Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 5

Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 5

Mtoto wako kwa sasa amekuwa mkubwa!

Inakaa kana kwamba ilikua jana ambapo mtoto wako alikuwa anakutegemea kufanya mambo yote. Ila kwa sasa, mtoto wako sio mdogo tena! Katika umri wa miaka 6 miezi 5, mtoto anajua anavyo endelea, kwa kina huenda akachukua jukumu la mtoto mzee!

Mtoto wako anazoea kuwa mbali na wazazi wake mara nyingi. Hata kama anataka kuonyesha kuwa ako tayari kuchukua majukumu mapya, huenda ukaona kuwa mdogo huyu anahitaji uangalifu wako anapokuwa nyumbani.

Tuangaze kwa kina hatua muhimu ambazo mtoto wako wa miaka 6 miezi 5 huenda akawa amefikisha.

Ila wazazi, tafadhali angazia kuwa hiki si kifaa cha kipimo ila ni mwongozo tu. Mtoto wako hukua katika mwendo wake ila unapaswa kuwa makini ukiona mambo yasiyo ya kawaida. Usikawie kuongea na daktari kupata ushauri iwapo una shaka zozote katika wakati wowote kwenye safari ya ukuaji wa mtoto wako.

Ukuaji na Hatua Muhimu Kwa Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 5: Je, Mtoto Wako Anakua Ipasavyo?

physical development at 6 years 5 months old

Ukuaji wa Kifizikia

Katika hatua hii, kimo cha uzito na urefu wa mtoto wako* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 118.3 cm (46.6 inchi)
  – Uzito: 21.8 kg (48 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 117.9 cm (46.4 inchi)
  – Uzito: 21.4 kg (47.1 lb)

Katika miaka 6 miezi 5, mtoto wako anataka kukuonyesha jinsi alivyokua kwa sasa. Mtoto wako ana ujasiri mwingi wa uwezo wake kwa sasa. Huenda ikahusisha mambo hatari kukuonyesha ama wanarika wake kukuonyesha uwezo wake. Ila, usitie shaka mama, haya yote ni kawaida. Hii ni ishara njema kuwa ukuaji wa mtoto wako unaendelea vyema.

Kuongeza hayo, watoto wengi katika umri huu wanahitaji kukata kilo nyingi za ufuta ulio mwilini hata ingawa huenda ikatukalia jambo la kuchosha kwetu.

Utagundua kuwa mtoto wako anaonyesha uwezo ulio imarika na pia kutangamanisha mikono na macho. Ataanza kuunganisha uwezo mwepesi kama vile kushika na kurusha mpira na michezo mingine ya kimakundi ya kifizikia. Huenda ikasababisha kujua mengi katika sehemu ya uchungu wa kifizikia kama vile kuumwa na tumbo, miguu na mengineyo.

Walakini, ukiangalia mtoto wako anapoteta kuhusu kuumwa na uchungu, huenda ikawa ni dalili ya matatizo makubwa ya kiafya, kwa hivyo kuwa mwangalifu haya yanapo tendeka.

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 5 anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya yafuatayo:

 • Kuanza kuandika herufi
 • Kuchora michoro iliyo kweli zaidi
 • Kutumia kamba ya kuruka kivyake
 • Kuruka kinyume nyume
 • Kujifunza jinsi ya kuendesha baiskeli
 • Kurusha mpira
 • Kuanza kupoteza meno ya watoto
Vidokezo vya ulezi:
 • Ratibisha lisaa limoja la michezo ya kifizikia kila siku kwa mtoto wako. Mwanzishie mtoto wako mtaala wa ziada ama kundi la michezo.
 • Unaweza mwanzishia mtoto wako darasa za kuogelea.
 • Mhimize mtoto wako kuanza kujifunza uwezo na shughuli anazo penda kufanya.
 • Mhusishe mtoto wako katika shughuli za kifizikia ambazo nyinyi wote wawili mnaweza fanya. Ni mfano mwema wa kuigwa ili awe hai zaidi kifizikia anapo endelea kukua.
Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo unafikiria kuwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 5 anabaki nyuma katika ukuaji wake, ongea na daktari iwapo mambo yafuatayo yatatendeka:

