Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 6

Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 6

Kwa sasa kwani mtoto wako amefikisha miaka 6 miezi 6, unaweza azimia kuona ukuaji muhimu wa kufurahisha.

Kutoka siku ambayo mtoto wako alizaliwa hadi sasa, ambapo anaweza fanya kazi nyingi kwa kipekee, imekuwa safari ya kufurahisha kwako. Katika muda mfupi sana, mtoto wako wa miaka 6 miezi 6 anaendelea kukua. Ila, kuna mambo mengi sana ambayo mtayapitia katika safari hii.

Kuna baadhi ya ukuaji unao onekana kwenye mtoto wako wa miaka 6 miezi 6. Huenda ukashangaa iwapo anakua na kuendelea katika mwendo unaofaa. Wazazi, cha muhimu zaidi ni kuwa katika hatua hii, huenda mtoto wako akawa ana tatizika kufanya uamuzi ambapo anachagua kati ya chocolate na strawberry.

Ila, usitie shaka, haya yote ni baadhi ya ukuaji wa mwezi huu.

Katika makala haya, tuna angazia sehemu tofauti za ukuaji wa mtoto wako wa miaka 6 miezi 6. Wazazi, tafadhali kumbuka kuwa hiki si kipimo cha ukuaji ila ni mwongozo. Usisite kuongea na daktari wako iwapo una shaka zozote kuhusu ukuaji wa mtoto wako.

Tuna angazia kwa kina hatua muhimu ambazo mtoto wako wa miaka 6 miezi 6 anafikisha katika mwezi huu.

Ukuaji na Hatua Muhimu Kwa Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 6. Je, Mtoto wako anakua ipasavyo?

6 Years 6 Months Old Development and Milestones

Ukuaji wa Kifizikia

Katika umri wa miaka 6 miezi 6, uwezo wa kifizikia wa mtoto wako unawekwa kwa kipimo. Atafurahikia mazoezi mengi ya kifizikia kama vile kurusha mpira na kuruka kamba. Mtoto wako ako hai zaidi kuliko hapo awali na hii huenda ikakuza uwezo wake wa mwendo.

Wakati ambapo uwezo wa mwendo wa mtoto wako unaendelea kuimarika kupitia kwa matendo haya, unaweza tarajia kuwa uwezo wake wa mwendo umekua kwa sana. Unaweza pumzika mtoto wako anapo sugua meno yake na kumaliza shughuli zake za kuzingatia usafi wa mwili.

Wazazi, ingekua vyema zaidi kujua kuwa mtoto wako huenda akaanza kulia kuhusu maumivu ya kifizikia kama vile kuumwa na tumbo, uchungu wa miguu na kadhalika. Hii ni kwa sababu anauelewa mwili wake zaidi.

Katika umri wa miaka 6 miezi 6- ambapo ukuaji ni wa kasi sana- una tarajia urefu wa kawaida wa mtoto wako wa miaka 6 ni wa inchi 42 hadi 51. Uzito wa afya ni kati ya kilo 16 hadi 26.

Watoto katika umri huu kwa ujumla hukua kwa inchi 2.5 kila mwaka na pounds 4 hadi 7 kila mwaka.

Katika hatua hii, urefu na uzito wa mtoto wako* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 118.9 cm (46.8 inchi)
  – Uzito: 22.0 kg (48.4 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 118.5 cm (46.6 inchi)
  – Uzito: 21.6 kg (47.6 lb)

Tuna angazia ukuaji na hatua muhimu ambazo mtoto wako wa miaka 6 miezi 6 anafikisha:

