Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 4: Ukuaji na Hatua Muhimu

Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 4: Ukuaji na Hatua Muhimu

Mzazi, kuna mambo mengi sana ya kutarajia katika mwezi huu wa mtoto wako wa miaka 6 na miezi 4

Mtoto wako amefikisha miaka 6 miezi 4! Kila siku inahisi kana kwamba ni siku mpya mnapo endelea kukua pamoja na mtoto wako. Nyinyi wote mnasoma mengi mnapo safiri safari hii ya uzazi kwa pamoja, na pia njiani, utagundua kuwa mtoto wako anakua.

Kwa sasa kwani mtoto wako wa miaka 6 miezi 4 anaanza kujua zaidi kuhusu dunia inayo mzingira. Huenda akawa na shaka ama woga, wa majini ama vyumba vyenye giza ama kuto kubalika ama kuadhibiwa.

Bila shaka wazazi, haya yote ni baadhi ya ukuaji wa mtoto wako mwezi huu. Katika makala haya, tuna angazia sehemu 6 za mtoto wako wa miaka 6 miezi 4 ya ukuaji wote wa mtoto wako. Wazazi, tafadhali kumbukeni kuwa hiki si kifaa cha kupima ukuaji wa mwanao ila ni mwongozo tu. Usi kawie kumwona mtoto wako akushauri iwapo una shaka zozote kuhusu ukuaji wa mtoto wako.

Wacha tuangazie kwa umakini kuhusu ukuaji na hatua muhimu za mtoto wako wa miaka 6 miezi 4 ambazo huenda akawa amefikisha.

Ukuaji na Hatua Muhimu kwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 4: Mtoto wako anakua ipasavyo?

6 Years 4 Months Old Development and Milestones

Ukuaji wa Kifizikia

Katika umri wa miaka 6 miezi 4, mtoto wako anataka kufanya kadri ya mambo yote peke yake na uhuru huu wa kujifanyia mambo kipekee huenda ukakupa wakati mgumu. Mbali na hayo ni kumbusho kwako kuwa mtoto wako anakua kwa kasi! Usiwe na shaka kwani kujitegemea huku ni ishara kuwa mtoto wako anakua ipasavyo.

Sehemu ya hili ni kuwa uwezo wa mwendo wa mtoto wako umekua kwa sana na kwa kasi. Huku kumkubalisha kufanya kazi zingine peke yake. Katika umri wa miaka 6 miezi 4, mtoto wako ana uwezo wa kujivalisha nguo, kushika mpira kwa ustadi na kufunga kamba zake za viatu.

Wazazi, ingekuwa vyema zaidi kujua kuwa mtoto wako huenda akaanza kuteta kuhusu uchungu wa kifizikia kama vile kuumwa na tumbo, miguu na mengineyo. Kwani katika hatua hii anajua mengi kuhusu mwili wake.

Katika hatua hii, kimo cha urefu na uzito* wa mtoto wako unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 117.8 cm (46.4 inchi)
  – Uzito: 21.6 kg (47.5 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 117.3 cm (46.2 inchi)
  – Uzito: 21.2 kg (46.6 lb)

Tuna angazia ukuaji wa kifizikia wa mtoto wako wa miaka 6 miezi 4:

 • Kufunga nyororo na vifungo kwa urahisi.
 • Kuchana nywele zake.
 • Kuruka na kushika mpira mkubwa kwa urahisi.
 • Kuchora michoro ya kweli (kwa mfano kuchora mtu aliye na kichwa, macho, mdomo, mapua na mwili wenye mikono na miguu).
 • Ana dhihirisha usawa na kutangamana zaidi.
 • Kukula vyakula peke yake.
 • Kuchora na kuandika kwa ustadi zaidi.
Vidokezo vya ulezi:
 • Hakikisha kuwa mtoto wako anapata angalau lisaa limoja la michezo ya kifizikia kila siku.
 • Mwanzishie mtoto wako michezo ya kifizikia mapema. Mhimize awe hai kucheza; kuwa na maisha iliyo hai ili mtoto wako aweze kuyaiga.
 • Anza darasa za kuogelea na kumfunza mtoto wako kuhusu usalama wa moto.
 • Jua hamu za mtoto wako katika michezo yoyote ile kwa kujihusisha na michezo tofauti, kisha um unge mkono.
Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo unafikiria kuwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 4 anabaki nyuma katika jambo lolote ukuaji wake wa kifizikia, ni vyema zaidi kuongea na daktari. Kuwa makini kuyaona mambo haya yafuatayo katika mtoto wako:

