Njia 3 Ambavyo Uhusiano Unaathiriwa Baada Ya Mchumba Kutoka Nje

Njia 3 Ambavyo Uhusiano Unaathiriwa Baada Ya Mchumba Kutoka Nje

Unapo salitiwa na mtu uliye mwamini na kumpenda kwa dhati. Ni asili kuwa na mawazo ya kulipiza kisasi kwa kupata mchumba wa kando pia.

Je, kurudiana baada ya mchumba kutoka nje ya ndoa kuna shauriwa? Kuna uwezekano wa kusahau kilicho fanyika? Unafahamu jinsi uhusiano unavyo badilika baada ya kutoka nje?

Kwa baadhi ya wanandoa, kutoka nje ya ndoa sio kitendo ambacho hakiwezi sameheka. Ni uchungu kujua kuwa mwenzi wako alidanganya na kuwa na mchumba mwingine. Lakini bado wana fanya uamuzi wa kurudiana na kusahau kilicho fanyika. Mojawapo ya sababu za kufanya hivi ni kuwa wana kitu moja sawa: wana amini kuwa mapenzi yao yana dhamani ya kupiganiwa.

Hata kama kuna uwezekano wa kuwa na furaha tena, uhusiano ulio vunjwa hauwezi kuwa ulivyo kuwa hapo awali. Sawa na kikombe cha glasi baada ya kuangushwa. Kamwe hakiwezi rejelea kilivyo kuwa hapo awali.

Unapo jipata katika hali sawa na hii, usiwe na shaka. Fahamu kuwa hakuna aliye na haki ya kuhakimu uamuzi wako. Ni wewe tu na mchumba wako ambaye mnafahamu jinsi mnaweza jiponya. Lakini mnapaswa kuwa tayari. Haya ndiyo mabadiliko ya kutarajia katika uhusiano baada ya kutoka nje.

Hivi ndivyo uhusiano unavyo badilika baada ya kutoka nje

uhusiano unavyo badilika baada ya kutoka nje

  1. Una tatizika kumwamini mchumba wako

Kiasili, imani ni kitu ambacho utahitajika kutia juhudi ili kuregesha kwa uhusiano wenu baada ya mchumba wako kutoka nje. Uhusiano nje ya ndoa una husu kumdanganya mchumba wako. Kwa hivyo, aliye danganywa ata tatizika kumwamini mchumba wake tena baada ya kitendo hicho.

Saikolojia Leo ina shauri wachumba kujaribu kuwa na mtindo wa kuzungumza ukweli wakati wote. Ili kujaribu kuregesha imani tena katika uhusiano wao.

2. Kujiamini kwako kuna kupunguka ama kuongezeka

uhusiano unavyo badilika baada ya kutoka nje

Mtu aliye vunjwa moyo na mchumba aliye toka nje ya ndoa huenda akaanza kushuku dhamani yake. Je, sipendezi vya kutosha, simpendi ninavyo paswa ama sim sisimui tena? Huenda pia wakaanza kujilaumu, kwa hofu kuwa kitendo walicho fanya kilisababisha yale.

Licha ya kutatizika kuwa na ujasiri na ushupavu, wachumba walio danganywa huenda wakaibuka kuwa na nguvu zaidi. Chukua muda ujikumbushe dhamana yako.

3. Huenda ukajaribiwa kulipiza kisasi

Hii ni hisia asili. Unapo salitiwa na mtu uliye mwamini na kumpenda kwa dhati. Ni asili kuwa na mawazo ya kulipiza kisasi kwa kupata mchumba wa kando pia. Lakini mawazo haya hayapaswi kuzingatiwa kwa muda mrefu. Kufanya jambo sawa kutafanya hali idorore zaidi, na iwe vigumu kwenu kurejesha uhusiano wenu.

Pia, ni vyema kwa wanandoa kuepuka kukumbushana kuhusu tendo la kutoka nje ya ndoa. Hasa mnapo kuwa mna bishana. Epuka kurejelea wakati ambapo mchumba wako alitoka nje ya ndoa ili kuwafanya wahisi vibaya. Hakuna athari chanya kwa uhusiano wenu.

Soma pia:Sababu 5 Kwa Nini Kutoka Nje Katika Ndoa Kumekuwa Kawaida Sana

Written by

Risper Nyakio