacha

Mihogo ina phytoestrogen, aina ya estrogen inayo ongeza homoni yako ya Follicle Stimulating Hormone (FSH). Na kukufanya uwe na kiwango cha juu cha ovulation. Baadhi ya kemikali inayo kuwa kwenye ngozi za mihogo na inahusishwa na ovulation ya juu zaidi. Katika aina hii, mwili unatoa zaidi ya yai moja na mara nyingi husababisha mimba ya mapacha. Imani hii imetushtua. Kuna sehemu ambazo mihogo ndicho chakula kikuu. Inaweza kuliwa katika njia tofauti; kukaangwa, kuchemshwa, ikiwa ime siagwa, ama kukaushwa.

Mimba ya mapacha hufanyika baada ya yai lililo kua fertilized kujishikilia kwenye kuta za uterasi na kugawana kuwa viinitete viwili. Ama wakati ambapo mayai mawili yana kuwa fertilized na kujishikilia kwenye kuta za uterasi vitofauti. Katika kesi hii kuna watoto wasio fanana ama fraternal. Uwezekano wa kuwa na mapacha wanao fanana ni asilimia 0.3% katika dunia yote. Visa vya mapacha wasio fanana hubadilika duniani na ni angalau 2.3%. Na nambari hii huwa kubwa zaidi katika nchi za magharibi. Na huenda nambari hii ikaendelea kuongezeka kufuatia utumiaji mwingi wa madawa ya uzazi na In Vitro Fertilization.

Dawa za Ulezi, IVF Na Umri wa Kula Mihogo Na Watoto Mapacha

mihogo na watoto mapacha

Zote hizi huongeza nafasi zako za kupata ovulations mbili ama zaidi. Pia, mwenendo unaovuma wa wamama wa umri mkubwa umeongeza visa vya kupata watoto zaidi ya mmoja. Kadri wanawake wanavyo zidi kuzeeka, mimba yao huenda ikawa ya watoto mapacha. Wanawake wa umri zaidi huwa na homoni ya FSH iliyoko kwenye miili yao kufuatia kuwa na miaka mingi. Kuna sababu nyingi tofauti kwa nini wanandoa wanaweza penda kuwa na mapacha. Baadhi ya wanawake wanataka kubeba mimba mara moja. Kwa hivyo kuwa na mapacha kuna wapatia familia wanayo taka kwa mara moja. Baadhi ya wanawake huwa na tatizo la kutunga mimba, mimba ya mapacha huenda ikawa mara moja kwao. Wakati ambapo baadhi ya watu hupendezwa na mapacha tu.

Iwapo wewe ni mojawapo wa wanawake hawa, huenda ukataka kutafuta kitabu cha mapishi ya mihogo. Mimi sio mwanasayansi wa jeni, lakini nitasema kuwa ni vyema kujaribu iwapo ungependa mimba ya watoto zaidi ya mmoja. Kula mihogo kwenye lishe yako mara kwa mara hakuna hatari yoyote. Mbali na hayo, ni bora kuliko kujaribu vidokezo vyenye hatari kama krimu za progesterone. Na dawa ya Clomid ili kupata mapacha.

Kama ilivyo kawaida, hii sio njia iliyo dhihirika kamili ya kujaribu kupata mapacha, kwani hakuna anayejua kiasi cha mihogo unacho hitajika kula. Pia, haijulikani iwapo athari za kula mihogo zinatokea mara tu unapokula ama baada ya muda mrefu. Cha muhimu zaidi, hakuna aliye elezea jambo hili kwa kina na hakuna ushahidi wa kimatibabu ambayo yanaweza dhihirisha kuwa ulaji wa mihogo unaweza sababisha kupata watoto zaidi ya mmoja. Ni imani tu.

Wakati ambapo kula sahani iliyojaa mihogo kila siku huenda ikakaa jambo lisilo la busara, angalau halina athari hasi na hakuna hatari zozote kujaribu. Huenda ukawa na bahati.

Soma pia: Dalili Za Mwanamke Mwenye Mimba Ya Mapacha

Written by

Risper Nyakio