 • Kuendelea kupoteza uwezo wake ambao hapo awali alikuwa nao.
 • Kushindwa kufanya kazi za kimsingi kama vile kuvalia sare yake ya shule.
 • Kukojoa kitandani: Iwapo mtoto wako hakuwa na tatizo hili hapo awali kisha aanze. Kibofu cha mkojo kudhibitiwa na umri wake.
 • Kutatizika kulala usiku ama kupata usingizi.

your child's development

Ukuaji wa Kiakili

Hamu ya mtoto wako ya kujua kuhusu dunia inayomzingira haikomi. Jambo hili ni sawa kwani kwa kupitia kila swali lililo ulizwa na kujibiwa, mtoto wako anasoma zaidi. Uwezo wake wa kuwa makini kwa jambo umeimarika, na kumruhusu mtoto wako kuwa makini zaidi kwa kazi anazo pewa nyumbani na shuleni.

Pia kuna saidia kuwa mtoto wako ana uwezo ulio ongezeka wa kuelewa maoni ya watu wengine ambayo huenda yakakosa kuwa sawa na yake. Huku kunamsaidia mtoto wako kuwa na urafiki zaidi na watu wengine na anasoma jinsi ya kuelewa kuingiliana na watu wengine na kutangamana nao.

Mtoto wako anaelewa vyema kati ya mema na mabaya.

Kuwa mwangalifu kwa hatua zifuatazo katika mtoto wako:

 • Ongezeko la kujua njema na mbaya.
 • Kuonyesha ukuaji wa kasi wa uwezo wa kiakili.
 • Anajua jinsi tofauti za kueleza matukio yake na kuongea kuhusu hisia na fikira zake.
 • Kuwa makini kwa watu wengine zaidi ya alivyo makini kwake.
 • Kukua urafiki wa karibu.
 • Uwezo wa kuwa na fikira ngumu.
 • Hamu iliyo ongezeka ya kujua mengi zaidi kuhusu dunia.
Vidokezo vya ulezi:
 • Huenda ukajibu maswali ya mtoto wako kwa kutumia maswali mengine iili kumhimiza kufikiria.
 • Mpeleke mtoto wako mahali pa kupendeza kuhimiza uwezo wake wa kuuliza maswali na kusoma. Kama vile kwa mbuga ama maktaba. Kutembea kwenye uga kuna mpatia nafasi ya kusoma kuhusu mazingara yake.
 • Changamoto mpya huenda zikawa za kuogofya kwa mtoto wako, hasa kwa sababu ya uwoga wa kuanguka. Hapa pata saidia sana unapo mpatia msaada wako. Mkumbushe kuwa wakati wote utakuwa na yeye haijalishi kitakacho tendeka.
Wakati wa kumwona daktari? Iwapo mtoto wako:
 • Anaonyesha tabia za ukatili mwingi, hasa kugonga watu, kurusha mateke ama kutupa ngumi kwa watoto wengine.
 • Anaoneka kujitenga na watu, wasiwasi ama tabia za kuhuzunika.
 • Matatizo ya kuongea ama kutangamana na watoto wengine wanapo cheza.
 • Halitambui jina lake anapoitwa.
 • Kuwa na wasiwasi mwingine anapo tenganishwa nawe.
 • Kutatizika kufuata maagizo ya sehemu mbili, "Weka mfuko wako mbali, kisha ulete sare yajei ya kadanda."

how is your child relating with the world around her

Ukuaji wa Muingiliano na Hisia

Katika umri wa miaka 6 miezi 4, mtoto wako anakuwa makini zaidi kwa urafiki na huenda wakati mwingine ikawa vigumu kwake kwani anasoma jinsi ya kudhabiti hisia ngumu kama vile wivu na kufadhaika.

Kwa upande chanya, huenda ukagundua kuwa ameanza kudhihirisha viwango vikubwa vya kustahimili. Mbali na hayo, mtoto wako huenda akataka kupata kibali chako na ili ufurahikie anayo timiza.

Hata kama anapenda kujifanyia vitu kwa kipekee, upendo na kibali chako bado ni muhimu sana kwake.