 • Kufunga nyororo na vifungo kwa ustadi.
 • Kukata miundo isiyo sawa.
 • Kuandika herufi ndogo ndani ya vitabu vyake vya shule.
 • Kuchora mchoro wa zigizagi.
 • Kuruka juu na chini ya ngazi za nyumba.
 • Uwezo wa kuruka kinyume nyume.
 • Kushika mipira midogo.
 • Kufunga kamba za viatu.
Vidokezo:
 • Jihusishe kwa hamu nyingi katika yote ambayo mtoto wako anapenda kufanya.
 • Mwanzishie mtoto wako darasa za kuogelea na umfunze usalama wa moto.
 • Mnapokuwa nje, ni bora kuzuru mbuga pamoja na mtoto wako.
 • Tenga kando wakati wa kucheza na mtoto wako na umkubalishe mtoto wako kufanya uamuzi wa kile anacho taka kufanya na wakati wake.
Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo unafikiria kuwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 6 anabaki nyuma katika ukuaji wowote wa kifizikia, ni vyema kuongea na daktari. Kuwa mwangalifu kuona ishara za kutia wasiwasi katika ukuaji wa mtoto wako kama hizi:

 • Kupoteza uwezo ambao alikuwa nao hapo awali.
 • Kushindwa kufanya kazi nyepesi kama vile kujivalisha nguo.
 • Iwapo mtoto wako hapo awali hakuwa anaenda haja ndogo kitandani ila sasa anaanza. Kibofu cha mkojo hudhibitiwa na umri.
 • Ana tatizika kulala usiku ama kupata usingizi usiku.

Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 6

Ukuaji wa Kiakili

Kwa mtoto wa miaka 6 miezi 6, kuna nyeusi na nyeupe tu: mambo huwa mema ama mabaya, mazuri ama yakuhuzunisha. Na mtoto wakoa anaona mtoto mwingine kama rafiki wake wa dhati ama adui yake- yote kwa sababu anashindwa kuona ardhi iliyo katikati.

Utapata mtoto wako wa miaka 6 akijaribu kutumia uhuru wake, wa kufikiria na hisia. Katika umri huu, huenda ukagundua mabadiliko katika masomo ya mtoto wako, kutumia lugha na fikira badala ya kuona na kushuhudia.

Michezo ya kufikiria pia hupunguka kwa sana, mtoto wako anapo endelea kupata hamu zaidi ya mambo ya haki, na kutaka kushuhudia dunia kana kwamba ye ni mtu mkubwa.

Kuwa mwangalifu kwa dalili hizi kwa ukuaji wa mtoto wako:

 • Kuelewa zaidi chanzo na athari za uhusiano.
 • Kuimarika kwa kumbukumbu.
 • Kupanga vitu kulingana na saizi, muundo na rangi.
 • Kufanya hesabu rahisi kama vile kuongeza ama kupunguza.
 • Kudhihirisha ongezeko la hamu kujua kuhusu dunia na kuuliza maswali mengi.
 • Kufanya majaribio madogo kupima fikira zake.
 • Kupoteza umakini wake kirahisi.
 • Kusahau maombi mepesi na maagizo.
Vidokezo:
 • Kuwa mpole na mtoto wako na uelewe kuwa anajaribu kuelewa dunia anayo ishi.
 • Saidia kuweka vitu kwa mpango ili mtoto wako akue kwa mpango.
 • Changamoto mpya huenda zikawa za kuogofya kwa mtoto wako, hasa kwa sababu ya uwoga wa kuanguka. Hapa, itakusaidia sana kumpa usaidizi wako. Mkumbushe kuwa utakuwa naye wakati wote haijalishi yatakayo tendeka.
 • Mfunze mtoto wako kuwa ni sawa kukosea. Pia, mkubalishe mtoto wako kujaribu mambo mapya na asiwe na hofu ya kufanya makosa.
Wakati wa kumwona daktari? Iwapo mtoto wako:
 • Ana dhibitisha tabia za kikatili, hasa zinazo husika na kupigana, kurusha mateke ama kuwapiga ngumi wengine.
 • Anaonyesha tabia za kujitenga, woga ama kukwazwa kimawazo.
 • Ana tatizika kuongea ama kujiunga na watoto wengine kucheza.
 • Hatambui jina lake anapo itwa.
 • Anatatizika kutenganishwa nawe.
 • Matatizo kufuata maagizo ya pande mbili, "Weka mkoba wako mbali kisha ulete karo yako ya kadanda."

Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 6

Ukuaji wa Muingiliano/kijamii na Hisia

Inapofika kwa ukuaji wa kijamii na hisia wa mtoto wako wa miaka 6 miezi 6, michezo ya kimakundi ni muhimu sana kwa ukuaji wake wa kipekee kwani anapata usalama wake.

Kuhisi kana kwamba umetamatisha jambo ndicho kitu ambacho mtoto wako wa miaka 6 anataka kuhisi. Shughuli za kimakundi kama vile kupanda shamba pamoja huenda kukamfanya ahisi ametamatisha jambo.

Litakuwa jambo la kawaida kumwona mtoto wako akiwa huru kusema mambo tofauti katika miaka 6 miezi 6. Kwa ujumla, mtoto wako mdogo atakuwa ana ngoja wakati wake ufike.

Katika uso wa changamoto ambazo huenda zika ibuka, anapaswa kuwa wazi kuwa na mjadala na asisite kutangamana, kuweka akilini kuwa kuna mambo makubwa zaidi (ambayo ni kutimiza lengo la kundi).

Kwa ujumla, mtoto wako mdogo atatimiza hatua muhimu zifuatazo katika umri huu:

 • Ana makini zaidi katika kukuabilika na wanarika wake. Anasoma jinsi ya kutangamana na kugawa na wenzake.
 • Ana kuwa makini zaidi kwa urafiki na kufanya kazi kama kundi.
 • Anataka kukubalika na kupendwa na marafiki wake.
 • Ana taka kuhisi kana kwamba ametimiza.
 • Anajadiliana anacho taka badala ya kuwa na kichwa kigumu kuhusu mambo anayo yataka.
 • Anajilinganisha na wanarika wake.
Vidokezo vya ulezi:
 • Itasaidia kumwanzisha kwa vilabu kama vile girl ama boys scouts.
 • Punguza kumwagiza na umkubalishe mtoto wako kuwa na uwezo wa kufanya uamuzi kivyake.
 • Msifu mtoto wako.
 • Ongeza ujasiri na kujiamini kwa mtoto wako- kuna saidia unapo kuwa makini kwa uwezo wake, nguvu zake na kuzitambua.
 • Chagua kuwa mpole unapo mkanya mtoto badala ya kuwa mkali kama vile, kugeuza mada badala ya kungoja ishike kasi hadi isipokuwa ya kupendeza tena.
 • Mshike mkono mtoto wako na umpe ujasiri na umhimize kufurahikia na kujieleza.
 • Ongea kuhusu hisia za mtoto wako na yeye ili kumsaidia kuweka maneno kwa hisia hizi.

Wakati wa kumwona daktari:

 • Iwapo mtoto wako ana aibu ama amenyamaza anapofika nyumbani kutoka shuleni, huenda ikawa ni ishara ya kunyanyaswa.
 • Anapo dhibitisha ishara za ukatili.

speech and language development

Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

Katika umri wa miaka 6 miezi 6, mtoto wako anaingia kwa dunia mpya ya kuhadithiana na vitabu na kushuhudia.

Ubunifu wake unaongezeka kadri anavyo endelea kusoma vitabu na kupenda kuongea kuhusu mawazo yake na marafiki wake. Mtoto wako huenda akajieleza anavyo hisi kwa kupitia maneno ya kusemwa, kumkubalisha kuelewana vyema na watu wengine.

Ni wakati bora kwa wazazi kuwaanzisshia watoto vifaa tofauti vya kusoma. Mpeleke mtoto wako kwa maktaba ajionee kwa macho mnapo endelea kuwa na wakati mwema pamoja.

Kwa kuyaongeza tuliyo yasema, kuna hatua zingine muhimu za lugha na mazungumzo ambayo mtoto wako wa miaka 6 miezi 6 atafikisha katika mwezi huu:

 • Kuongea kwa sentensi rahisi zilizo kamilika za maneno kati ya 5 hadi 7.
 • Ongea naye kuhusu uwezo ama tabia zake (kwa mfano, naweza kula nyama kwa mara moja!).
 • Kuwa na mijadala midogo midogo.
 • Anafuata maagizo ya pande tatu, kama vile, "Tafadhali nawa mikono, weka vitabu vyako mbali kisha uje tule chajio."
 • Anaanza kuona baadhi ya maneno huwa na maana zaidi ya moja.
 • Anatumia ngeli ya sasa na iliyopita katika sentensi zake.
 • Anaanza kuona mfumo fulani katika maneno.
 • Kukiri maneno na nambari mara kwa mara.

Vidokezo vya ulezi:

 • Jaribu uwajue walimu na wasimamizi wa shule ya mtoto wako.
 • Endelea kumsomea mtoto wako, na umhimize akusomee. Ni sawa akifanya makosa na usimpuuze kwa kufanya makosa.
 • Jihusishe katika kazi ya ziada ya mtoto wako ila tu, pale anapo kuuliza umsaidie ama unapoona ni muhimu kuingilia kati.
 • Mfunze maadili ya darasa. Mpe mtoto wako kazi nyepesi kusaidia kuongeza umakini wake na kufuata maagizo machache.
 • Kuwa na mazungumzo kuhusu vitu anavyo penda kufanya ama pia michezo anayo furahia ama wanyama anao wapenda. Mhimize asikize, aitikie na kuuliza maswali.

Wakati wa kumwona daktari:

Kuwa mwangalifu kwa ishara hizi za kutia wasiwasi.

 • Anatatizika kusoma maneno mafupi sana ama sentensi rahisi.
 • Kugugumaa kwa sana.

miaka 6 miezi 6

Afya na Lishe: Mtoto wako wa miaka 6 miezi 6

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 6 anakuwa kwa kasi zaidi kuliko ulivyo dhania. Anahitaji nishati nyingi kumpa nguvu siku yote. Wakati ambapo kuna chaguo nyingi za kuchagua kutoka, ni muhimu sana kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata viwango vinavyo faa vya virutubisho vinavyo hitajika kwa siku.

Vidokezo:

 • Hakikisha kuwa nyumba yako imejazwa na vyakula vya afya kama vile matunda, mboga, yoghurt, maziwa na cheese. Fanya iwe rahisi kwa mtoto wako kuviona vyakula hivi na kuvifikia.
 • Punguza vinywaji kabla ya kula.
 • Azimia wakati mwema wa kula kadri iwezekanavyo.
 • Mbakishie peremende kwa wakati muhimu peke yake.
 • Mlishe kiwango kidogo cha chakula na umwongeze anapo itisha.

Hasa na vyakula vya aina nyingi zilizo kwenye soko, unaweza msaidia mtoto wako kufanya uamuzi bora zaidi wa chakula anacho kitaka.

Lishe na shughuli za kifizikia hutangamana kwa hivyo wazazi, hakikisha kuwa unamsaidia mtoto wako wa miaka 6 miezi 6 kupata angalau dakika 60 za michezo ya kifizikia kila siku.

Watoto wa umri huu wanapaswa kula vitu vifuatavyo kila siku:

Mwongozo wa kila siku wa maziwa kwa mtoto wa miaka 6 ni angalau kalori 1,200, ukihusisha vyakula kutoka kwa familia tofauti vya virutubisho kama vile maziwa, protini na pia mboga na matunda.

