Kinacho Fanya Uhusiano Kufuzu

Kinacho Fanya Uhusiano Kufuzu

Ili wachumba waaminiane, kunapaswa kuwa na uwazi na kufanya matendo ya kuaminika. Usiwe na siri na mchumba wako.

Ikiwa uko katika uhusiano wa kimapenzi, nafasi kubwa ni kuwa ungetaka kuwa na uhusiano wenye afya. Lakini uhusiano wa kiafya ni upi hasa? Ina lingana na maelezo haya hutofautiana kati ya watu kwani watu wanataka vitu tofauti katika mahusiano yao. Mahitaji pia hutofautiana na umri na wakati. Kwa hivyo vitu unavyo tafuta katika uhusiano ukiwa na miaka 20 vitabadilika unapo fikisha miaka 30.

Ishara maarufu kati ya uhusiano wenye afya

uhusiano wenye afya

Wachumba katika uhusiano wenye afya huongea kuhusu mambo yanayo tendeka maishani mwao: kupasi, kufeli na kila kitu. Unapaswa kuwa na starehe kuongea kuhusu matatizo yoyote yanayo ibuka katika maisha ya kila siku, kama vile kazi, marafiki ama matatizo nyeti kama afya ya kiakili na shaka za kifedha.

Hata kama wana maoni tofauti, wata sikiza bila kukuhakimu na kukuambia wanavyo fikiria. Mazungumzo huwa njia mbili. Ni muhimu uhisi kuwa wana kuambia wanacho fikiria.

  • Imani

Ili wachumba waaminiane, kunapaswa kuwa na uwazi na kufanya matendo ya kuaminika. Usiwe na siri na mchumba wako. Na mnapo kuwa mbali, usiwe na shaka kuwa ata tafuta mchumba mwingine. Kuwaamini pia kuna husisha kuhisi uko salama na una starehe na unajua hawata kuumiza kihisia ama kifizikia. Wana taka ufuzu maishani na pia wana kuheshimu na kukuhimiza ufanye mambo yanayo faa maishani.

  • Una maisha yako

uhusiano wenye afya

Uhusiano wenye afya unawa kubalisha wachumba kuwa na maisha yao kando na uhusiano. Hata kama mna tegemeana, kila mtu ana uutu wake. Kwa njia hii, uhusiano wenu ume sawasishwa. Unajua una kibali chao na mapenzi yao, lakini kujiamini kwako hakuwategemei. Bado una marafiki wako kando na uhusiano wenu. Na unafuata ndoto zako.

  • Wakati kando

Watu wengi walio katika uhusiano hupenda kupatia kipau mbele wakati wanapo kuwa pamoja. Wakati huu una tofautiana kulingana na mahitaji ya kibinafsi, kazi na mnavyo ishi. Pia ni muhimu kufahamu nafasi na wakati binafsi wa mchumba mwingine wa kuwa peke yake na kufanya vitu vyake. Unaweza chukua muda huu kufanya mambo unayo penda ama kuwatembelea marafiki na jamaa zako.

Soma Pia: Jinsi Kufikiria Sana Kutakavyo Haribu Uhusiano Wako

Written by

Risper Nyakio