Kwa ujumla, mtoto wako mdogo atafikisha hatua muhimu zifuatazo katika umri huu:

 • Kuwa makini zaidi na kukubalika na wanarika wake. Anasoma jinsi ya kujihusisha na kugawa.
 • Ana makini zaidi kwa marafiki na kufanya kazi kama kikundi.
 • Anataka kupendwa na kukubailika na marafiki wake.
 • Anakuwa mwema zaidi katika kueleza matukio yaliyo tendeka: anacho hisi na kufikiria, kujihusisha na wanarika wake kunaongezeka.
 • Kuanza kufikiria kuhusu siku za hapo usoni.
 • Anaelewa nafasi yake katika dunia hii.
Vidokezo vya ulezi:
 • Punguza maagizo, mkubalishe mtoto wako kuwa na uwezo wa kufanya uamuzi wake.
 • Usiwe na aibu kuongea kuhusu mada ngumu na mtoto wako kama vile kunyanyaswa, na kwa kutumia lugha inayofaa kwa umri wake.
 • Zingatia kumweleza ama kuuliza mambo pole pole ikilinganishwa na kumpuuza. Kama vile, badilisha mada badala ya kungoja ifike vipimo ambavyo havipendezi.
 • Mtie nguvu mtoto wako kuwa na ujasiri wa kibinafsi, na umhimize kufurahikia na kujieleza.
 • Ongea kuhusu hisia za mtoto wako na umsaidie kutumia maneneo kueleza hisia zake.
Wakati wa kumwona daktari:
 • Iwapo mtoto wako ana aibu ama amenyamaza baada ya kufika nyumbani kutoka shuleni, huenda ikawa ni ishara za kunyanyaswa.
 • Iwapo anaonyesha ishara za ukatili mwingi.

Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 4: Ukuaji na Hatua Muhimu

Ukuaji wa Lugha na Mazungumzo

Katika miaka 6 miezi 4, mtoto wako anaonyesha uwezo wa kuongea kwa ufasaha na ujasiri, huku akiunda sentensi zilizo kamilika.

Walakini, ni vyema kujua kuwa wakati ambapo mtoto wako huenda akaanza kuongea kwa sentensi ngumu zilizo kamilika, mhusihse kwenye ngumzo za watu wakubwa, huenda aka vipata vigumu kueleza mawazo yake ama matukio magumu.

Katika umri huu, ambapo mtoto wako mdogo huanza kueleza hamu yake ya kusoma na kuandika. Kwa hivyo, ni vyema kwa wazazi kuanzisha aina nyingi ya vifaa vya kusoma. Mchukue mtoto wako mdogo kwenye maktaba aweze kujionea kwa macho na ili mtumie adhuhuri yenu pamoja.

Hatua zingine muhimu za lugha na mazungumzo za kuangazia katika mtoto wako wa miaka 6 miezi 4 kwa sasa ni:

 • Anaanza ubishi mdogo.
 • Anafuata maagizo ya njia tatu, kwa mfano, "Tafadhali nawa mikono yako, kisha uweke vitabu mbali na uje ule chajio."
 • Anaanza kuona kuwa baadhi ya majina hukuwa na zaidi ya maana moja.
 • Tumia ngeli ya wakati huu na wakati uliopita kwenye sentensi.
 • Anaonyesha hamu ya kusoma na kuandika.
 • Anaanza kuona mfumo wa maneno.
 • Kwa kawaida anatumia majina ama nambari kinyume nyume.
Vidokezo vya ulezi:
 • Jaribu ujue wasimamizi wa shule ambapo mtoto wako anasomea na wazazi wake.
 • Endelea kumsomea mtoto wako, pia, mhimize akusomee. Ni sawa iwapo anafanya makosa na wala usikubali kumpuuza kwa haya.
 • Jihusishe katika kufanya kazi ya ziada ya mtoto wako, ila kama mwelekezi, kwa kusmaidia pale tu anapotaka msaada wako.
 • Jifunzeni maadili ya darasa. Mpe mtoto wako kazi ndogo ndogo kumsaidia kuongeza umakini wake ama maagizo mepesi ya kufuata.
 • Kuwa na mazungumzo kuhusu hamu za mtoto wako ama michezo anayo ipenda zaidi, inayo mhimiza kusikiza, kuitikia na kuuliza maswali.
 • Tumia kuhesabu kusaidia kusoma kwa mtoto wako ("wacha tuone iwapo unaweza fanya hivi kabla kumaliza kuhesabu 1 hadi 10.")

Wakati wa kumwona daktari:

Kuwa mwangalifu kuona mambo yafuatayo ambayo ni dalili za kutia woga.