 • Mtoto wako anadhihirisha kupoteza kwa uwezo aliokuwa nao hapo awali ulio dhahiri
 • Kushindwa kufanya kazi nyepesi kama kuvalia nguo zake
 • Matatizo ya kulala usiku
 • Kukujoa kitandani hasa kama alikuwa amewacha hapo awali kisha kuanza tena

6 Years 5 Months Old

Ukuaji wa Kiakili

Ukuaji wa kiakili wa mtoto wako na kuelewa kwa mambo magumu kunaendelea kupanuka katika hatua hii. Tangu kuingia shuleni, utagundua kuwa mtoto wako anaweza kumbuka maagizo tofauti na kuwa makini kwa jambo kwa muda mrefu.

Hamu yake ya kujua mambo inaendelea kukua na kumsaidia kuwa na mazungumzo yenye maana zaidi. Ni kawaida anapo anza kuuliza maswali ili kupata maana na kuelewa zaidi dunia anayo ishi. Hali hii ya kuwa na maswali mengi kuna ashiria hamu isiyo toshelezwa ya mtoto wako kujua mambo mengi na kuwa na uwezo wa kutumia busara hii katika visa tofauti.

Kuwa mwangalifu kwa ukuaji huu katika mtoto wako:

 • Anaweza kumbuka maagizo ya sehemu tatau tofauti
 • Anaweza kuchora njia kutoka kwa kisa kigumu
 • Anaanza kuiga michoro migumu kama vile almasi
 • Kuuliza maswali ya maana
 • Huenda akawa na uwezo wa kurudia nambari tatu kinyume nyume
Vidokezo vya ulezi:
 • Mhimize mtoto wako kuuliza maswali na anapo kuuliza maswali, mwulize pia ili muwe na mazungumzo marefu.
 • Mpe mtoto wako nafasi asome kwa kuenda mahali ambapo hamja tembea hapo awali kama vile kwenye mbuga ama mahali pa kihistoria.
 • Jua nafasi mpya ambazo zita mpatia changamoto la kukua. Mfunze kuwa sio kuhusu kukua wakati wote, ila ni kuhusu kusoma mengi kuhusu kisa na kutumia busara hiyo maishani mwake.
Wakati wa kumwona daktari? Iwapo mtoto wako:
 • Tatizo la kusoma sentensi rahisi
 • Kushindwa kufuata maagizo rahisi
 • Halitambui jina lake
 • Tabia za kikatili zina anza kuonekana kupitia kuwagonga wengine mara kwa mara

making friends and being social at 6yrs 5 months old

 Ukuaji wa Muingiliano na Hisia

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 5 anachukulia kwa makini maoni ya watu wengine kuliko hapo awali. Anasoma jinsi ya kufanya kazi na wengine na kugawa vitu vyake. Mtoto wako mdogo anapata marafiki wapya, huenda ukagundua kuwa wavulana wanapenda kukaa na wavulana huku wasichana wanapenda kucheza na wasichana wenzao. Haya yote ni kawaida katika hatua hii wanapo endelea kujielewa zaidi.

Mtoto wako anapo endelea kuwa na marafiki zaidi, pia anasoma jinsi ya kujieleza kwa lugha hasa ikiwa ni kuhusu hisia zake. Wakati ambapo huenda mtoto wako anaendelea kusoma jinsi ya kuwa huru kuwaeleza wengine hisia zake, sio jambo geni kusikia akidanganya ili aende akacheze na wanarika wake. Watoto wanajaribu mambo tofauti yanayo kubalika na yale ambayo hayakubaliki.