Kwa ujumla, idadi ya kalori inayohitajika kwa wavulana na wasichana katika umri huu ni ifuatavyo:

 • Wavulana: 1796 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1686 Kcal/kwa siku
Familia ya maziwa

Mojawapo ya vikundi vya virutubisho muhimu kabisa kwa mtoto anaye kua ni maziwa. Mtoto katika umri huu anahitaji vikombe 2.5 vya maziwa ama yoghurt kwenye lishe yake. Hakikisha kuwa unachagua vyakula vyenye ufuta wa chini.

Jaribu njia zifuatazo za kufanya kuongeza maziwa kwenye chakula cha mtoto wako ikae njia ya kufurahisha:

 • Yogurt popsicles
 • Banana smoothie
 • Rice cream pudding
 • Fettuccine carbonara
 • Date scones
 • Homemade strawberry frozen yoghurt
Familia ya protini

Kwa watoto wa umri wa miaka 6, CDC ina shauri angalau gramu 19 za protini kila siku. Kwa wazazi wanao kuwa na watoto wa kuchagua vyakula, usitie shaka!

Baadhi ya njia za kuhusisha vyanzo vya protini, ni kuongeza kwa vyakula hivi:

 • Kuongeza mbegu za ground flax seed kwa smoothies.
 • Badilisha oats na ngano kwa vyakula vya kubake.
 • Weka edamame (kama baadhi ya mboga za kijani). Ama uzibonde kisha uziweke kwa vyakula vingine.
 • Ongeza lentils nyekundu kwa supu na vyakula vingine ambavyo mtoto wako anapenda.
 • Badili vipande vya viazi vya kawaida na protini packed chip.
Familia ya matunda na mboga

Kwa kutumia ubunifu wa kiwango cha chini tu, unafanya jambo hili kuwa la kufurahikia kwako na mtoto wako wa miaka 6 na miezi 4! Hakikisha kuwa unamhusisha mtoto wako katika kazi zako za jikoni. Hakikisha una angalia jinsi jambo hili linamsaidia kukuza uwezo wake wa lugha na hesabu.

Mtoto wa umri huu anahitaji angalau kikombe 1 cha matunda na 1.5 vya mboga katika kila lishe.

Nafaka

Unapaswa kumwanzishia mtoto wako nafaka vyema. Unaweza mpatia ounsi 4 za nafaka kila siku. Huenda ikawa ni kikombe kimoja cha cereal zilizo tayari kuliwa, kipande kimoja cha mkate ama nusu kikombe cha pasta ama cereal zilizo pikwa. Hizi zote mara nne kwa siku.

Unaweza chagua nafaka, kama vile oatmeal, quinoa, mkate wa wimbi mzima, popcorn, mchele wa hudhurungi. Ila, hakikisha kuwa unapunguza nafaka zilizo tengenezwa kama vile wali, pasta ama mkate mweupe.

Kwa kifupi, hapa ni mahitaji ya mwanao ya kila siku (tazama hapo juu kuona viwango vinavyo hitajika):

 • Matunda: vikombe vitatu kwa wavulana; na vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 36 kwa wavulana; gramu 36 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)

Vidokezo: 

 • Changanya vyakula ambavyo mtoto wako anavipenda zaidi na mboga.
 • Mhusishe mtoto wako katika kuvitayarisha vyakula hivi.
 • Jaribu njia tofauti za kutayarisha vyakula tofauti: mashed, wali, vya kupakwa, kuchomwa. Angalia ni ipi ambayo mtoto wako anapenda kuwa nayo wakati mwingi.
Wakati wa kumwona daktari:
Unapaswa kumtembelea daktari, iwapo mtoto wako:
 • Ana uzito mdogo zaidi ama mwingi zaidi.
 • Anatapika ama kunyongwa anapo kula.
 • Hana hamu ya vyakula anavyopenda kuvila zaidi.
 • Ana shuhudia kupoteza hamu ya kula kuliko ilivyo kawaida.

Chanjo na Maradhi ya Kawaida: Mtoto wako wa miaka 6 miezi 6

Nyingi kati ya chanjo za mwanao zinapaswa kuwa zimeisha katika umri huu. Wasiliana na daktari wako kwa chanjo za kawaida ambazo mtoto wako anahitaji kwa sana, kama vile flu shot.

Kadri mtoto wako anavyo kuwa shuleni kwa wakati mwingi, huenda akaugua ama akakosa maradhi ya kawaida kama homa na mafua. Pia, kuwa makini kuona upele unao ibuka kwenye mwili wa mwanao. Na cha muhimu zaidi, mtie moyo akwambie iwapo anahisi kujikuna mwili ama anahisi hayuko sawa.

Ni muhimu kwa wazazi kukumbuka kuwa watoto wote hushuhudia ukuaji tofauti. Kila mtoto ni wa kipekee. Inapofika kwa hatua muhimu, hii ni miongozo tu ila haipaswi kufuatwa kwa umakini.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kutibu matatizo ya kiafya yaliyo kawaida sana kwenye watoto- joto jingi, kukohoa na homa - fuata maagizo haya:

 • Kutibu joto jingi: Iwapo mtoto wako ana joto jingi hadi 38°C (100.4°F), unaweza jaribu matibabu machache ya kinyumbani. Tumia maji ya vuguvugu kumpaka mtoto wako, hasa iwapo ana joto jingi hadi 39 degree celsius. Mvalishe mtoto wako nguo nyepesi ili asibaki na joto jingi mwilini. Unapaswa kuhakikisha kuwa mtoto wako anakula vyema na ana maji tosha mwilini. Iwapo matibabu ya kinyumbani hatitafanya kazi, wasiliana na daktari wako kuhusu madawa ya kununua. Ila, kumbuka kuto tumia aspirin kwa watoto. Huenda ikasababisha Reye's syndrome - maradhi ya kutishi maisha ambayo yana athiri ubongo na maini.
 • Kutibu kikohozi: Mpe kijiko nusu cha asali nyeusi kama vile buckwheat, inayofanya kazi vyema kwa sababu ina idadi ya juu ya viungo vinakumbana na uongezeko wa kilo. Jaribu kumlisha mtoto wako supu ya kuku kwani ina uwezo wa kuosha mfumo wa mapua. Pia, unaweza mpatia mtoto wako maji moto ya sharubati ama chai iliyo pikwa na asali.
 • Kutibu homa: Kwa kawaida, homa inapaswa kuisha baada ya siku chache. Ila, iwapo haiishi, unaweza jaribu kutumia matibabu ya kinyumbani kama vile kuweka kifaa cha kupepeta hewa kwenye chumba cha mtoto wako. Karibu na yeye kusaidia kulegeza kifua chake. Inua kichwa cha mwanao kwa kutumia mto ama taulo iliyo kunjwa kumsaidia kupumua kwa urahisi.

Walakini, iwapo matibabu haya ya kinyumbani hayafanyi kazi, ni vyema kuwasiliana na daktari wako. Huenda akaagiza madawa ya kununua ambayo yata saidia kupunguza uchungu kwa mtoto wako mdogo.Pia ni jambo la busara kumhimiza mtoto wako kuangazia usafi. Mhimize anawe mikono yake na pia kutumia kijitambaa cha kamasi.

Wakati wa kumwona daktari

Ni wakati wa kumtembelea daktari, iwapo mtoto wako,

 • Ana joto jingi zaidi ya 39 degrees Celsius
 • Ana upele, vidonda ama kugwaruzwa kusiko kwa kawaida
 • Kulia mara kwa mara kuhusu kuumwa na mwili ama kichwa
 • Amekuwa akitapika ama kuendesha zaidi ya siku mbili

Kumbukumbu: WebMD, CDC,  Kidshealth, MSF, Psychology Today, Livestrong

Mwezi uliopita: 6 years 5 months

Mwezi ujao: 6 years 7 months

Makala haya yamechapishwa na idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio