Ikiwa unatafuta mchumba, ama unataka kuingia katika uhusiano na mwanamke mwenye mtoto unapaswa kuwa tayari. Utafiti wa hivi punde huko Marekani umedhibitisha kuwa idadi ya wanawake wanaowalea watoto peke yao iko juu zaidi, kwa hivyo iwapo unatafuta mchumba, wanawake wenye watoto watakuwa kwenye kiwanja chako.
Wanawake wenye watoto huwa na maoni, majukumu na uraibu tofauti ya kimaisha, na huwa wachumba wema. Wanajua kutumia muda walio nao kuwa wazazi, kufanya kazi na kuwa na marafiki zao. Ikiwa una uhusiano, ungetaka kuingia kwenye uhusiano ama unaingia katika uhusiano na mwanamke mwenye mtoto, unapaswa kufahamu mambo haya.
Uhusiano na mwanamke mwenye mtoto

Fahamu kuwa ni tofauti
Unapokuwa katika uhusiano na mama aliye na watoto, ni vyema kufahamu kuwa mambo yatakuwa tofauti. Katika uhusiano na mwanamke asiye na mtoto, unaweza kupima iwapo wanahisia zako kulingana na nishati na wakati wanaokupa. Mambo ni tofauti kwa wanawake walio na watoto. Muda wao mwingi watakuwa na watoto wao. Usitarajie wakupe wakati sawa na watoto wao. Ni muhimu kwenu kuwa na mazungumzo wazi kuhusu uhusiano wenu na mwelekeo mtakao chukua.
Kubali kuwa watoto wake ndiyo kipaumbele chake
Kwa wazazi wa kipekee watoto wao huwa jukumu la kwanza. Elewa kuwa hata mnapoanza uhusiano, juhudi zake nyingi zitakuwa kwa mtoto wake. Kukubali ukweli huu kutasaidia uhusiano wenu kukua. Baadhi ya wazazi wa kipekee huenda wakawa na shaka kuwa kuingia katika uhusiano mpya kutaathiri uhusiano wao na watoto wao. Ni muhimu kwa mtu aliye na uhusiano nao kuwaelewa na kuwahakikishia kuwa hatabadilisha familia yao.

Usiwe na mbio
Mzazi wa kipekee hana uhakika kuhusu nia yako, unapokiri matakwa yako ya kuwa na uhusiano nao. Mpe muda akujue vyema kabla ya uhusiano wenu kunoga. Mnapoanza uhusiano wenu, usiwe na kasi ya kuchukua jukumu la kuwa baba ya watoto wake. Mpe muda ahisi kuwa mtoto wako atakuwa salama mikononi mwako, na pia hutakuja kisha uondoke baada ya muda mfupi.
Kuwa mwaminifu
Ikiwa unataka uhusiano utakao dumu na kuwa ndoa, kuwa mwaminifu kwa mchumba wako. Matendo yako yaandamane na maneno yao. Zungumza kwa uwazi ili apate kukuamini. Kwa njia hii, uhusiano wenu utakuwa na msingi wenye nguvu.
Soma Pia: Kuwa Na Baadhi Ya Ishara Hizi Kunadokeza Kuwa Uko Tayari Kuwa Mzazi