Kwa ujumla, mtoto wako mdogo atahitimisha hatua zifuatazo katika umri huu:

 • Anaweza cheza peke yake ila anapenda kutafuta marafiki wake wacheze pamoja
 • Kuwaiga watu wazima
 • Kucheza na marafiki wake wa jinsia moja
 • Anafurahikia kucheza michezo ya kufuatana na marafiki wake
 • Anapenda kuwaonyesha wengine uwezo wake
 • Ana uwezo zaidi wa kujidhibiti
 • Kupunguka kwa mlipuko wa hisia
Vidokezo vya ulezi:
 • Tenga wakati wa kuongea na mtoto wako kuhusu mambo magumu kama vile kunyanyaswa, vurugu, kutumia madawa ya kulevya. Ongea kwa njia inayomfaa katika umri wake ili usimtie woga.
 • Weka mipaka ya wakati wa kutazama runinga ili isi adhiri michezo ya kifizikia, wakati wa familia ama kulala.
 • Weka dhibiti za mzazi kwenye runinga ama kompyuta kudhibiti vipindi vyovyote vya watu wazima.
 • Mhimize mtoto wako kufanya uamuzi wake kuhusu shughuli zake.
 • Mhusishe mtoto wako katika kazi za kinyumbani.
Wakati wa kumwona daktari:
 • Anapo dhihirisha ishara za kunyanyaswa ama aibu anapo fika nyumbani kutoka shuleni.
 • Kujitenga na watoto wengine
Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

Mtoto wako ana ujasiri wa kupiga ngumzo na wanarika wake na watu wazima kwa usawa, anaongea kwa kutumia sentensi mufti na kupeana majibu yanayo takikana.

Katika umri wa miaka 6 miezi 5, utagundua kuwa mtoto wako anaanza kupenda kusoma. Huenda hata akataka kukusomea unapo mpatia nafasi ya kukusomea. Unapo soma kitabu ambacho mtoto wako anakipenda, huenda akakueleza kinacho tendeka kwa hadithi hiyo na hata kukumbuka wahusika wengine.

Endelea kukuza upendo huu wa kusoma kwa kumwanzishia vitabu vipya baada ya muda kuongeza matamshi ya mtoto wako.

Ukuaji mwingine wa lugha na mazungumzo ambao huenda mtoto wako wa miaka 6 na miezi 5 akawa amefikisha ni kama vile:

 • Anaanza kugundua kuwa maneno fulani yana maana zaidi ya moja
 • Uwezo wa kuelewa ucheshi
 • Kuongea kwa sentensi zilizo kamilika zenye maneno kati ya matano na saba
 • Anafurahikia kusoma vitabu vya umri wake
 • Kuanza kuandika hadithi hasa kujihusu
 • Kusoma majina mengi zaidi, ila kwa kutumia majina ya kujiundia
 • Kuanza kuelewa herufi kubwa na vikomo kwenye sentensi
Vidokezo vya ulezi:
 • Endelea kuunda uhusiano na walimu na wasimamizi wa shule ya mwanao ili uweze kuelezwa jinsi anavyo endelea.
 • Tenga wakati zaidi wa mtoto wako kusoma.
 • Jitolee kumshauri na kumwonga anapo fanya kazi yake ya ziada, kwa kumsaidia. Mpe nafasi ya kufanya makosa.
 • Mpe maagizo machache yaliyo rahisi kufuata ili kukuza umakini wake.
 • Tumia njia tofauti kueleza matukio ama hadithi bora zaidi ambazo mtoto wako anazipenda ili kukuza maneno mapya.
 • Jaribu kuwa mcheshi kuashiria jinsi jina moja huenda ikawa na maana tofauti.

Wakati wa kumwona daktari:

Kuwa mwangalifu kuona ishara zifuatazo iwapo una shaka kuwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 5 huenda akawa anabaki nyuma katika ukuaji wake:

 • Ana taabika kusoma maneno mafupi ama sentensi rahisi.
 • Ana kigugumizi.
 • Hapigi ngumzo ama kuongea sana.

continue to give your child a balanced diet with essential nutrients and minerals

Afya na Lishe: Mtoto wako wa miaka 6 miezi 5

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 5 anaendelea kukua kiakili, kihisia na kifizikia. Kuhakikisha kuwa anakuwa kwa mwendo wenye afya, endelea kumlisha lishe bora iliyo na virutubisho na madini yanayo hitajika.

Mbali na kuendelea kupata michezo ya kifizikia ifaayp (angalau dakika 60 kila siku), mtoto wako pia anahitaji kula lishe bora kumpa nguvu anazo hitaji. Kama wazazi, kuwa mfano mwema wa kuigwa na watoto wako kwa kula chakula kinacho fanana!

Vidokezo: 

 • Tafuta vyakula vilivyo na nafaka asilimia 100 badala ya vyakula vilivyo tengenezwa kwa nafaka ama ngano. Aina ya kwanza ina afya na ni bora kwa mtoto wako.
 • Punguza kiwango cha chakula cha mtoto wako na ujitolee kumwongeza iwapo atahisi njaa.
 • Changanya vyanzo vya iron kama vile nyama na mboga, na vyakula vilivyo na kiwango cha juu cha vitamini. Vyakula kama nyanya ama viazi vitamu vinasaidia mwili kutumia iron vyema zaidi mwilini.
Watoto wa umri huu wanapaswa kula vyakula vifuatavyo kila siku:

Kwa ujumla, kalori zinazohitajika kwa wavulana na wasichana wa umri huu ni kama ifuatavyo:

 • Wavulana: 1789 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1678 Kcal/kwa siku

Mwongozo unao shauriwa wa lishe ya kila siku kwa mtoto wa miaka 6 ni angalau kalori 1,200, ukihusisha vyakula kutoka kwa familia tofauti za virutubisho kama vile maziwa, protine, matunda na mboga.

Familia ya maziwa

Mojawapo ya vikundi vya virutubisho muhimu kabisa kwa mtoto anaye kua ni maziwa. Mtoto katika umri huu anahitaji vikombe 2.5 vya maziwa ama yoghurt kwenye lishe yake. Hakikisha kuwa unachagua vyakula vyenye ufuta wa chini.

Unaweza ongeza maziwa kwa lishe ya mtoto wako kwa njia tofauti kama vile kuongeza cheese kwenye mayai na mboga zake. Kutumia yoghurt kwenye chakula chake pia ni njia bora ya kuongeza maziwa kwa lishe yake.

Baadhi ya wakati, chaguo rahisi hufanya kazi vyema zaidi. Weka maziwa kwenye chai ya mtoto wako badala ya kutumia maji moto.

Familia ya protini

Kwa watoto wa umri wa miaka 6, CDC ina shauri angalau gramu 19 za protini kila siku. Kwa wazazi wanao kuwa na watoto wa kuchagua vyakula, usitie shaka! Kuna vyanzo vya protini ambavyo mtoto wako anaweza furahikia. Hizi ni kama vile:

 • Mayai ya kupigwa/ kuchanganya
 • Yoghurt
 • Nyama ya nguruwe ama vipande vya kuku
 • Siagi ya njugu
 • Pasta ya mipira ya nyama
Familia ya mboga na matunda

Huenda mtoto wako akawa hapendi mboga, ila unaweza vichanganya kwenye vyakula vyake na avisherehekee bila ya juhudi nyingi. Rangi tofauti huenda zikafanya kazi unayo hitaji.

Kwa kifupi, hapa ni mahitaji ya mwanao ya kila siku (tazama hapo juu kuona viwango vinavyo hitajika):

 • Matunda: vikombe vitatu kwa wavulana; na vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 36 kwa wavulana; gramu 36 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)

Vidokezo: 

 • Mwanzishie matunda na mboga kama vyakula vidogo. Weka matundwa yakiwa yameoshwa, kukatwa na kuonekana kwa urahisi kwenye friji.
 • Tengeneza saladi nyingi mara kwa mara.
 • Mwanzishie mchanganyiko wa mboga kwa kila lishe.
Wakati wa kumwona daktari: Iwapo mtoto wako:
 • Ana uzito mdogo zaidi ama mwingi zaidi
 • Anatapika ama kunyongwa anapo kula
 • Ana joto jingi zaidi ya 39 degrees Celsius

Chanjo na Magonjwa ya kawaida: Mtoto wako wa miaka 6 na miezi 5

Mtoto wako wa miaka 6 na miezi 5 anapaswa kuwa amepata chanjo zifuatazo:

 • Chanjo ya DTaP inayo linda dhidi ya diphtheria, tetanus, na pertussis
 • Chanjo ya IPV inayo linda dhidi ya polio
 • Chanjo ya MMR inayo linda dhidi ya measles, mumps, na rubella
 • Chanjo ya Varicella inayo linda dhidi ya chickenpox
 • Flu shot inayo hudumiwa kila mwaka

Wasiliana na daktari wako kuona iwapo chanjo za mtoto wako zina afikiana na tarehe.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kutibu matatizo ya kiafya yaliyo kawaida sana kwenye watoto- joto jingi, kukohoa na homa - fuata maagizo haya:

 • Kutibu joto jingi: Iwapo mtoto wako ana joto jingi hadi 38°C (100.4°F), unaweza jaribu matibabu machache ya kinyumbani. Tumia maji ya vuguvugu kumpaka mtoto wako, hasa iwapo ana joto jingi hadi 39 degree celsius. Mvalishe mtoto wako nguo nyepesi ili asibaki na joto jingi mwilini. Unapaswa kuhakikisha kuwa mtoto wako anakula vyema na ana maji tosha mwilini. Iwapo matibabu ya kinyumbani hatitafanya kazi, wasiliana na daktari wako kuhusu madawa ya kununua. Ila, kumbuka kuto tumia aspirin kwa watoto. Huenda ikasababisha Reye's syndrome - maradhi ya kutishi maisha ambayo yana athiri ubongo na maini.
 • Kutibu kikohozi: Mpe kijiko nusu cha asali nyeusi kama vile buckwheat, inayofanya kazi vyema kwa sababu ina idadi ya juu ya viungo vinakumbana na uongezeko wa kilo. Jaribu kumlisha mtoto wako supu ya kuku kwani ina uwezo wa kuosha mfumo wa mapua. Pia, unaweza mpatia mtoto wako maji moto ya sharubati ama chai iliyo pikwa na asali.
 • Kutibu homa: Kwa kawaida, homa inapaswa kuisha baada ya siku chache. Ila, iwapo haiishi, unaweza jaribu kutumia matibabu ya kinyumbani kama vile kuweka kifaa cha kupepeta hewa kwenye chumba cha mtoto wako. Karibu na yeye kusaidia kulegeza kifua chake. Inua kichwa cha mwanao kwa kutumia mto ama taulo iliyo kunjwa kumsaidia kupumua kwa urahisi.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo mtoto wako,

 • Ana joto jingi zaidi ya 39 degrees Celsius
 • Ana upele, vidonda ama kugwaruzwa kusiko kwa kawaida
 • Kulia mara kwa mara kuhusu kuumwa na mwili ama kichwa
 • Amekuwa akitapika ama kuendesha zaidi ya siku mbili

Kumbukumbu: WebMD

Mwezi uliopita: 6 years 4 months

Mwezi ujao: 6 years 6 months

Vyanzo: Webmd, Kidshealth, MSF

Makala haya yamechapishwa tena kwa idhini ya  theAsianparent

Written by

Risper Nyakio