Sababu Kwa Nini Uhusiano Wako Haudumu: Jinsi Ya Kuwa Na Uhusiano Unao Dumu

Sababu Kwa Nini Uhusiano Wako Haudumu: Jinsi Ya Kuwa Na Uhusiano Unao Dumu

Sote tungependa kuwa katika uhusiano unao dumu na wenye maana. Vidokezo hivi vinakuongoza kutimiza lengo hili.

Watu wengi huingia katika uhusiano wakiwa na matarajio mengi. Sote tungependa kuwa katika uhusiano unao dumu na wenye maana. Walakini, sote tuna hitilafu zetu na huenda zika athiri uhusiano wetu. Ikiwa umegundua kuwa uhusiano wako huwa na siku 90 za kufuzu kisha una isha, huenda ukawa wewe ndo tatizo.  Tuna angazia baadhi ya tabia ambazo huenda zikamsukuma mchumba wako mbali na kukufanya usiwe na uhusiano wenye maana.

uhusiano unao dumu

Epuka Tabia Hizi Ili Kuwa Na Uhusiano Unao Dumu

Kuto Zungumza

Uhusiano unahitaji kuzungumza mara kwa mara na kwa uwazi. Ikiwa hauzungumzi kuhusu hisia zako, itakuwa vigumu kwako kuwa na uhusiano unaodumu muda mrefu. Haupaswi kuhisi kana kwamba huwezi mwambia mwenzi wako jambo lolote linalo kusumbua. Hakikisha kuwa una uhuru wa kumwelezea kinacho kusumbua moyoni, unacho taka kitendeke kwenye uhusiano wenu na hata jinsi siku yako ilivyo kuwa. Bila mazungumzo ya wazi, uhusiano wenu hautafanikiwa. Pia mnapo zungumza, mna elewana zaidi.

Kuwa Na Mahitaji Mengi Ya Kihisia

Ni muhimu sana kuhisi kuwa mchumba wako anakutaka, anakupenda na anakujali. Lakini unapokuwa kwa uhusiano, wewe na mchumba wako hamhitaji kuwa pamoja kila wakati. Ikiwa wewe ni mtu ambaye anapenda kuwa na mchumba wake siku nzima, huenda mchumba wako akahisi kuwa hana mwanya wa kupumua. Ikiwa ungependa kuwa na uhusiano unao dumu, ni vyema kufahamu kuwa nyote mna maisha yenu kando. Na wakati huo ni muhimu sana ili uweze kufanya mambo yako na mchumba wako aweze kuishi maisha yake pia.

Sababu Kwa Nini Uhusiano Wako Haudumu: Jinsi Ya Kuwa Na Uhusiano Unao Dumu

Kukosa Wakati Wa Mchumba Wako

Siku hizi, wanawake wanajivunia kuishi maisha huru, bila kumtegemea mwanamme yeyote kutimiza mahitaji yao ya kifedha. Ambalo ni jambo linalo paswa kuhimizwa. Walakini, uhusiano hufuzu katika kuwa na wakati tosha na mchumba wako. Huenda ukakosa wakati wa kuwa na mchumba wako, kujuana, kuzungumza na hata kufanya mambo yanayo wafurahisha pamoja. Na sio wanawake tu ambao hukosa wakati wa wachumba wao, huenda pia mwanamme akawa ana tumia muda mwingi na marafiki zake na kupuuza mahitaji ya mchumba wake. Uhusiano unahitaji juhudi nyingi na wakati na ikiwa unakosa mojawapo kati ya hizi, itakuwa vigumu kuwa na uhusiano unao dumu.

Kuto Jiamini

Huwa vigumu sana kuwa na uhusiano wenye mafanikio na mtu asiwe kuwa na ujasiri na ana matatizo ya kujiamini maishani. Kuto jiamini kwako kunaweza sababisha matatizo mengi kwenye uhusiano wako, kukosa imani, chuki, kuona wivu na kuhitaji maneno ya imani kutoka kwa mchumba wako. Kama ulivyo sikia mara nyingi, kabla ya mtu mwingine kukupenda, unahitaji kujipenda kwanza.

Kuwa Na Matarajio Yasiyo Wezekana

Siku hizi, watu wanaamini kuwa kuna uwezekano wa kupatana na mtu, kufunga ndoa na kuishi maisha mema yasiyo na taswira kwa muda mfupi sawa na kufunga jicho. Lakini kwa wengi wetu, hii ni ndoto tu, sote tuna fahamu kuwa uhusiano sio rahisi hivyo. Kuingia katika uhusiano na matarajio yasiyo wezekana kuta ambulia patupu.

Kuwa Na Matatizo Mengi Ya Kitoto

Uhusiano wenye mafanikio huwa kati ya watu wawili walio na uzima unao hitajika katika mapenzi. Katika siku za kwanza mapenzi yanapo kuwa yamenoga, huenda mchumba wako akapuuza tabia zako za kitoto. Lakini huenda mapenzi yakaanza kufifia kadri muda unapo pita. Kwa hivyo hakikisha kuwa ume suluhisha matatizo yoyote uliyo nayo kabla ya kuingia katika uhusiano. Kwa njia hii, utakuwa na uhusiano unao dumu muda zaidi.

Chanzo: Madame Noir

Soma Pia: Malengo 10 Ya Uhusiano Yatakayo Fanya Mapenzi Yenu Yakue

Written by

Risper Nyakio