 • Ana tatizika kusoma majina mafupi na sentensi nyepesi.
 • Ana gugumaa kwa sana.

child development 6 years 4 months old (1)

Afya na Lishe: Mtoto wako wa miaka 6 miezi 4

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 4 kwa sasa anakua kwa kasi na kuhakikisha ukuaji wa afya, ni muhimu kuhakikisha kuwa anapata aina zifuatazo za virutubisho. Mbali na haya, ni muhimu kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata viwango vifuatavyo vya virutubisho vinavyo hitajika kila siku.

Lishe na shughuli za kifizikia vina tangamana, kuwa haki kuhakikisha kuwa unamsaidia mtoto wako wa miaka 6 miezi 4 kupata angalau dakika 60 za shughuli za kifizikia kila siku.

Hasa na aina tofauti za vyakula vikuu vinavyopatikana sokoni, unaweza msaidia mtoto wako kupata uchaguzi bora wa mahitaji yake.

Vidokezo:

 • Wakati wote, hakikisha kuwa unachagua nafaka zilizo 100% badala ya vyakula vilivyo tengenezwa kutoka kwa ngano ama nafaka, " vyakula ambavyi vina nafaka za kutengeneza ndani yake.
 • Unapo tayarisha nyama ama vyanzo vingine vya iron kama vile mboga za majani mengi ama maharagwe. Una shauriwa kuvichanganya na chakula kilicho na idadi ya juu ya vitamini C kama vile viazi vitamu ama nyanya- vinasaidia mwili wa mwanao kuweza kutumia iron ile vyema zaidi.
 • Weka kiwango kidogo cha chakula kwa mtoto wako na umwongezee pale ambapo anaomba.
Watoto wa umri huu wanapaswa kula vitu vifuatavyo kila siku:

Mwongozo wa kila siku wa maziwa kwa mtoto wa miaka 6 ni angalau kalori 1,200, ukihusisha vyakula kutoka kwa familia tofauti vya virutubisho kama vile maziwa, protini na pia mboga na matunda.

Kwa ujumla, idadi ya kalori inayohitajika kwa wavulana na wasichana katika umri huu ni ifuatavyo:

 • Wavulana: 1782.0 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1672.0 Kcal/kwa siku
Familia ya maziwa

Mojawapo ya vikundi vya virutubisho muhimu kabisa kwa mtoto anaye kua ni maziwa. Mtoto katika umri huu anahitaji vikombe 2.5 vya maziwa ama yoghurt kwenye lishe yake. Hakikisha kuwa unachagua vyakula vyenye ufuta wa chini.

Jaribu baadhi ya uchaguzi wa kuhusisha maziwa kwenye lishe ya mtoto wako. Kama vile milk shakes ama saladi na mboga za kijani kama vile broccoli.

Mwaga jibini kwenye mboga, mayai ama pasta. Kuwa m-bunifu unapo kitengeneza chakula chako kwa kukitayarisha kwa njia tofauti.

 Familia ya protini

Kwa watoto wa umri wa miaka 6, CDC ina shauri angalau gramu 19 za protini kila siku. Kwa wazazi wanao kuwa na watoto wa kuchagua vyakula, usitie shaka!

Vyanzo vikuu vya protini ambazo watoto wadogo hufurahikia ni kama vile kuku ya kutayarishwa ya nyumbani, yoghurt, pizza zenye matunda, mayai ya kupiga na vinginevyo.

Familia ya matunda na mboga

Kwa kutumia ubunifu wa kiwango cha chini tu, unafanya jambo hili kuwa la kufurahikia kwako na mtoto wako wa miaka 6 na miezi 4! Hakikisha kuwa unamhusisha mtoto wako katika kazi zako za jikoni. Hakikisha una angalia jinsi jambo hili linamsaidia kukuza uwezo wake wa lugha na hesabu.

Mtoto wa umri huu anahitaji angalau kikombe 1 cha matunda na 1.5 vya mboga katika kila lishe.

Nafaka

Unapaswa kumwanzishia mtoto wako nafaka vyema. Unaweza mpatia ounsi 4 za nafaka kila siku. Huenda ikawa ni kikombe kimoja cha cereal zilizo tayari kuliwa, kipande kimoja cha mkate ama nusu kikombe cha pasta ama cereal zilizo pikwa. Hizi zote mara nne kwa siku.

Unaweza chagua nafaka, kama vile oatmeal, quinoa, mkate wa wimbi mzima, popcorn, mchele wa hudhurungi. Ila, hakikisha kuwa unapunguza nafaka zilizo tengenezwa kama vile wali, pasta ama mkate mweupe.

Kwa kifupi, hapa ni mahitaji ya mwanao ya kila siku (tazama hapo juu kuona viwango vinavyo hitajika):

 • Matunda: vikombe vitatu kwa wavulana; na vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 32.4 kwa wavulana; gramu 32.4 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)

Vidokezo: 

 • Mwanzishie matunda na mboga kama vyakula vidogo. Weka matundwa yakiwa yameoshwa, kukatwa na kuonekana kwa urahisi kwenye friji.
 • Tengeneza saladi nyingi mara kwa mara.
 • Ongeza mboga nyingi kwa nyama yako na pasta sauces.
Wakati wa kumwona daktari: Iwapo mtoto wako:
 • Ana uzito mdogo zaidi ama mwingi zaidi
 • Anatapika ama kunyongwa anapo kula

Chanjo na Maradhi ya Kawaida: Mtoto wako wa miaka 6 miezi 4

Nyingi kati ya chanjo za mwanao zinapaswa kuwa zimeisha katika umri huu. Wasiliana na daktari wako kwa chanjo za kawaida ambazo mtoto wako anahitaji kwa sana, kama vile flu shot.

Kadri mtoto wako anavyo kuwa shuleni kwa wakati mwingi, huenda akaugua ama akakosa maradhi ya kawaida kama homa na mafua. Pia, kuwa makini kuona upele unao ibuka kwenye mwili wa mwanao. Na cha muhimu zaidi, mtie moyo akwambie iwapo anahisi kujikuna mwili ama anahisi hayuko sawa.

Ni muhimu kwa wazazi kukumbuka kuwa watoto wote hushuhudia ukuaji tofauti. Kila mtoto ni wa kipekee. Inapofika kwa hatua muhimu, hii ni miongozo tu ila haipaswi kufuatwa kwa umakini.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kutibu matatizo ya kiafya yaliyo kawaida sana kwenye watoto- joto jingi, kukohoa na homa - fuata maagizo haya:

 • Kutibu joto jingi: Iwapo mtoto wako ana joto jingi hadi 38°C (100.4°F), unaweza jaribu matibabu machache ya kinyumbani. Tumia maji ya vuguvugu kumpaka mtoto wako, hasa iwapo ana joto jingi hadi 39 degree celsius. Mvalishe mtoto wako nguo nyepesi ili asibaki na joto jingi mwilini. Unapaswa kuhakikisha kuwa mtoto wako anakula vyema na ana maji tosha mwilini. Iwapo matibabu ya kinyumbani hatitafanya kazi, wasiliana na daktari wako kuhusu madawa ya kununua. Ila, kumbuka kuto tumia aspirin kwa watoto. Huenda ikasababisha Reye's syndrome - maradhi ya kutishi maisha ambayo yana athiri ubongo na maini.
 • Kutibu kikohozi: Mpe kijiko nusu cha asali nyeusi kama vile buckwheat, inayofanya kazi vyema kwa sababu ina idadi ya juu ya viungo vinakumbana na uongezeko wa kilo. Jaribu kumlisha mtoto wako supu ya kuku kwani ina uwezo wa kuosha mfumo wa mapua. Pia, unaweza mpatia mtoto wako maji moto ya sharubati ama chai iliyo pikwa na asali.
 • Kutibu homa: Kwa kawaida, homa inapaswa kuisha baada ya siku chache. Ila, iwapo haiishi, unaweza jaribu kutumia matibabu ya kinyumbani kama vile kuweka kifaa cha kupepeta hewa kwenye chumba cha mtoto wako. Karibu na yeye kusaidia kulegeza kifua chake. Inua kichwa cha mwanao kwa kutumia mto ama taulo iliyo kunjwa kumsaidia kupumua kwa urahisi.

Walakini, iwapo matibabu haya ya kinyumbani hayafanyi kazi, ni vyema kuwasiliana na daktari wako. Huenda akaagiza madawa ya kununua ambayo yata saidia kupunguza uchungu kwa mtoto wako mdogo.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako,

 • Ana joto jingi zaidi ya 39 degrees Celsius
 • Ana upele, vidonda ama kugwaruzwa kusiko kwa kawaida
 • Kulia mara kwa mara kuhusu kuumwa na mwili ama kichwa
 • Amekuwa akitapika ama kuendesha zaidi ya siku mbili

Vyanzo: WebMD, CDC, Webmd, Kidshealth, MSF

Mwezi uliopita: 6 years 3 months

Mwezi ujao: 6 years 5 months

Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio