Ujauzito Na Mazoezi: Ni Salama Kufanya Mazoezi Katika Kipindi Hiki?

Ujauzito Na Mazoezi: Ni Salama Kufanya Mazoezi Katika Kipindi Hiki?

Makala haya ya ujauzito na mazoezi yana angazia umuhimu wa kufanya mazoezi unapokuwa na mimba na jinsi mtoto anafaidika kutokana na mazoezi.

Manufaa ya mazoezi hayawezi orodheshwa yote kwani ni mengi na mazoezi ni muhimu sana kwa afya ya binadamu. Kuna watu ambao huwa makini sana kuhusisha mazoezi kwenye maisha yao ya kila siku, huku wengine wakipuuza umuhimu wa mazoezi. Na kamwe hawapendi hata kutembea kwa masafa marefu. Kila wanapo kwenda mahali, wana amua kutumia magari. Ujauzito na mazoezi yana endana.

Mazoezi rahisi yanayo fahamika sana ni kama vile kutembea, michezo tofauti kama vile kadanda, mpira wa vikapu, volliboli, dondi na riadha. Tumeshuhudia ongezeko la vituo vya mazoezi nchini ambavyo hapo awali vilikuwa maarufu nchi za ugeni. Kwa hivyo wasio weza kufanya mazoezi peke yao wanaweza pata wataalum wa kuwasaidia. Mazoezi yana saidia afya yako ya kifizikia, hisia na akili. Ni muhimu pia kwa wanawake walio na mimba.

Ujauzito Na Mazoezi: Mazoezi salama katika mimba

mazoezi na ujauzito

Mama anapokuwa mjamzito, anashauriwa kuepuka mazoezi yanayo shinikiza sehemu ya tumbo. Pia, ni vyema katika kipindi hiki ahakikishe kuwa hafanyi mazoezi magumu ama kwa muda mrefu zaidi. Ikiwa hapo awali ulikuwa umezoea kufanya mazoezi magumu, punguza na ufanye mepesi.

Kuna mazoezi rahisi ambayo mama ambaye hakuwa anafanya mazoezi hapo awali anaweza fanya. Kama vile, kutembea kwa dakika kati ya 30-40. Kuogelea ama baadhi ya michezo ya mipira.

Mazoezi kama vile yoga yanamsaidia mama kupunguza uchungu kwenye mgongo

na pia anaweza kujifungua kwa urahisi.

Hitimisho

Ujauzito Na Mazoezi: Ni Salama Kufanya Mazoezi Katika Kipindi Hiki?

Kwa mama mjamzito, hana kisingizio chochote cha kutofanya mazoezi. Kwani umuhimu wa mazoezi katika ujauzito umeegemezwa na sayansi. Lakini kumbuka kuwa unapaswa kufanya mazoezi huku ukishauriwa na mtaalum wa mazoezi ya mama mjamzito. Kwani sio mazoezi yote ambayo ni salama kwa mama na mtoto katika kipindi hiki. Epuka michezo kama vile dondi, rugby, michezo ya hoki na soka katika kipindi hiki. Unapo fanya mazoezi kisha uanze kuhisi uchungu ama kizungu zungu, koma kwa kasi.

Kumbuka kuwa, hata baada ya kujifungua, utachukua muda wa angalau wiki mbili hadi nne kabla ya kurejelea kufanya mazoezi tena. Daktari wako atakushauri wakati bora kuanza mazoezi tena.

Chanzo: WebMD

Soma pia:Mambo 5 Muhimu Unayo Paswa Kufanya Kabla Ya Kufanya Mazoezi

Written by

Risper Nyakio