Ukosefu wa mafuta taa na bidhaa za mafuta taa unaendelea kushuhudiwa nchini Kenya. Kufuatia ruzuku ya serikali kabla ya hakiki ya mwezi ya bei za fueli.
Stesheni za mafuta nje ya mji mkuu wa Nairobi zilianza kushuhudia ukosefu wikendi iliyopita, huku ukosefu huu ukishuhudiwa mjini mkuu kutoka Jumatatu.

Wauzaji mafuta wanashirikisha ukosefu huu na kukosa uhakika kwa ruzuku ya mafuta ambayo serikali ilitangaza Aprili ili kuimarisha bei za mafuta. Kuchelewa kwa kulipa ruzuku na serikali kumesukuma bei ya mafuta na wauzaji wa jumla wanaowauzia wauzaji wa rejareja. Wauzaji wa rejareja wanadhibiti hadi asilimia 40 ya soko ya mafuta nchini. Wauzaji wa rejareja walibaki na tashwishi kuhusu bei hizi za mafuta kwa hofu kuwa watauza mafuta kwa bei ya chini kuliko walivyonunua na kupata hasara. Jambo hasi katika kila biashara.
Wauzaji wa jumla pia wana shaka kuhusu kuongeza kiwango cha mafuta kwani hakuna uhakika iwapo serikali italipa pesa inazowadai wauzaji mafuta nchini. Katika mwezi uliopita wa Machi, serikali haikulipa ruzuku kama ilivyokusudiwa na kufanya bei ya petroli na dizeli kufika bei ya juu zaidi kutoka mwezi wa Oktoba mwaka uliopita.
Wauzaji mafuta wana shaka ya kuuza bidhaa zote walizo nazo kufuatia ruzuku ya serikali. Hofu kuwa huenda serikali ikadumisha bei za hapo awali ilhali wauzaji walinunua mafuta kwa bei ya juu na kuleta hasara kubwa. Serikali inadaiwa na bilioni 13 na kampuni za mafuta nchini. Katika mwanzo wa mwezi wa Aprili, serikali iliachilia bilioni 8.2 ili kutatua suala la mafuta nchini.

Wafanyabiashara wanasemekana kuongeza kiwango cha mafuta wanachouza kwa nchi zinazokaribia kama Rwanda na Uganda hadi asilimia 60 ikilinganishwa na asilimia 40 hapo awali.
Katika wiki iliyopita, stesheni nyingi za mafuta zilikuwa zimefunga kufuatia ukosefu wa mafuta. Huku stesheni zilizokuwa na mafuta zikiuza kwa bei ya juu ya shilingi 200 kwa lita moja. Baada ya hakiki na serikali, bei ya dizeli na petroli mjini mkuu wa Nairobi imefikia shillingi 115.60 na 134.72.
Bei iliyoongezeka ya mafuta kufuatia ukosefu wa mafuta nchini Kenya imesababisha gharama ya juu ya maisha nchini Kenya. Bei ya usafiri imeongezeka na bei za kimsingi kuwa na bei ghali.
Soma Pia: Will Smith Aomba Msamaha Baada Ya Kumzaba Chris Rock Kofi Kwenye Tuzo Za Oscars