Ujauzito Baada Ya D&C (Dilation na Curettage): Kuna Uwezekano?

Ujauzito Baada Ya D&C (Dilation na Curettage): Kuna Uwezekano?

Ni kweli kuwa ujauzito baada ya utaratibu wa d&c unawezekana. Ila utakuwa na matatizo machache.

Baada ya utaratibu wa upasuaji wa dilation na curettage (d&c) mwezi wa Oktoba, Katie Ong, aliambiwa kuwa ujauzito baada ya d&c, iwapo inawezekana, huenda ikafutwa na matatizo chungu nzima. Alipatiwa orodha ya vitu vya kujitahadhari dhidi yake na jinsi ya kufanya mapenzi.

Miezi sita baadaye, mwanamke huyu wa miaka 30 alikuwa na furaha tele alipo tangaza kuwa alikuwa anatarajia mapacha. Ong, ambaye wake kwa wakati wote alikuwa anashuhudia kipindi cha hedhi kenye damu nyingi na kushauriwa na daktari wake kupata utaratibu wa d&c. Hii ni baada ya kumweleza matarajio yake ya kuwa mama.

Kama inavyo onekana, utaratibu huu ulikuwa kitu hasa ambacho mwili wake ulihitaji.

Je, d&c ni nini na inafanywa kwa nini?

pregnancy after d and c

Whether it is to try for pregnancy after d&c or to get rid of heavy bleeding, the procedure’s two main functions are to diagnose and treat. | Image courtesy; Mayo Clinic

Utaratibu mdogo unao onekana wa upasuaji, dilation an curettage ni utoaji wa tishu kutoka sehemu ya ndani ya uterasi. Kizazi (sehemu ya chini iliyo nyembamba ya uterasi yako) inapanuliwa kwanza na kifaa spesheli kinacho itwa curette kutumika kutoa sehemu ya ndani ya uterus (uterus lining).

Madaktari kwa ujumla wanafanya upasuaji huu ili kutibu hali hasa za uterasi, ikiwemo kipindi cha hedhi chenye damu nyingi kama vile Ong, ama kutoa kipande kilicho baki baada ya kuharibika kwa mimba ama utoaji wa mimba.

Walakini, huenda kukawa na sababu zingine ambazo zitamfanya daktari wako kukushauri kupata d&c.

1) Kugundua tatizo la kimatibabu

Baadhi ya wanawake mara kwa mara wanashauriwa utaratibu wa dilation na curettage hasa unaoitwa sampuli ya endometrial. Hii inasaidia kugundua aina tatu za hali za kimatibabu, zikiwemo:

 • Kutoa damu kwa uterasi kusiko kwa kawaida
 • Kutoa damu baada ya kutimiza wakati wa kuto jifungua
 • Seli za endometrial zisizo za kawaida kuangalia iwapo kuna saratani ya kizazi

Ili kufanya kipimo hiki, daktari wako atachukua kipande kidogo cha tishu kutoka kwa sehemu ya ukuta wa uterasi (endometrium) na vipimo vya maabara vitadhibitisha iwapo una kata ya mambo yafuatayo:

 • Endometrial hyperplasia ( hali kabla ya saratani ambapo ukuta wa uterasi unakuwa mnene na kusababisha kutokwa na damu kusiko kwa kawaida)
 • Uterine cancer ( aina ya saratani inayo anza kwa ukuta wa uterasi na huenda ukaongeza nafasi za homini kutokuwa sawa mwilini na unene zaidi) 
 • Uterine polyps ( huu ni ukuaji zaidi wa seli zisizo sababisha saratani kwenye ukuta wa uterasi na kisha kusababisha kipindi cha hedhi chenye damu nyingi zaidi na kutokwa na damu baada ya kufikisha umri wa kutojifungua)

2) Kutibu hali fulani

pregnancy after d&c

Daktari wako anapofanya utaratibu wa d&c, atatoa sehemu ya tishu ya uterasi ili kutibu baadhi ya hali zifuatazo:

 • Toa tishu zinazo baki ndani ya uterasi baada ya kupoteza mimba ama kutoa mimba. Huku kuna saidia kuepuka maambukizo na hata kutokwa na damu nyingi.
 • Kutolewa kwa ujauzito wa molar ambapo uvimbe unatokea ndani ya placenta, kufuatia ukuaji usio wa kawaida wa trophoblasts.
 • Utaratibu wa d&c unafanyika kutoa placenta inayo baki kwenye uterasi baada ya kujifungua.
 • Huenda pia ukafanyika ili kutoa polyps za uterasi ambazo huwa hazisababishi saratani.

Daktari kwa ujumla atafanya d&c kando na utaratibu unaoitwa hysteroscopy. Katika utaratibu huu, kifaa chembamba kilicho na mwangaza kinaingizwa kwenye uke wako kwa kupitia kizazi chako hadi kinapofika kwenye uterasi yako.   

Huku kunamkubalisha mtaalum kuangalia ndani ya uterasi yako. Wakati wa mchakato huu, anaweza angalia ukuta na kutoa polyps ama fibroids inavyo hitajika. Mchakato huu unahakikisha kuwa ujauzito baada ya d&c unawezekana na damu nyingi inathibitiwa.

Sasa iwapo una mawazo ya kupata d&c kuna vitu vichache unavyopaswa kujua.

Nini Kinacho tendeka wakati wa D&C

pregnancy after d&c

Post the anaesthesia, you will be made to lie down on your back, as your legs rest on stirrups. | Image courtesy; Shutterstock

Daktari wako atakujuza kuwa ujauzito baada ya d&c unawezekana, ila na tahadhari ambazo zinahitajika. Walakini, kuna vitu vichache unavyopaswa kujua kuhusu mchakato huu.

Kabla ya utaratibu huu, utapata dawa ya kukufanya ulale kuzingatia hali yako ya kimatibabu na historia. Huenda dawa hizi zikawa za ujumla ama za kienyeji. Ya hapo awali inaulaza mwili wote iwapo ya hapo mwisho ni ya sehemu hasa. 

Wakati wa utaratibu wa d&c utayapitia yafuatayo:

 • Kwanza utalazimika kulala kwa mgongo wako, na uilaze miguu yako juu ya stirrups.
 • Daktari wako kisha ataingiza speculum, ambacho ni kifaa chembamba kinacho ingia kwenye uke wako kwa kupitia kizazi chako.
 • Daktari wako kwa upole ataingiza rods nene ili kuweza kukipanua kizazi chako vyema.
 • Baada ya hapo daktari wako ataingiza kifaa kinacho fanana kijiko, ama kifaa cha kunyonya kutoa sampuli ya tishu za uterasi.

Kwa sababu ya kugandishwa, hautahisi kutokuwa na starehe. Ila, hautakuwa na budi ila kukaa kwenye kliniki ama hospitali kwa masaa machache baada ya utaratibu huu ili wauguzi waangalie unavyo endelea. Madaktari watafanya vipimo kudhibitisha iwapo una matatizo yoyote ya kutokwa na damu ama mengineyo.

Iwapo kugandishwa kule kulikuwa kwa kijumla, huenda ukahisi kichefu chefu ama hata kutapika. Huenda hata ukawa na koo linalo uma ama iwapo koo ya pumzi ilitumika kukusaidia kupumua. Na ikiwa ulipata dawa za kugandishwa za kienyeji, huenda bado ukahisi kana kwamba unataka kulala masaa machache baada ya utaratibu huu.

Daktari wako huenda akakujuza kuwa ujauzito punde tu baada ya d&c haushauriwi. Na kuwa muda wa mapumziko wa miezi 3-4 unahitajika kwako ili uweze kupona kabla ya kujaribu tena.

Kuwa makini iwapo utashuhudia athari mbili kuu za baada ya utaratibu wa d&c.

 • Huenda ukashuhudia uchungu mwepesi wa hedhi
 • Huenda kukawa na damu ama kutokwa na damu kiasi

Iwapo unashuhudia kuto starehe kokote, daktari wako huenda akashauri dawa za kutuliza uchungu. Walakini, la muhimu zaidi ni kujua kuwa unapaswa kuepuka kuingiza kitu chochote kwenye uke wako hadi kizazi chako kitakapo pona.

Huku kuna epusha maambukizo ya bakteria kwenye uko. Unapaswa kuhakikisha kuwa unamwuliza daktari wako wakati ambapo unaweza fanya mapenzi tena.

Jambo lingine la kutilia maanani hapa ni wakati wa kipindi hiki. Kwani katika muda huu bado unapona, huenda ukakosa kushuhudia kipindi chako cha hedhi wakati sawa mwezi ujao. Iwapo ulishuhudia d&c kufuatia upoteza mimba, ni vyema kumwuliza daktari wako iwapo ujauzito punde tu baada ya d&c ni salama.

Kwa kuyasema hayo, kama kesi ilivyo na utaratibu wote wa upasuaji, wakati ambapo d&c ni salama, huenda matatizo yakawa nadra ila kuna uwezekano.

Baadhi Ya Hatari Baada Ya Utaratibu Wa D&C 

Matatizo haya sio kawaida sana, ila nafasi za matatizo haya kutendeka haziwezi tupiliwa mbali. Haya ni kama vile:

 • Mashimo kwenye uterasi. Matatizo haya huenda yakafanyika pale ambapo kifaa cha upasuaji kina gusa na kutengeneza shimo kwenye uterasi yako. Huenda ikawa kawaida zaidi kwa wanawake ambao wamejifungua tu ama waliofikisha miaka ya kuto jifungua. Iwapo mashimo haya kwa mara nyingi huwa machache, iwapo kuna kiungo ambacho kime jeruhiwa, hali hii itarekebishwa tu kwa upasuaji.
 • Kuharibika kwa kizazi. Huenda kukawa na nafasi kuwa kizazi chako kilijeruhiwa katika kipindi chako cha d&c. Iwapo jambo hili linatendeka, huenda daktari wako akaongeza shinikizo ili kufanya damu iwache kutoka. Mbali na hivyo, daktari pia anaweza kupatia sutures.
 • Asherman’s syndrome. Hii ni mojawapo ya matatizo yaliyo kawaida zaidi baada ya d&c, hasa kwa wale waliopitia utaratibu huu hapo awali baada ya kupoteza mimba. Kwa urahisi, ni kuundwa kwa tishu ya alama ndani ya uterasi yako. Huenda jambo hili likasababisha kutokwa na damu kwenye uchungu ama vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida, na hata kupoteza kwa ujauzito.
 • Maambukizo. Maambukizo ya uterasi ama kizazi baada ya d&c ni nadra, ila yanawezekana. Ni sababu ambayo madaktari wengi wana fanya uamuzi wa kuwaweka wagonjwa hospitalini mwao waki waangalia wanavyo endelea kwa muda kabla ya kuwa ruhusu kuenda manyumbani mwao.

Baada ya d&c iwapo una dalili za kutahadharisha , ni vyema kumjuza daktari wako bila kusita.

 • Joto jingi
 • Kutokwa na damu nyingi ambapo lazima ukae ukibadili kila baada ya lisaa limoja
 • Uchungu wa hedhi
 • Uchafu wa uke unaonuka

Kumbuka kuwa matatizo huwa nadra mara nyingi baada ya utaratibu huu na pia ujauzito baada ya d&c unawezekana. Walakini, njia bora zaidi ya kuhakikisha kuwa una uwezo wa kuanza familia ni kuhakikisha kuwa unamjulisha daktari wako kuhusu historia yako ya kimatibabu na hali unavyo endelea.

Also read: Incompetent Cervix And Miscarriage

Vyanzo: Healthline, Mayo Clinic, WebMD, Medline Plus

Republished with permission from theAsianparent

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Deepshikha Punj kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio