Kwa kweli, mapenzi haya bagui umri, unaweza penda mzee ama kijana kama mwana muziki alivyo sema. Huenda ukajipata katika kikundi cha wanaume wanao penda wanawake wenye umri zaidi. Na hakuna jambo mbaya na hilo. Kwani huenda ukapendezwa na jambo moja usilo lipata katika wanawake wa umri sawa na wako. kuna mambo muhimu unayo paswa kufahamu kabla ya kuwa na uhusiano na mwanamke mzee kukuliko.
Ni kawaida sana kwa wanaume kuwa na wachumba wenye umri mdogo kuwaliko. Na hii ndiyo sababu kwa nini kuwa na mchumba mdogo kukuliko ni jambo la kipekee. Pia ni jambo linalo wasisimua wanawake wenye umri zaidi mwanamme anapo waacha wanawake wa umri mdogo na kuwachagua. Hisia hiyo ita ongeza hamu ya mawasiliano yenu.
Wakati ambapo wanawake wenye umri zaidi wako wazi kuwa na uhusiano na wanaume wenye umri mdogo kuwaliko, haimaanishi kuwa wanataka kuwa na "vijana". Wanataka kuwa na wanaume wenye nguvu na walio na usemi na wanao fahamu jinsi ya kuwafanya wahisi kuwa wao ni wanawake, ila wenye umri mdogo kuwaliko. Wakati ambapo utapenda wanawake hawa kwa mambo fulani, hapa kuna vitu vichache unavyo stahili kufahamu.
Mambo ya kujua kabla ya kuwa na uhusiano na mwanamke mzee kukuliko

-
Hata kukubalisha kuwa na uhusiano mwingine nje
Kwa kweli, kama hauko tayari, tafadhali usiwapotezee muda. Kwa sababu ana umri zaidi yako, huenda akawa alimalizana kucheza kitambo. Kwa sasa anatafuta mtu aliye na mwelekeo maishani. Ata fanya juhudi kuhakikisha kuwa uhusiano wenu una fuzu. Kwa hivyo kama hungependa kuwa naye siku za usoni, sio jambo la busara kuwa katika uhusiano wa kimapenzi naye.
-
Uamuzi wa busara hautakuwa tatizo
Inapofika kwa kufanya uamuzi wa busara katika uhusiano wenu, hautakuwa na suala kwani atachukua usukani. Kwa sababu ana umri zaidi, ameyapitia mengi kukuliko na anayajua mengi. Pia, hata kutwika mzigo wa matatizo yake kwani ana uwezo wa kukabiliana nayo mwenyewe. Kwa hivyo hamtakuwa na matatizo ya kitoto.
-
Anajua anacho taka maishani
Umri zaidi huja na kuwa hakika unacho taka maishani. Kwa hivyo, mwanamke mzee kukuliko anapo fanya uamuzi wa kuwa na uhusiano nawe, bila shaka anaona maisha marefu nawe.
-
Maisha ya ngono yatakuwa mema
Wanaume wengi huwa na shaka kuwa, huenda waka kosa kutoshelezwa kingono wanapo kuwa katika uhusiano na mwanamke mzee kukuliko, hawata toshelezwa kingono. Usiwe na shaka kwani bado wana hamu ya kuwa na wakati mwema.
Soma Pia: Utamwambia Vipi Mchumba Wako Ajitahidi Zaidi Kitandani?